Jumatano, 25 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/27
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Watawala Wafisadi, na sio Uislamu, ndio Sababu ya Umma wa Kiislamu Kuporomoka Kisayansi

(Imetafsiriwa)

Habari:

Kampuni ya Marekani ya SpaceX ilifanikiwa kuzindua chombo cha uzinduzi aina ya Falcon 9, ambacho kilirusha takriban satelaiti 50 zaidi za Starlink kwenye obiti.

Hatua ya kwanza baada ya ndege hiyo kurudi salama Duniani. Ilikuwa tayari ni uzinduzi wake wa kumi. Roketi hiyo ilitua kwenye pedi ya utuaji inayoelea. (Chanzo: https://ru.euronews.com/2022/08/13/spacex-starlink-launch)

Maoni:

Huku ulimwengu wa Kimagharibi ukiwa umeanza kuvinjari anga kupitia makampuni binafsi ya kibiashara, sekta ya anga ya juu katika nchi za Kiislamu imekwama kabisa.

Watawala wa nchi za Kiislamu, kwa miongo mingi ya kuwa madarakani, hawajaweza kumudu teknolojia ya anga za juu, iwe katika nyanja ya misheni zenye ulinzi au zisizo na ulinzi.

Watu wenye fikra finyo wanaharakisha kuulaumu Uislamu kwa kuwa nyuma huko kwa ulimwengu wa Kiislamu.

Hapa, kwanza kabisa, ni muhimu kutambua kwamba maendeleo ya sayansi na teknolojia ni dhihirisho la utabikishaji wa mfumo fulani, mtazamo wa maisha, kwa mujibu ambao kwao jamii maalum ya watu inaagizwa.

Historia inatoa mifano mingi ya mlipuko wa kisayansi na kiteknolojia katika jamii fulani baada ya kutabanniwa kwa maadili fulani ya kimfumo.

Kwa hivyo, maendeleo ni jambo la pili ilinganisha na mfumo unaotabikishwa katika mujtamaa.

Ikiwa watu wanaoishi katika eneo fulani wanapata upanuzi wa kimfumo, baada ya muda tunakuwa mashahidi wa maendeleo ya haraka ya sayansi na teknolojia. Na kinyume chake, ikiwa mujtamaa unakabiliwa na mporomoko wa kimfumo, basi huonekana katika nyanja zake zote, ikiwemo maendeleo ya teknolojia.

Na hapa kimsingi sio muhimu kutoa mwanga juu ya msingi wa upanuzi huu wa kimfumo.

Kwa hivyo, kwa mfano, Uislamu uliwaongoza Waarabu wa Urabuni wa zama za kati kwenye upanuzi wa kimfumo, ambao kwa muda mno ulisababisha maendeleo yasiyo na kifani ya sayansi na teknolojia katika Khilafah ya Kiislamu. Waislamu hawakukubali tu mafanikio katika uwanja huu kutoka kwa watu wengine, lakini pia walichangia maendeleo ya sayansi ya ulimwengu.

Wakati karne kadhaa zilizopita, mataifa ya Ulaya yalipo tabanni wao wenyewe fikra ya kutenganisha dini na maisha kama msingi wa kimfumo, na kukomesha nguvu ya Ukristo inayowalemaza watu wao; hili pia lilisababisha uvumbuzi muhimu zaidi katika sayansi na teknolojia.

Hili pia lilitokea katika Urusi ya kilimo mwanzoni mwa karne iliyopita wakati fikra ya ukomunisti na ujamaa, ilipotabanniwa katika kiwango cha dola, iliugeuza Muungano wa Kisovieti kuwa moja ya dola yenye nguvu iliyoongoza kwa miaka 20 (kutoka 1917 hadi 1939).

Uhusiano kama huo kati ya maendeleo ya sayansi na mujtamaa kutabanni mfumo fulani unatokana na ukweli kwamba kila mfumo huonyesha njia fulani ya kukidhi mahitaji ya mujtamaa; mojawapo ni kutaka maendeleo ya kisayansi na kiteknolojia.

Kwa hivyo, urasilimali umepata maendeleo kwa kutoa uhuru kamili, usio na mipaka kwa mujtamaa. Mtazamo kama huo, baada ya udikteta mkali na udhibiti wa kanisa la Kikristo, ulipelekea kustawi kwa sayansi. Ni muhimu kutambua kuwa, madhara ya mtazamo huu yalikuwa ni kuzorota kabisa kwa vima vya kiroho, kimaadili na kiutu katika jamii hizi; kiashiria dhahiri ambacho ni karibu kuporomoka kabisa kwa taasisi ya familia katika nchi za Magharibi.

Ukomunisti umepata maendeleo kwa kutabikisha fahamu yake kwamba "mwanadamu ni mithili ya inzirani katika gurudumu." Udhibiti mkali ulianzishwa na dola, ambao kwa muda mfupi huenda ilisababisha maendeleo fulani, lakini baadaye dola ya ukomunisti ilianguka bila ya kufyatua risasi, chini ya uzito wa matatizo yaliyokusanyika kutokana na kwa mtazamo huu mbaya.    

Kwa hivyo, miundo ya serikali zilizotungwa na wanadamu bila shaka hupelekea ukweli kwamba baada ya kutoa kipengee kimoja chanya, kipengee chengine muhimu huharibiwa.

Ama kuhusu Uislamu, unayachukulia maendeleo ya sayansi kama suala la ulimwengu wote, la kawaida kwa watu wote, ambapo inaruhusiwa kuchukua elimu kutoka kwa watu wengine.

(أنتم أعلم بأمور دنياكم

“Nyinyi ndio mnaojua zaidi (ujuzi wa kiufundi wa) mambo ya dunia yenu.” (Muslim).

Aidha, Uislamu umeweka idadi ya sheria nyinginezo zinazochochea moja kwa moja maendeleo ya sayansi na teknolojia.

Kwa hivyo, kwa mfano, moja yao ni kanuni ifuatayo inayojulikana vyema:

Uislamu unayachukulia manufaa ya mujtamaa wa Kiislamu kuwa ni sadaka ya kuendele (Sadaqat al-Jariya), mchango ambao huleta thawabu kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa Muislamu hata baada ya kifo chake. Ugunduzi wa kisayansi pia unaangukia chini ya ufafanuzi huu.

Kwa hiyo, Waislamu hawakutafuta tu, kwa mfano, kuchimba kisima ili baada ya kifo cha mtu aliyechimba, kumletea malipo kutokana na matumizi ya watu, lakini pia walitafuta kufanya kitu katika uwanja wa uvumbuzi wa kisayansi, kwa sababu inajulikana vyema kuwa unarahisisha maisha ya kila siku ya mujtamaa.

Katika juhudi ya kiasi fulani kujiunga na sadaka ya kuendelea (Sadaqat al-Jariya), watawala wengi wa Kiislamu, makhalifa, walipanga na kufadhili vituo vya kisayansi na maabara, ambavyo vilikuwa pambo la mji mkuu wa Khilafah ya Kiislamu.

Kwa bahati mbaya, hatuwezi kuorodhesha hukmu zote za Sharia katika nyanja hii ndani ya mpangilio wa makala haya.

Ama kuhusu hali ya sasa ya kudidimia kwa sayansi katika ulimwengu wa Kiislamu, hii haitokani na Uislamu; kinyume chake, inafungamana na kutawala tawala za kiimla za kisekula zinazoungwa mkono na Magharibi, kupitia kuzikomesha katika mustakbali wa karibuni na kutabikisha fahamu za Kiislamu katika uwanja wa kuchochea sayansi, Waislamu wataweza tena kuregesha uongozi wao katika sayansi, teknolojia na uvumbuzi.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Fazyl Amzaev
Mkuu wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Ukraine

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu