Jumatano, 25 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/27
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Rais Mpya: Hali Imebakia Kama Ilivyokuwa nchini Somalia

Habari:

Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud mnamo Alhamisi alichukuwa uongozi kwa mara ya pili, akiahidi kuyaunganisha makundi yaliyogawanyika nchini mwake, pamoja na kuleta uhusiano mwema na majirani zake baada ya miaka mingi ya mizozo. Mohamud, alipochukua uongozi kutoka kwa Mohamed Farmaajo, alisema kuwa nchi yake itachukua msimamo wa kati na kati katika masuala ya kimataifa, huku ikijikurubisha kwa nchi zinazo heshimu ubwana wake na kutafuta suluhisho kwa matatizo ya pamoja kama al-Shabaab na umasikini. “Tukio tunaloshuhudia leo [kutawazwa kwake] ni mfano wa kukita kwa demokrasia katika taasisi nchini Somalia,” alisema, alisisitiza kwamba isipokuwa pale ambapo nchi ilikuwa chini ya utawala wa kijeshi kwa miaka 21 (1969 – 1991), Wasomali wamekuwa wakiegemea demokrasia. (The EastAfrican, Ijumaa, 10 Juni 2022).

Maoni:

Vyombo vya habari nchini, kieneo na kimataifa vimepongeza uhamishaji wa mamlaka kwa amani kutoka utawala wa zamani hadi mpya. Kiujanja, vimefeli kutaja kwamba rais mpya haleti lolote jipya kuhusiana na sera wala sheria kando na kumakinisha hali iliyoko sasa inayoikumba Somalia. Mwanzoni, alikuwa uongozini kutoka mwaka 2012 – 2017 kipindi ambacho Somalia ilishuhudia mtafaruku mkubwa wa kisiasa, kiuchumi na kijamii na ambao unaendelea hadi sasa. Rais mpya anaingia uongozini kwa mara ya pili, akiwa mwingi wa ahadi lakini ni porojo tupu.

Somalia inakumbwa na matatizo mengi ambayo yanahitaji utatuzi wa kweli na dharura. Baadhi ya matatizo yanajumuisha ukame wa kujirudia ambao unaendelea kuwadhikisha watu. Uporaji wa kupindukia wa rasilimali za umma kupitia kampuni za kigeni ambazo zinafanya miamala ya kisiri na walioko mamlakani. Ufadhili na uchocheaji wa kimakusudi wa makundi ya kisilaha na mizozo ya kikabila kupitia mikono ya wageni ambao hunufaika kwa ukosefu wa usalama endelevu nchini Somalia ni tatizo jingine kubwa.

Utawala mpya HAUWEZI kattu kusuluhisha changamoto hizo hapo juu, kwa sababu msingi wa utawala wenyewe unahitaji kubadilishwa. Hakika, hali imebakia kama ilivyokuwa nchini Somalia kwa kuwa utawala mpya ni muendelezo wa nidhamu ya sumu iliyopo na ambayo msingi wake ni mfumo wa kisekula wa kirasilimali.  Nidhamu ya utawala ambayo imeiweka mbali dini kuhusiana na masuala ya utungaji sheria! Hivyo basi, imeipa kipaumbele akili ya mwanadamu yenye kikomo katika kusimamia mambo ya watu kwa kutegemea kubahatisha waliko kuchukua kutoka kwa mabwana zao wakoloni Wamagharibi.

 Kwa hiyo, watu nchini Somalia wameruka kutoka katika kikaango kimoja kwenda kingine, kwa kuwa suala la dharura zaidi linalohitaji utatuzi ni kubadilisha nidhamu ya uongozi ya kisekula ya kidemokrasia ambayo inatanua kupitia fujo na uchafu. Badala yake kuweka katika sehemu yake nidhamu ya utawala ya Kiislamu ya Khilafah, nidhamu inayochipuza kutoka kwa Muumba wa ulimwengu, mwanadamu na uhai kwa maana Mwenyezi Mungu (swt). Khilafah hainasibishwi na wakoloni Wamagharibi ambao wanaushawishi katika sera ya ndani na nje kama inavyofanyika nchini Somalia na kwingineko duniani. Kwa mfano, uchaguzi wa hivi juzi wa urais ulifanyika mnamo Mei 2022 kama natija ya msukumo ili kutimiza masharti ya kigeni yaliyowekwa na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) ili kuiwezesha Somalia kupata kitita cha dola milioni 400 kama msaada ikiwemo ahadi nyingine za kutoka ng’ambo! (Reuters, 16 Mei 2022).

Hivi sasa Somalia inataabika kutokamana na kukosekana uongozi wa Kiislamu. Wale walioko mamlakani sio chochote bali ni watawala vibaraka wa wakoloni Wamagharibi. Kuwepo kwao madarakani ni kwa ajili ya kulinda maslahi ya mabwana zao na kutekeleza sera wanazochorewa kutoka katika miji mikuu ya Wamagahribi hususan Washington na London. Muonekano wao kiinje na wawenzao kutoka Mashariki ya Kati na ulimwengu wa Waislamu kwa ujumla huwahadaa watu kwamba wao ni ngao na walinzi wa kweli wa Waislamu na Uislamu. Alas, sio wa kweli, kwa kuwa hawana utambulisho wa Kiislamu kwa maana wanavyofikiria na kutenda ni kinyume na maamrisho ya Uislamu kama ilivyoletwa na Mtume (saw).

Kinyume chake, Khilafah itaongozwa na mwanamume Muislamu, Khalifah ambaye atajituma usiku na mchana kutekeleza nidhamu za Kiislamu zinazochipuza kutoka kwa Shari’ah ya Kiislamu ambayo inadhamini utulivu na ustawi kwa wote pasi na kuzingatia rangi, kabila wala dini. Pia, atakuwa ndiye mlinzi na ngao kwa walioko chini yake na hususan heshima ya Mtume (saw) ambayo inakejeliwa hadi leo na maadui wa Uislamu na Waislamu. Hali ya kusikitisha ya Somalia itadumu, mpaka pale ambapo Waislamu wa kweli ndani na nje watatambua makosa ya kimsingi ya kubeba mfumo wa kisekula wa kirasilimali, na kuanza kufanyakazi na Hizb ut Tahrir ili kurudisha tena maisha ya Kiislamu kwa kusimamisha Khilafah kwa njia ya Utume. Wakati ni sasa, upatilize na hautojuta.

Imeandikwa kwa ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Ali Nassoro Ali

Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu