Jumatano, 25 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/27
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Ni Nani Anayehudumiwa na Ukanda wa Nafaka Uliofunguliwa na Uturuki?

(Imetafsiriwa)

Habari:

Makubaliano yalitiwa saini jijini Istanbul kati ya Urusi na Ukraine kupitia upatanishi wa Umoja wa Mataifa (UN) na Uturuki kwa ajili ya kuregesha mauzo ya nafaka kutoka bandari za Ukraine. Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ambaye alitoa hotuba kabla ya kutia saini, aliitathimini siku hii ya kutiwa saini kwa makubaliano ya nafaka kama "siku ya kihistoria", na kusema kwamba makubaliano hayo yatachangia kuzuia njaa ambayo inawasubiri mabilioni ya watu kote duniani. (VOA ya Kituruki, Julai 22, 2022)

Maoni:

Suala la kizuizi kilichotekelezwa na Urusi kwa meli zilizojaa nafaka zilizokuwa zikisubiri kwenye bandari za Ukraine kujibu vikwazo vya Amerika na Muungano wa Ulaya, lilitatuliwa kwa muda na Mkataba wa Ukanda wa Nafaka uliotiwa saini kupitia upatanishi wa Uturuki. Kulingana na makubaliano hayo, tani milioni 20 hadi 25 za nafaka zilizozuiliwa nchini Ukraine zinaweza kusafirishwa nje. Usafirishaji nje wa nafaka na mbolea wa Urusi ambazo zilizuiliwa kwa sababu ya vikwazo hivyo dhidi ya Urusi, utafanywa kuwa rahisi tena.

Baada ya makubaliano hayo, Marekani ikiwa katika nafasi ya kwanza, Umoja wa Mataifa, NATO, Muungano wa Ulaya na Urusi walielezea kuridhika kwao na kuishukuru Uturuki. Na Uturuki ililileta suala hilo katika upande wa hatari ya njaa na mwelekeo wa kibinadamu, na kujaribu kuficha dori yake maalum ya kisiasa iliyotolewa na Amerika. Ile inayoitwa dori ya Uturuki ya kisiasa, ni pamoja na kuwa nchi ya upatanishi ambayo inaweza kuanzisha mazungumzo na Urusi kunapokuwepo na maendeleo ambayo yanaweza kukatiza mipango na masilahi ya Amerika katika mchakato wa uvamizi wa Urusi nchini Ukraine. Kuingilia kwake mamlaka yake ya kisiasa kuhusiana na mzozo wa nafaka na matokeo ambayo imepata ni kielelezo tosha cha dori ya Uturuki. Kwa kauli yake "Uturuki iko tayari kucheza dori yoyote iwezayo katika kupunguza taharuki kati ya Urusi na Ukraine. Tunafanya hivi kama mshirika wa Urusi na Ukraine, pamoja na ukweli wa kuwa mshirika wa NATO. (Turkiye Gazetesi 20.01.2022), Msemaji wa Rais Ibrahim Kalin alikuwa ametamka rasmi dori ya kimataifa iliyopewa Uturuki wakati wa hotuba yake katika jopo lililofanywa na taasisi ya wasomi ya London iitwayo Circle Foundation, mwezi mmoja kabla ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

Kwa hakika, kwa makubaliano yaliyotiwa saini jijini Istanbul kwa mipango ya Uturuki, Urusi imezuiwa kutumia suala la nafaka kama turufu ya kisiasa kama ilivyofanya katika suala la mafuta na gesi asilia.

Ingawa Urusi ilisema kuwa ilifurahishwa na makubaliano hayo, iliishambulia bandari ya Odessa ya Ukraine siku moja baadaye, na kutuma ujumbe kwamba itatumia suala la nafaka kama turufu wakati wowote inapotaka. Inashangaza sana kwamba wakati Wizara ya Ulinzi ya Uturuki ilikuwa ikijaribu kukwepa hali hiyo kwa kusema Urusi haikubali shambulizi kwenye bandari ya Odessa, Urusi ilisema wazi kwamba ilifanya shambulizi hilo. Kwa sababu Uturuki inajua kwamba kufeli kwa makubaliano kutasababisha mshikamano kati ya Marekani na Ulaya. Na Urusi inafikiri kwamba wakati mzozo wa nafaka unapoendelea, matatizo ya kiuchumi ya Ulaya yataongezeka zaidi na kwa njia hii itaweka shinikizo kwa Amerika katika suala la kuhafifisha vikwazo dhidi ya Urusi. Kwa sababu mfumko wa bei ambao umepanda hadi asilimia 9 katika eneo la Euro unawakera watu wa Ulaya. Kwa hiyo, kupitia njia ya mgogoro wa nafaka, Urusi ilionyesha nukta mbaya za Ulaya na imeonyesha nini inachoweza kufanya. Na kupitia njia ya makubaliano yaliyotiwa saini jijini Istanbul, imeondoa vikwazo vilivyowekwa kwa nafaka, mbolea na bidhaa zinazotokana nazo zake yenyewe kando na nafaka za Ukraine.

Ama Marekani, imeshindwa kutimiza ahadi zake kwa Ulaya kwa badali ya kuandamana nayo katika vita vya Urusi na Ukraine. Kwa sababu gharama ya vita vya Urusi-Ukraine hailipwi na Marekani, bali na nchi za Muungano wa Ulaya, zinazoitegemea Urusi katika uwanja wa nishati na chakula. Kwa sababu hii, kutatua mzozo wa nafaka ni muhimu kwa Ulaya kuendelea kusonga katika mzunguko wa Amerika. Hata hivyo, inasikitisha kwamba maslahi haya muhimu ya makafiri wa kikoloni Marekani yanatekelezwa na Uturuki kwa kujificha nyuma ya hoja za kibinadamu. Hata hivyo Uturuki hiyo hiyo haikuchukua hatua yoyote wakati miji waliyokuwa wakiishi watu wa Syria ikizingirwa na Urusi kafiri na utawala wa Assad. Kwa mara nyengine tena, Uturuki haikucheza dori yake muhimu leo ​​wakati maelfu ya Waislamu nchini Syria walipokufa kwa njaa kwa sababu hawakupata chakula. Na msaada wa Umoja wa Mataifa ulikuwa kutuma mifuko ya maiti kwa watu wa Syria.

Kwa hivyo, Mkataba wa Ukanda wa Nafaka uliotiwa saini jijini Istanbul sio kulinda watu kutokana na hatari ya njaa, bali kulinda masilahi ya Amerika na Magharibi kafiri. Kwa sababu dola zinazotabanni mfumo wa kirasilimali kamwe hazifikirii juu ya wanadamu. Katika ulimwengu leo ambao wanatawala, watu milioni 821 wamehujumiwa kwa njaa. Kitu pekee ambacho ni kitakatifu kwao, ni maslahi yao ya kikoloni na utawala fisidifu.

Na dola pekee itakayomchukulia mwanadamu kama mwanadamu na kuiokoa dunia kutokana na migogoro bandia iliyotengenezwa na makafiri wakoloni, ni Dola ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume ambayo ni nembo ya rehma, kukithiri na uadilifu.

(وَاِذَا ق۪يلَ لَهُمْ لَا تُفْسِدُوا فِي الْاَرْضِۙ قَالُٓوا اِنَّمَا نَحْنُ مُصْلِحُونَ)

“Na wanapo ambiwa: Msifanye uharibifu ulimwenguni. Husema: Bali sisi ni watengenezaji!” [Al-Baqarah: 11]

 

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari Hizb ut Tahrir na
Muhammed Emin Yıldırım

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu