Jumanne, 24 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/26
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Demokrasia Huzaa Tabaka Fisadi la Wanasiasa Waliojivisha Ngozi ya Kondoo

(Imetafsiriwa)

Habari:

Kila msimu wa uchaguzi nchini Kenya huleta miungano mipya ya kisiasa. Huku uchaguzi ujao ukikaribia, tabaka hilo la wanasiasa linajishughulisha na kuunda miungano mipya huku hatamu ya Uhuru Kenyatta ikifikia mwisho.

Maoni:

Kama Ambrose Bierce – mwandishi wa hadithi fupi wa Kiamerika anavyosema, 'Siasa: ni kung'ang'ania maslahi chini ya pazia la pambano la maadili. Kuendeshwa kwa maswala ya umma kwa faida ya kibinafsi '. Nukuu hii haiwezi kuwa ya kirongo kwani kila pambano katika muundo wa kisiasa wa kidemokrasia, nidhamu unayotokana na itikadi ya kisekula ambayo iliyozalisha uongozi wa kisiasa wenye ulafi na ubinafsi.

Kwa ndoa za muda za kisiasa zilizoko kwa sasa nchini Kenya, wanasiasa wanazurura kote nchini wakiuza 'miungano mipya ya kisiasa' wakiwa na matumaini yaliojadidishwa upya. Historia ya kisiasa ya Kenya imejaa utajiri wa ndoa na usaliti wa kisiasa. Katika zama zote za baada ya ukoloni, ufadhili na ugavi wa ngawira za kisiasa iliwasaidiwa viongozi wa Kenya kudhibiti mianya ya kikabila. Kwa kurudi siasa za vyama vingi tangu mwanzoni mwa miaka ya tisiini, ukuaji wa vyama vya kisiasa umebaki kudumaa, ukishikwa mateka na kuenea kwa miungano ya kisiasa. 

Swali kubwa ni je; kutokana na miungano yote hii mipya inayoibuka wanaonufaika halisi ni kina nani? Hakika, miundo yote ya zamani na mipya sio chochote isipokuwa njia ya kudumisha maslahi ya kisiasa na kiuchumi na ushawishi huku raia wa kawaida wakianguka ndani ya shimo na utumwa zaidi.

Ni muhimu kutaja kuwa Demokrasia huzaa tabaka fisadi la wanasiasa waliojivisha ngozi ya kondoo. Wanasiasa wa kidemokrasia huwaona raia kama njia ya kufikia lengo badala ya kuchunga mambo yao. Huu ndio uhalisia mchungu wa Demokrasia ambayo imezigeuza siasa kutoka kuwa ni jukumu hadi kuwa tu ni njia ya utajiri na ushawishi.

Uislamu ndio mfumo pekee mbadala unaoweza kuzalisha siasa nzuri na wanasiasa halisi wanaomiliki sera madhubuti za ustawi wa kisiasa, kiuchumi na kijamii kama ilivyoshuhudiwa katika karne kumi na tatu zilizopita wakati wa utawala wa Khilafah. Na tunaamini, Mwenyezi Mungu akipenda, kwamba Khilafah atarudi hivi karibuni ili kuongoza tena ulimwengu kwa siasa za ikhlasi ambazo zitaujaza ulimwengu mzima ukweli na haki.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Ali Omar
Mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Kenya

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu