Jumatano, 25 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/27
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Uongozi wa Kisiasa na Kijeshi wa Pakistan Uko katika Ukurasa Mmoja Kuhusiana na Kujisalimisha kwa Chombo cha Amerika, FATF

(Imetafsiriwa)

Habari:

Mkuu wa Majeshi ya Pakistan (COAS), Jenerali Qamar Javed Bajwa, mnamo Ijumaa tarehe 17 Juni alilitaja tangazo la Jopo Kazi la Kifedha (FATF), kama "mafanikio makubwa" kwa Pakistan. Mkuu huyo ilisema ilikuwa ni "juhudi kubwa" ambayo ilifungua njia kwa nchi “kuwekwa katika orodha nyeupe”. Alisema zaidi kwamba kiini kikuu cha Makao Makuu (GHQ) kiliongoza juhudi za kitaifa za timu ya kijeshi na kiraia ambayo iliunganisha nishati ya utabikishaji wa mpango wa utendakazi.

Maoni:

Ingawa Pakistan haijaondolewa rasmi kutoka kwa orodha ya kijivu ya FATF, inaweza kuondolewa, mara tu shirika hilo litakapozuru Pakistan. Pakistan iliwekwa kwenye orodha ya kijivu mnamo Juni 2018 na kupewa mpango wa utendakazi wa nukta 34 na FATF. Baadhi ya nukta kutoka kwa orodha ya mahitaji ya FATF ni pamoja na; kuhakikisha ushirikiano wa kimataifa katika uchunguzi na hukumu dhidi ya mashirika na watu waliopigwa marufuku, kuyashtaki mashirika na watu waliopigwa marufuku, maonyesho ya mashtaka kutoka mahakama ya sheria ya mashirika na watu waliopigwa marufuku na ugeuzaji wa madrasa za Kiislamu kuwa shule na vitengo vya afya.

Nukta hizi zaonyesha wazi wazi lengo la FATF. Ni kuondoa uungaji mkono wa kimwili na kifedha kwa Jihad katika Kashmir Iliyokaliwa kimabavu, pamoja na kukandamiza ufahamu unaoongezeka kuhusu kuhukumu na Uislamu. Orodha zilizotolewa kwa Pakistan za mashirika na watu waliopigwa marufuku zilikuwa hasa za wale waliohusika katika Jihad dhidi ya majeshi ya India katika Kashmir Iliyokaliwa kimabavu, lakini pia ilijumuisha Hizb ut Tahrir, ambayo inafanya kazi ya kusimamisha tena Khilafah.

Hapa swali linaibuka. Kwa nini FATF inajali sana kuhusu mashirika na watu hawa mahususi? Ni wazi kwamba FATF ni chombo chengine cha kikoloni cha Marekani cha kulazimisha mataifa mengine kuhakikisha utabikishaji wa mipango yake ya kimataifa na kikanda. Katika kanda yetu mpango wa Amerika ni kuimarisha India, ili iweze kutekeleza mpango wa Marekani wa kupunguza nguvu na ushawishi wa China pamoja na Waislamu. Na juu ya yote, inataka kukwamisha uregeshaji wa Khilafah.

Sakata ya FATF imeweka wazi kuwa katika mfumo wa sasa wa ulimwengu wa dola za kitaifa, ubwana wa kitaifa ni udanganyifu tu. Licha ya kuwa na jeshi la saba kwa ukubwa duniani, lenye kombora la nyuklia na makombora ya balistiki, Pakistan haina sera huru ya kigeni au ya kiuchumi. Kushikamana na FATF kwa hakika ni khiyana dhidi ya Waislamu wa Pakistan, Kashmir Inayokaliwa kimabavu na kanda hii, pamoja na wajibu wa kuhakikisha utawala wa kimataifa wa Uislamu, kupitia Khilafah.

Suala hili limethibitisha kwamba uongozi wa kijeshi na kisiasa, ikiwemo PML-N, PPP na PTI, ni watumwa wa Marekani. Wote walidai kuhusika na Pakistan kutoka kwenye orodha ya kijivu, akiwemo mkuu wa jeshi, Qamar Javed Bajwa, Waziri Mkuu Shahbaz Sharif na Waziri Mkuu wa zamani, Imran Khan. Ni wazi kwamba hakuna tofauti ya maoni kati ya uongozi wa kisiasa na kijeshi, linapokuja suala la kufuata maagizo ya Marekani. Ugomvi wowote tunaouona kati yao ni siasa za madaraka tu, ambapo mshindi anakuwa mtumishi muhimu wa Marekani.

Wale ambao kwa hakika wanataka kuwa watawala na kukomesha utumwa wa Marekani, lazima wasimamishe tena Khilafah kwa Njia ya Utume nchini Pakistan. Khilafah inayokuja hivi karibuni itapindua mfumo wa sasa wa dunia wa dola za kitaifa, na kuunganisha ardhi zote za Waislamu chini ya Khilafah moja, kwa wakati ambao Mwenyezi Mungu (swt) atauchagua. Huu ndio msimamo pekee wa kuwa na maisha ya heshima katika dunia hii. Misimamo mengine yote inahakikisha kudumu kwa mfumo wa Marekani, na kutuzamisha katika udhalilifu na mateso.

]اَفَحَسِبۡتُمۡ اَنَّمَا خَلَقۡنٰكُمۡ عَبَثًا وَّاَنَّكُمۡ اِلَيۡنَا لَا تُرۡجَعُوۡنَ]‏

“Je! Mlidhani ya kwamba tulikuumbeni bure na ya kwamba nyinyi kwetu hamtarudishwa?” [Surah Al-Mu’minun 23:115].

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Mhandisi Shahzad Shaikh
Naibu Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu