Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Musiwaunge Mkono Madhalimu

(Imetafsiriwa)

Habari:

Rais Recep Tayyip Erdogan anahudhuria Mkutano wa Wakuu wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO), ambayo inafanya mkutano wake wa 22, kwa mara ya kwanza. Ukweli kwamba Uturuki, ambayo si mwanachama wa shirika hili lakini ina ushirikiano wa kimazungumzo, itashiriki katika kupiga picha ya familia katika mkutano huo; Ni muhimu katika mfumo wa kuendeleza mahusiano na kuimarisha mazungumzo na shirika la usalama lenye nguvu zaidi barani Asia, linalojumuisha China, Urusi na India. (16.09.2022 Agencies)

Maoni:

Mkutano huo wa 22 wa Shanghai, ulioanza na kipindi cha janga na kuendelea na vita vya Ukraine na kufanyika katika kivuli cha mgogoro wa chakula na kawi ulimwenguni, unafuatilia kwa hamu na nchi za ulimwengu. Angazo la hamu hii ni kwamba Urusi inadhibiti sehemu kubwa ya gesi asilia na chakula muhimu kinachohitajika na nchi za Ulaya. Sera za ulinzi na vitisho zaidi za Warusi katika vita vya muda mrefu vya Ukraine bila shaka zinatishia zaidi nchi za Ulaya.

Kwa mara nyengine tena, ukweli kwamba mkutano huu unafanyika wakati ambapo Marekani inajaribu kuitenganisha Urusi na China ndani ya mfumo wa sera yake ya kuitenga Urusi, hasa katika masuala ya kiuchumi na kisiasa, imeongeza umuhimu wake zaidi kidogo. Wakati sera ya Amerika hadi sasa imewadhoofisha Warusi kijeshi, kisiasa na kiuchumi, imekuwa ni kuizuia China kuwa na utulivu katika mahusiano yake na Urusi. Bila shaka, haitarajiwi kwamba hili litaendelea kwa ushajiisho ule ule kwa muda mrefu. Ikiwa China haiwezi kushughulikiwa kwa michezo tofauti tofauti ya kisiasa.

Kwa hakika nukta kuu inayohitaji kushughulikiwa kwa ajili ya mkutano huu ni misimamo ya watawala ambao watu wao ni Waislamu, na kutokuwa kwao na kitambulisho... Kwa upande mmoja China ambayo imekuwa ikitekeleza mateso, mauaji ya halaiki, utengaji, mauaji yasiyo tarajiwa. Bila kuridhika na haya, haijiepushi na kukanyaga imani, maadili na matambiko ya Waislamu, na inavunjia heshima na utu wao kwa njia mbaya zaidi.

Kwa mara nyengine tena, kuweza kupiga picha za dhati na watawala wa Urusi ambao, pamoja na dhalimu Assad, wamekuwa wakiwachinja mamilioni ya Waislamu nchini Syria na kuwafanya kuwa wakimbizi kwa takriban miaka 10. Kila mtu alisikia kuhusu ukandamizaji wa watawala wa Uzbekistan na Kazakh, ambao wamueona kuwa unaostahiki kwa watu. Sio heshima bali ni aibu kujumuika pamoja na viongozi wa dola hizi za katili, kikafiri na kigaidi na kupiga nao pozi za ikhlasi. Zaidi ya hayo, Waislamu lazima wawe macho dhidi ya dhana za operesheni za wapambe wa makasri, wanaopigia debe umahiri wa kisiasa kutokana na aibu hii ya kisiasa.

Ijapokuwa ni ukweli kwamba kila mwenye akili timamu anaona kuwa mashirika, mapatano na taasisi zinaongoza na kuanzishwa na makafiri wa kimagharibi katika pande zote mbili za mashariki na magharibi, ni ala tu zinazohudumia maslahi ya makafiri, bali ni ukosefu tu wa kuona mbele kushiriki katika mashirika haya na kujitahidi kuhusishwa. Swali ambalo kila Muislamu anapaswa kuwauliza sasa ni hili. Je, haijatosha kuwa mumewaunga mkono makafiri? Je, haijatosha kwamba mumeshirikiana nao katika dhuluma na mauaji yao?

Kwa hakika, mambo ambayo Waislamu watayafurahia ni pozi ambazo watawala watazipiga upande wa waliodhulumiwa na dhidi ya madhalimu. Watawala ambao watakusanya majeshi yote dhidi ya makafiri kwa ajili ya tone moja la damu ya ndugu na dada zao Waislamu. Sio kuchafua mikono ya mkandamizaji wa Kichina kwa pesa zao chafu huku Turkestan Mashariki na ardhi nyenginezo mithili ya hiyo zikililia msaada. Ni kumchukulia Putin, aliye na damu ya mamilioni ya Waislamu mikononi mwake, kama adui kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Sio kufanya hibvi kwa niaba ya Amerika na Ulaya. Ni kuwapa mgongo wote na kuwa upande wa Waislamu. Hii ndio siasa ambayo kwayo munaweza kujivunia na ambayo mutapata thamani yenu.

Makhalifa, wanaoona ujasiri huu, fursa hii kama suala la imani, wanaoifanya tu hofu kuwa pekee kwa Mwenyezi Mungu, na wanaotoa mali zao kwa ajili ya Dini ya Mwenyezi Mungu, ndio watakaofanya hili. Maombi yetu kwa Mola wetu Mlezi ni kwamba azilete siku hizo, watu hao karibu nasi.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Ahmet SAPA

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu