Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

FSB ya Urusi Yawakamata na Kuwauwa Wahamiaji kutoka Asia ya Kati

Habari:

Mnamo 27 Julai FSB ya Urusi ilitangaza kummaliza yule anayeitwa "gaidi" katika jiji la Khimki karibu na Moscow. Kwa mujibu wa Huduma Maalum, Mtajik Odil Kayumov mwenye umri wa miaka 19 alidaiwa kupanga shambulizi la kigaidi katika sehemu zilizo na umati mkubwa.

"Wakati wa kukamatwa huko, aliwafyatulia risasi maafisa na kuuwawa kwa risasi ya makabiliano" kituo cha mahusiano ya umma cha FSB kilieleza. "Mhalifu alianza kuwafyatulia risasi maafisa waliokuwa waliotekeleza ukamataji kwa silaha za kiotamatiki… bunduki na maguruneti kadhaa zilipatikana nyumbani kwake – alikuwa akijitayarisha kufyatulia risasi sehemu iliyo na umati mkubwa jijini Moscow," – maafisa hao wa usalama walisema. RBC ilisambaza video ambayo mwili wa mtu huyo aliyeuwawa ulikuwa ukisakwa na maafisa wa FSB na mshikiliaji mbwa mmoja. 

Maoni:

Mwanaharakati maarifu wa haki za kibinadamu na raisi wa Jumuiya ya Wahamiaji wa Kisiasa wa Asia ya Kati Bakhrom Khamroev aliita operesheni maalumu ya FSB ili kuzuia shambulizi la kigaidi ambayo ni marudio ya operesheni za awali zinazo wahusisha wahamiaji. Alishuku uhusiano wa mwendazake na makundi ya kijeshi ya Syria na ana hakika kuwa ameona tofauti katika historia ya FSB kuwa Kayumov alitoka na bunduki kutoka kwa mahame ya gereji jijini Khimki na alikuwa anakwenda Bustani ya Gorky kuwafyatulia watu risasi. Kwa mujibu wa Khamroev, operesheni nzima ya FSB ilikuwa ni "jaribio la kipumbavu" la mamlaka za Urusi kupotosha umakini wa umma kutoka kwa maandamano katika jiji la Khabarovsk na miji mingine ya Mashariki ya Mbali. 

Rai mithili ya hii pia ilitolewa na watumiaji wengi wa mitandao ya kijamii. "Watu walipoanza kuasi, mara moja magaidi walitoka nje ya nyufa zote. Sasa jijini Khabarovsk, sasa jijini Khimki. Ukamataji kama huu ni njama ya kale ya utawala tangu miaka ya elfu mbili: ili kuwatishia watu kwa adui wa nje", - alisema mtumizi wa Twitter wa Urusi Sergei Tegorov. k

Kumbuka kuwa muda chini ya wiki moja nyuma, huduma maalum za Urusi tayari zishatekeleza operesheni nyingi maalum katika mji mkuu na miji kadhaa ya Serbia na Mashariki ya Mbali ili kuwakamata wale wanaoitwa "magaidi", ambapo matokeo yake watu wengi kutoka nchi za Asia ya Kati waliwekwa kizuizini na kukamatwa kwa mara moja, baada ya hapo mnamo Julai 29, operesheni mpya maaalum ilitekelezwa jijini St. Petersburg: kundi moja la wahamiaji kutoka Tajikistan waliwekwa kizuizini kwa kushukiwa ule unaoitwa "ugaidi", kesi ya jinai ilianzishwa dhidi ya mmoja wao chini ya kifungu "Kusaidia vitendo vya kigaidi kupitia ufadhili", - vyombo vya habari vimeripoti "Pazia ya Operesheni".

Wanaharakati wa haki za kibinadamu wamegundua kwamba wafanyikazi wahamiaji kutoka Asia ya Kati wanaongezeka kuwa ima waathiriwa wa michezo ya kisiasa ya serikali ya Urusi, ambayo kwa muda mrefu imezoea kuyazima maandamano ya upinzani na kuwaunganisha watu kwa mashambulizi ya kigaidi yasiyo tarajiwa au kuzuiliwa, au ni waathiriwa wa maslahi ya kiuchumi ya usimamizi wa huduma maalum, ambazo, kupitia kuchochea lile linaloitwa "tishio la kigaidi" nchini Urusi, hupata viwango vikubwa vya pesa kutoka kwa bajeti ya kitaifa ili kupambana na tishio hili lisilo kuwepo.

Watu wa Asia ya Kati kihistoria ni waathiriwa wa sera ya kikoloni ya Urusi, ambayo, baada ya miaka mingi ya uvamizi, waliacha katika eneo madikteta wa kisekula, ambao hawawezi kuwapa hata kazi watu, bali wanachoweza pekee ni kuupiga vita Uislamu na wabebaji wake. Matokeo yake, hatma ya watu wote imekuwa ni uhamishaji nguvu kazi wa kudumu, kukaa mbali na familia zao kwa miaka, kufanya kazi nguvu zaidi na ya kudhalilisha nchini Urusi. Na hatimaye huduma maalum za Urusi kwa uraisi "huwateuwa" wafanyi kazi wahamiaji waliotelekezwa kuwa magaidi, wakichukua maisha yao na uhuru wao, ili kujipatia malengo ya kisiasa au maslahi ya kiuchumi. Na licha ya kuwa nchini Urusi mtindo huu unajulikana na kila mmoja – sio upinzani wa Urusi, wala vyombo huru vya habari vya Urusi hutangaza upande huu, huku wakifadhilisha kuachana na mada hii yenye sumu ya ule unaoitwa "ugaidi", ambayo inabeba picha za hatari kwao.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Muhammad Mansour

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu