Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Habari na Maoni

Ubalozi wa EU nchini Kenya: Njama ya Ukoloni Mamboleo Kudhibiti Koloni Lake Afrika!

Habari:

Ujumbe wa Umoja wa Ulaya (EU) mjini Nairobi ulizindua ubalozi mpya ukiifanya Kenya kuwa ndio ujumbe wake wa kigeni wa pili kiukubwa duniani baada ya ulioko mjini London. Zaidi ya hayo, Mwakilishi Mkuu wa Masuala ya Kigeni na Sera ya Usalama wa EU, Federica Mogherini alisema, "Tunaiona Kenya ndio njia ya kupitia kuingia katika eneo na Afrika lakini pia ni kituo muhimu. Nimefurahi kuzindua ubalozi wetu mpya hapa mjini Nairobi; ndio wa pili kiukubwa duniani na hii sio sadfa," na akaongeza kusema kuwa, "Uwekezaji wetu wa kiuchumi na kisiasa, hususan mahusiano ya kiusalama ni muhimu mno kwa Umoja wa Ulaya na tunayathamini mahusiano ya Kenya kiukamilifu." (https://www.capitalfm.co.ke/)

Maoni:

Uzinduzi wa EU wa ubalozi mkubwa nchini Kenya unakuja wakati ambapo bwana mkoloni wa Kenya, Uingereza yupo katika msuguano na EU kuhusiana na suala la Brexit. Zaidi ya hayo, EU imo katikati mwa vita vya kiuchumi vya Karne ya 21 ambavyo vinaongozwa na Amerika chini ya mwito wake "Amerika Kwanza." Kuzidisha msumari moto, koloni lake Afrika linaegemea Uchina hususan kiushirika wa kibiashara miongoni mwa miradi mengineyo.

EU imeichagua Kenya kwa kuwa ndio moyo wa tatu wa Uingereza baada ya Afrika Kusini na Nigeria na pia ndio iliyolengwa na Amerika katika mipango yake ndani ya eneo la Afrika ya Kati na Mashariki. Na ndio sababu Amerika ikamualika Rais Uhuru Kenyatta kuzuru ikulu ya White House mnamo Jumatatu, 27 Agosti 2018 ili kwenda kuitongoza Kenya naye Theresa May akamzuru Rais Uhuru Kenyatta mnamo Alhamisi, 30 Agosti 2018 ili kwenda kumakinisha mamlaka ya Uingereza nchini Kenya!

Uzinduzi huu umechangiwa na vigezo hivyo na ni sehemu ya mpango mpana wa EU kuweza kujitanua ndani ya bara la Afrika ambapo Uingereza imekita zaidi kwa mujibu wa mchoro wake unaoitwa nchi za Jumuiya ya Madola ikiwemo Kenya. Kuongezea hapo ni kuwa EU inajali tu kuhifadhi maslahi yake ndani ya bara la Afrika ambalo linatumika kama shamba la kikoloni na lengo lake ni kuporwa rasilimali zake na kutumika kama jaa la kutupa bidhaa zake zilizo tengenezwa ng'ambo kupitia sera nyingi kwa mfano; Makubaliano ya Ushirika wa Ulaya (EPAs), Sera ya Pamoja ya Ukulima (CAP), Mkakati wa Muungano wa Afrika na Ulaya (JAES) na uendelezaji wa utumwa wa watu wake ili wawahudumie katika miradi yao mipya inayolenga kujipanga upya kimuundo duniani!

Linalovunja moyo ni kuwa Kenya na Afrika kwa ujumla zimebakia kimya na kufanya kazi kwa kushirikiana ili kufaulisha njama hizi za Wamagharibi Wakoloni ambao ndio chanzo cha kuganda kwao kisiasa, kiuchumi, kijamii na kielimu kwa makarne kuanzia karne ya 16 hadi leo! Wamefaulu kufanya hivyo kupitia utekelezaji wa mfumo wao batili wa kisekula wa kirasilimali na nidhamu zake ovu zinazo jumuisha demokrasia, jamii huru na uchumi kwa msingi wa ushuru na riba n.k. Wamagharibi bado ndio walioko mamlakani lakini sio kwa njia ya moja kwa moja katika usimamizi wa koloni lao Afrika bali ni kupitia watawala vibaraka ambao wamewaweka au kuwabakisha katika madaraka. Watawala vibaraka wa wakoloni wako tayari kufanya maisha ya raia wao kuwa yenye dhiki kutokana na kutekeleza sera na sheria zilizo chorwa na kupitishwa na mabwana zao Wamagharibi wakiongozwa na Amerika, Uingereza na EU (Ujerumani, Ufaransa) n.k. Baadhi ya sera na sheria zinajumuisha vita dhidi ya Uislamu na Waislamu kwa kisingizio cha kupambana na ugaidi na misimamo mikali ndani ya Afrika. Sera hizi zimepelekea kuwafanyia ujasusi, kuwahangaisha na kuwaua Waislamu kote barani.

Hatua msingi kwa Kenya na Afrika kwa ujumla ya kuchukua ni kujiunga na Mwito wa kurudisha tena maisha ya Kiislamu kwa kusimamisha Khilafah kwa njia ya Utume. Ni Khilafah pekee ambayo inaweze kiukweli kuikomboa Afrika kutoka katika mikono ya chuma ya Wamagharibi wakoloni. Khilafah iliyosimama kwa njia ya Utume itatekeleza Shari'ah (Qur'an na Sunnah) pekee na ambayo kipimo chake cha vitendo kitakuwa ni Halali (imeruhusiwa) na Haramu (haikuruhusiwa) na wala sio kwa mujibu wa kipimo cha kisekula cha kirasilimali ambacho kipimo chake ni maslahi/manufaa! Uwezo wa kweli wa Afrika utaonekana chini ya ulinzi wa Khalifah muadilifu anayetafuta radhi za Mwenyezi Mungu (swt) kinyume na watawala vibaraka ambao wanatafuta radhi za mabwana zao wakoloni! Khalifah atakuwa ni ngao kwa raia wote (Waislamu na wasiokuwa Waislamu) ndani ya Khilafah na kuwadhamini utulivu, ustawi na ufanisi pasina kuzingatia rangi wala dini.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Hizb ut Tahrir na
Ali Nassoro Ali
Mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Kenya

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumapili, 09 Agosti 2020 06:31

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu