Jumanne, 24 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/26
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Siasa za Hasina ni Kulinda Kiti chake cha Enzi kupitia Kuonyesha Utiifu kwa Dola Adui ya Kishirikina ya India

(Imetafsiriwa)

Habari:

Waziri Mkuu wa Bangladesh Sheikh Hasina atazuru India kuanzia Septemba 5 hadi 8, kwa lengo la kuimarisha uhusiano "wenye pande nyingi". Akitangaza ziara ya Hasina, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje Arindam Bagchi alisema atafanya majadiliano ya nchi mbili na Waziri Mkuu Narendra Modi na atawatembelea Rais Droupadi Murmu na Makamu wa Rais Jagdeep Dhankar. Hasina alizuru New Delhi mara ya mwisho mnamo Oktoba 2019. "Katika miaka ya hivi majuzi, pande zote mbili zimeendeleza uhusiano wa hali ya juu, pamoja na kiwango cha juu," Bagchi alisema. "Ziara inayokuja ya Waziri Mkuu Sheikh Hasina itaimarisha zaidi uhusiano wa pande nyingi kati ya nchi hizo mbili uliojengwa juu ya mafungamano imara ya kihistoria na kitamaduni na kuaminiana na kuelewana," alisema. Mafungamano jumla ya kimkakati kati ya India na Bangladesh yamekuwa yakiimarika katika miaka michache iliyopita. (The Business Standard, September 1, 2022)

Maoni:

Wasomi na wanasiasa wa kisekula wanaoongozwa na Awami wanaichukulia ziara ya Hasina nchini India kabla ya uchaguzi ujao wa kitaifa kuwa muhimu sana kwa Bangladesh na wanaifanyia kampeni kama mafanikio makubwa katika urafiki wa India na Bangladesh. Iwe ziara hiyo inaitwa uhusiano baina ya nchi mbili, au kwa ajili ya kuimarisha muungano wa kikanda au malengo ya kiuchumi, ni lazima iangaliwe kwa kuzingatia muktadha wa kijiografia wa eneo hilo, yaani, mkakati wa Marekani wa Indo-Pasifiki wa kuimarisha India ili kukabiliana na China na kuzuia kurudi kwa Khilafah Rashida ya pili katika eneo hilo. Kwa vile Sheikh Hasina, aliyeingia madarakani bila ya mamlaka ya wananchi hana ofa ya kuvutia ya kuwapa wananchi, matumaini yake pekee ni kupata baraka za India za kuendelea kuwa madarakani kwa kutabikisha ajenda ya kikanda ya mabeberu. Kutokana na hayo, tangu aingie madarakani mwaka 2008, Hasina amekuwa akikabidhi ubwana na mali ya kimkakati ya Bangladesh kwa India kwa jina la kile kinachoitwa maafikiano na makubaliano ya pande mbili moja baada ya nyingine. India tayari imepata mwanya wa kuzifikia sekta zetu za kimkakati na nishati kama vile bandari, kawi na ulinzi kupitia mikataba mingi ya kujiua wenyewe. Sheikh Hasina alipendekeza kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa India, Jaishankar, ambaye alizuru Bangladesh hivi karibuni, kukabidhi bandari kuu ya Bangladesh - Bandari ya Chittagong - kwa matumizi ya India! Hapo awali aliipatia India usafiri wake wa muda mrefu wa maji na ardhini dhidi ya ada za chini mno, na kuhatarisha miundombinu na usalama wa Bangladesh. Aliiwezesha kampuni za India kutumia sekta yetu ya huduma na maliasili ikijumuisha bandari, uchimbaji madini, mawasiliano ya simu, mitambo ya kuzalisha umeme, elimu na mavazi. Kwa sababu ya sera na tabia hii ya utumwa ya Hasina, India sasa inatia shinikizo ili kuondoa aina zote za ushuru na vizuizi vya kuingia kwa bidhaa za India kwenye soko la Bangladesh. Ni ukweli uliothibitishwa kuwa maslahi ya nchi na wananchi hayana thamani kwa serikali ya Hasina. Kwa hivyo kwa kujitenga na watu, Sheikh Hasina anapapatika sana kushikilia madaraka kupitia kuwafanya maadui zetu wa Makafiri-Washirikina waridhike. Tangu alipoletwa madarakani na dola za kigeni, amekuwa mtiifu kwa mabwana zake, akihudumia na kutekeleza ajenda zao nchini Bangladesh.

Serikali mhaini ya Hasina itaendelea kuhatarisha ubwana wa Ummah kupitia kukabidhi uchumi wetu, rasilimali za kimkakati na miundombinu kwa maadui hawa wa Makafiri-Washirikina hadi tutakapong'oa siasa ovu za khiyana za wanasiasa hawa waovu wa kisekula pamoja na mfumo wa tawala wa kisekula unaoungwa mkono na Magharibi. Hivyo basi, ili kukomesha utiifu wa Makafiri na Washirikina, watu wenye ikhlasi na wanasiasa wa nchi hii hawana budi kufanya kazi ya kurudisha mfumo wa kiulimwengu wa Kiislamu kupitia kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume iliyoahidiwa, itakayoondoa utawala wa Makafiri na Washrikina kutoka eneo hili milele. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

(هُوَ الَّذِىۡۤ اَرۡسَلَ رَسُوۡلَهٗ بِالۡهُدٰى وَدِيۡنِ الۡحَـقِّ لِيُظۡهِرَهٗ عَلَى الدِّيۡنِ كُلِّهٖ وَلَوۡ كَرِهَ الۡمُشۡرِكُوۡنَ)

“Yeye ndiye aliye mtuma Mtume wake kwa uwongofu na Dini ya haki ili ipate kuzishinda dini zote, ijapo kuwa washirikina watachukia.” [As-Saff: 9].

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Sifat Newaz
Mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Bangladesh

 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu