Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Rais wa Palestina Mahmoud Abbas Aomba Kutambuliwa na Ushiriki na Umbile Halifu la Kiyahudi katika Baraza la Umoja wa Mataifa

(Imetafsiriwa)

Habari:

Tarehe 23 Septemba 2022, Mahmoud Abbas, rais wa Mamlaka ya Palestina alikariri ombi lake la kutaka Dola ya Palestina kuwa mwanachama kamili wa Umoja wa Mataifa, na kuonya kuhusu kufifia matarajio ya amani na Israel, katika hotuba yake kwa Baraza Kuu mnamo Ijumaa. [UN News]

Israel "kwa kupitia sera zake zilizopangwa kabla na za kimakusudi, inaangamiza suluhisho la dola mbili," rais wa Mamlaka ya Palestina alisema katika hotuba yake kwa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. "Hili linathibitisha bila shaka kwamba Israel haiamini katika amani," aliongeza. "Kwa hivyo, hatuna tena mshirika wa Kiisraeli ambaye tunaweza kuzungumza naye."

Abbas, mwenye umri wa miaka 87, alisema Israel imekuwa katika kampeni ya unyakuzi wa ardhi katika maeneo yanayokaliwa kwa mabavu na ilikuwa inawapa wanajeshi "uhuru kamili" kuua au kutumia nguvu kupita kiasi dhidi ya Wapalestina. "Huu ndio ukweli: wao ni utawala wa kibaguzi," alisema. [English Al-Arabiya]

Maoni:

Huo ni uwakilishi wa kusikitisha wa rais wa dola ya Palestina, bila ya aibu au hadhi yoyote anasema, "Kwa hiyo, hatuna tena mshirika wa Kiisraeli ambaye tunaweza kuzungumza naye."

Je, “Israel” inawezaje kamwe kusifiwa kama mshirika?! Ni kwa wale tu ambao wamezoea kudhalilishwa mbele ya ulimwengu haswa mbele ya watu wake mwenyewe, ilhali huzungumza kwa niaba yake tu. Mshirika katika nini hasa?! Kuua? Kufuatilia? Uhangaishaji? Ukandamizaji wa watu wa Palestina?

Mithili ya omba omba anayeendelea kuomba tonge akijua wazi atakataliwa kwa ukali, Abbas hajui maana ya kujiheshimu - baya zaidi anachupa mipaka kwa kuifanya serikali yake kunyenyekea  kwa wazi na kwa siri kwa dola hiyo ya vamizi. Tukio la hivi punde lilikuwa huko Nablus, eneo la kutisha la vikosi vya usalama vya PA vikivamia Nablus kwa mtindo ule ule unaotumiwa na vikosi vya umbile la Kiyahudi (IDF).

Kisha katika onyesho la kihisia lakini la kusikitisha mbele ya Umoja wa Mataifa, Abbas alitangaza malalamishi yake ila tu kwa dola hiyo ya kihalifu kuyachana chana madai yake kupitia Balozi wa "Israel" katika Umoja wa Mataifa, Gilad Erdan, ambaye alielezea hotuba iliyotolewa Ijumaa na rais wa Mamlaka ya Palestina katika Umoja wa Mataifa kama ya "udanganyifu, uliojaa uongo na iliyo tenganishwa na uhalisia. Abu Mazen amethibitisha kwa mara nyingine kwamba wakati wake umekwisha." [I24News].

Huu hapa ni mtazamo wa "labeka bwana" kama inavyoonyeshwa na Abbas na wasaidizi wake - wanajua fika kwamba wanakataliwa waziwazi na bado wanajinyenyekesha kwa udhalilifu.

Hii ni tofauti kabisa na watu wa Palestina ambao wana hadhi ya kibinafsi na nguvu ya ndani na nje - kama ilivyotajwa hapo juu wakati PA ilipoiga onyesho la mbinu ya "Israeli" kuvamia Nablus - Wapalestina jasiri walirusha mawe kwa vifaru vya Vikosi vya Usalama vya PA wanaoelewa ushirikiano pamoja na umbile la Kiyahudi hufanywa kwa gharama ya Wapalestina.

PA inafungua njia kwa wahalifu wa Kiyahudi kuwaua na kuwaangamiza Wapalestina - PA ina damu mikononi mwake mithili ya umbile ya Kiyahudi kwa hivyo labda huo ndio "ushirikiano" wanapobeba vifaa na uratibu pamoja na wahalifu kuwafuata wanaume na wanawake wasafi wa Palestina pamoja na kuwapatia majasusi.

Kwa hiyo Abbas kuiomba Umoja wa Mataifa - taasisi inayolitambua na kulilinda kikamilifu umbile la kihalifu ... akiomba amani kutoka kwa mbwa mwitu wenye njaa - Abbas ni mbwa mwitu vilevile na Wapalestina wanalipia gharama ya kuwa wana-kondoo walio hatarini.

Palestina kamwe haitakombolewa na baraza lolote lililoundwa ugenini au kutambuliwa kwa mamlaka yoyote. Kinyume chake, kila wakala haswa Marekani na nchi za Ulaya zitalisaidia umbile hili halifu huku likifumbia macho uhalifu wa kudumu na unaoendelea dhidi ya wanadamu nchini Palestina.

Majeshi ya Waislamu - Dola ya Kiislamu katika muundo wa Khilafah Rashidah kwa njia ya Utume haitaacha juhudi zozote za kuwakomboa watu wa Palestina na ardhi zao. Bila shaka Dola ya Kiislamu haitajiruhusu kamwe kudhalilishwa au kulegeza msimamo mbele ya kamati yoyote ya kigeni iliyoundwa na Magharibi ili kupata kutambuliwa; mamlaka ya dola inayoongoza ambayo ndiyo itakayoamua iwapo dola nyingine inastahiki wakati wake. Dola ya Kiislamu itazikomboa ardhi zilizonyakuliwa na kuziregesha kwa wamiliki wake halali (ambao wamehamishwa kote ulimwenguni). Mwenyezi Mungu (swt) anaahidi,

(إِنَّ ٱلَّذِينَ يُحَآدُّونَ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُ أُو۟لَٰٓئِكَ فِي ٱلْأَذَلِّينَ * كَتَبَ ٱللَّهُ لَأَغْلِبَنَّ أَنَا۠ وَرُسُلِي إِنَّ ٱللَّهَ قَوِىٌّ عَزِيزٌ)

“Hakika wanao mpinga Mwenyezi Mungu na Mtume wake, hao ndio miongoni mwa madhalili wa mwisho. Mwenyezi Mungu ameandika: Hapana shaka Mimi na Mtume wangu tutashinda. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye kushinda.” [Al-Mujadalah 20-21]. Hakika Mwenyezi Mungu atawapa Waislamu ushindi na kwa hakika hiyo itakuwa ni nguvu ya kuzingatiwa pale zimwi lililolala litakapoamka kutoka katika usingizi wake mzito. Hivyo kuunda mfumo mpya wa kilimwengu na kutokomeza kabisa uvamizi wa kihalifu ya Mayahudi.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Manal Bader

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu