Jumanne, 24 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/26
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Ufyatuliaji Risasi wa Shule Eneo la Uvalde, Texas, Amerika

Serikali Iliyosambaratika Kuanzia kwa Katiba Yake

(Imetafsiriwa)

Habari:

Ufyatuliaji Risasi katika Shule ya Msingi ya Robb, Uvalde, Texas, Amerika

Mauaji ya kinyama katika shule moja ya msingi ya Texas yamevuta hisia tena kwa hamasisho lenye nguvu la kumiliki bunduki nchini Marekani, huku maafisa wa chama cha Democratic wakiwalaumu wabunge wa chama cha Republican kwa kubaki kuwajibika kwa maslahi yenye ushawishi ya waungaji mkono wa bunduki ambayo watetezi wanasema yamekwamisha mageuzi ya kitaifa ya bunduki. Rais Joe Biden, akizungumza saa chache baada ya kijana mwenye bunduki mwenye umri wa miaka 18 kuvamia Shule ya Msingi ya Robb huko Uvalde, Texas, na kuwaua kwa kuwapiga risasi watoto 19 na walimu wawili mnamo siku ya Jumanne, aliuliza: “Ni lini, katika jina la Mwenyezi Mungu, tutasimama ili kukabiliana na hamasisho la bunduki?" (Aljazeera 25 Mei 2022)

Maoni:

Biden alaumu ushawishi wa watu wa bunduki kwa kupigwa risasi watu wasio na hatia licha ya kuwa alikuwa makamu wa rais wa Obama wakati ufyatuliaji risasi pia ulitokea wakati wa mihula yake. Ni mzunguko wa kudumu na matokeo yale yale yanayotarajiwa. "Ilikuwa ni mara ya 27 mwaka huu kwa mpiga risasi aliyejihami kwa bunduki kujeruhi au kuua watu shuleni, kwa mujibu wa hesabu iliyowekwa na EducationWeek. Siku 10 tu kabla ya mauaji katika Shule ya Msingi ya Robb huko Uvalde, mpiga risasi mwenye kiburi cha uzungu mweupe huko Buffalo, N.Y., aliwalenga watu Weusi, na kuwaua 10 ndani ya duka kubwa kwa bunduki aina ya AR-15 iliyokuwa na klipu za risasi za hali ya juu katika shambulizi alilolipanga kulipeperusha moja kwa moja mtandaoni." (Time)

Chama cha Kitaifa cha Bunduki (NRA) sasa ni miongoni mwa makundi yenye nguvu zaidi ya kushawishi maslahi maalum nchini Marekani, chenye bajeti kubwa ya kuwashawishi wanachama wa Congress kuhusu sera ya bunduki. (BBC) NRA ilitumia dolari milioni 1.6 katika nusu ya kwanza ya 2019 kushawishi bunge la Congress dhidi ya sheria ambazo zingeweka ukaguzi mkali wa asili za watu wanaotaka kununua bunduki, kulingana na ripoti za ufichuzi. "Ripoti za ushawishi hazifichui nani watetezi wa NRA waliyekutana naye katika Congress. Rekodi ya mchango wa kisiasa wa shirika hilo, hata hivyo, inaonyesha ni wanasiasa gani ambao NRA inapendelea kuwaona wakiwa mamlakani. (cnbc)

Hivi ndivyo warasilimali wakuu wanavyofanya kazi bila ya uwajibikaji kwa sababu wao ndio washawishi halisi wa sheria kwa kutumia wanasiasa wanaojulikana ili kupata maslahi yao kwa njia ya kisheria. Kutojali kuchinjwa kwa wasio na hatia.

Kwa jumla ili kubadilisha sheria za umiliki wa bunduki kwa ajili ya raia hasa watoto, marekebisho ya katiba ya Marekani yanahitaji kubadilishwa, ili hili lifanyike NRA itahitaji kulainisha misimamo yao au kulegeza mshiko wao wa mamlaka na rushwa (ufadhili mzito… kwa kiasi kikubwa hili litapunguza faida zao). Mzunguko huu ni uvunaji wa umwagaji damu wa kudumu, mamilioni ya dolari kama faida kwa wafanyibiashara wa silaha kwa njia zote za kisheria (kwani wafanyibiashara wa bunduki hawawajibikiwi kwa bunduki na risasi zao).      

Marais wa Marekani ima wanademocrat au wanarepublican hawawezi kubadili hili isipokuwa Mahakimu wa Mahakama ya Upeo warekebishe katiba zao zilizotungwa na mwanadamu, mada ya maslahi finyo ya kibinafsi ya kirasilimali kwa huruma ya mabepari hasa wa mrengo wa kulia wanaoshinikiza udhibiti mdogo wa serikali katika masuala.

Aina za visingizio vinavyodaiwa na wapigaji risasi havina athari yoyote kwani watu kote ulimwenguni wana hali mbaya zaidi kutokana na njaa hadi vita hadi mauaji ya halaiki hadi ufisadi, lakini ni jambo lisilosikika kuwepo ufyatuliaji risasi shuleni kwa silaha mithili ya zile za kijeshi zinazotumiwa na watu wa kawaida. Ni matusi kwa wazazi ambao wamebaki na nyoyo zinazovuja damu ambao wanaweza na watakuwa jinamizi baya la mzazi mwingine kwa sababu kamati za sheria zinakataa kurekebisha sheria zinazoendeshwa na mashini za pesa.

Suala hilo ni kubwa kuliko kubadilisha sera ya umiliki wa bunduki nchini Marekani, mabadiliko hayo yanahitaji kuhusisha mabadiliko msingi ambayo huleta mabadiliko makubwa ili mambo yote yanayotokana na mfumo huo yaweze kutoa haki za binadamu kwa wote. Hili halitapatikana kamwe katika mfumo wa Kibepari. Wataalamu na wajuzi katika nyanja mbalimbali wanathibitisha hili kutokana na mateso ya wazi ya walio wengi wanaoishi Marekani na wale ambao wameathiriwa kikatili na sera za kigeni nje ya nchi.

Hotuba zenye hisia kali za wabunge mbalimbali wa Congress na marais hazitaleta afueni yoyote kwa familia zinazoomboleza. Mabadiliko ya sheria za bunduki (aghlabu hayawezekani) endapo kamwe yatafanywa yataleta tu afueni fupi hakuna chochote zaidi. Watu wa kawaida sio wanaotunga sheria zinazotumikia usalama na ustawi wao, ingawa serikali inajivuna kuwa ni demokrasia ya watu inayoendeshwa na watu, ni kauli mbiu dhaifu, bali kipote cha mabepari wachache matajiri ambao dhamira yao kuu ni kuzidisha faida kwa ajili yao wenyewe ndio watunzi halisi wa sheria nchini Marekani.

Iko badali atakayo dhamini utu na usalama wa mwanadamu kwa sababu imejikita katika mfumo na sheria, mfumo huo ni Uislamu na sheria zake zimetoka kwa Muumba kwa ajili ya viumbe vyake. Uislamu sio tu kwa ajili ya ibada za kiroho wala sio kama unavyoonyeshwa na tawala hadaifu za Magharibi na nguvu zake laini. Uislamu ulikuja na mfumo wa wazi kwa mambo yote ya maisha kwa raia wake wote, Waislamu na wasiokuwa Waislamu, bila ya ubaguzi na hivyo kudhamini haki za binadamu katika hali halisi na si kwa nadharia. Ni juu ya wale wanaotafuta afueni kutafuta nidhamu za Uislamu na kile kichozisimamia ili kuona jinsi Uislamu unavyothamini maisha ya mwanadamu kuliko chochote.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Manal Bader

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu