Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Beijing +25: Barakoa ya Usawa wa Kijinsia Imeanguka?

Kalima 1: Tangazo la Beijing na Uingizaji wa Siasa Katika Masuala ya Wanawake

na Zeineb Djebbi - Hizb ut Tahrir / Wilayah TUNISIA

(Imetafsiriwa)

Dada zangu wapendwa,

Vipi leo imekuwa sawa na jana, katika karne ya kumi na nane, Mary Wollstonecraft aliandika kuhusu ukombozi wa wanawake, kudai haki zao katika Mapinduzi ya Ufaransa ya ahadi ambazo wanaume walizipata na wanawake walizikosa. Miaka imepita, na fikra, matunda na matokeo ya Mapinduzi ya Ufaransa yakafanywa ya kimataifa, na kuwa, kama nidhamu nyengine yoyote ya kifikra ya Kimagharibi, kuwa ni suala la kiulimwengu na fikra ya kiulimwengu. Leo tunaona na kusikia nchi za ulimwengu, zikiwemo nchi za Waislamu, zikitafakari hatua zilizo pigwa katika kutekeleza Azimio la Beijing na Jukwaa la Utekelezaji yanaoegemea juu ya kile kilichokamilishwa katika utekelezaji wa matokeo ya Mkutano wa Beijing na mikutano mengine ya kimataifa ambayo yamehodhi ushindi kwa kile kinachoitwa masuala ya wanawake.

Fikra ya madai ya haki za wanawake yameanzia kutoka katika utamaduni wa kutenganisha dini na maisha (ambao umetokana na uzao wa Mapinduzi ya Ufaransa) katika mazingira ya kisiasa na kijamii hasa kwa Wamagharibi. Ilikuwa ikijulikana kwa kuwabagua kwake wanawake katika jamii, wanawake walikuwa ni raia wa tabaka la pili. Madai ya haki za wanawake yameangalia historia ya wanawake kutoka kwa mtazamo halisi wa Kimagharibi. Historia ya Wamagharibi, unyanyasaji wake kwa wanawake na taswira yake kwa wanawake kuwa ni chanzo cha ubaya na chanzo cha uovu imekuwa ni historia ya walimwengu wote na hatua ya nchi zote, hata zile ambazo hatuzijui maeneo yao katika ramani, na tusiojua chochote kuhusu tamaduni zao. Kama kawaida, Magharibi imebagua, bali imeangamiza kila turathi isio tokana na turathi yake, na kila utamaduni usio tokana na utamaduni wake (haukutathmini tamaduni kwa namna iliyo sahihi na muwafaka, bali kwa namna ya kulazimisha utambulisho na hadhara juu ya makoloni). Kwa hivyo,utetezi wa wanawake zimeifanya tabia ya Wamagharibi ya ukiukaji wa haki za wanawake kuwa ni urithi kwa wanawake wote, na kukifanya kipindi cha kabla ya ukombozi wa wanawake kuhusishwa na zama za utumwa wa wanawake, na zama mpya zilizo fuatia kuwa ni za ukombozi wa wanawake. Ukombozi huu ulichukuliwa kuwa ni sehemu muhimu sana ya maendeleo ya wanaadamu na hatua ya kuendelea kwa mataifa, na hapa tunafuatilia mijadala kuhusu kongamano lililopita la Beijing na ya baada yake kuwa kama ni kipindi cha kufanya maamuzi muhimu na ni wakati muhimu sana katika historia ya wanawake. 

Istilahi ya madai ya haki za wanawake ilipendekezwa kwa mara ya kwanza mnamo miaka ya 1880 na Mfaransa Hubertine Auclert, ambae alitaka ukombozi wa wanawake na kuwapatia haki zao kama zilivyo ahidiwa na Mapinduzi ya Ufaransa, na kukashifu, kama wanawake wengine wa tabaka la wenye fursa nchini Ufaransa, kutawala kwa mamlaka ya wanaume ambapo wanawake wameshuhudia kuchafuliwa heshima, kudhalilishwa, kubaguliwa na uangalizi mbaya. Kinaya ni kuwa, nchini Ufaransa, mapinduzi yao yaliwadhalilisha kinyama wanawake katika makoloni, na watetezi wa haki za wanawake wa Magharibi kwa miaka hawakutoka mitaani katika miji yao katika kuwaunga mkono dada zao, wanawake, na hawakuathiriwa na udhalilishaji wa wanawake nchini Algeria chini ya kivuli cha ukoloni wa Ufaransa, na hawakushutumu kile ambacho wanawake wa Afrika Magharibi kiliwafika kutokana na utumwa.

Kuchanganyikiwa huku katika kushughulikia masuala ya madai ya haki za wanawake kumeendelea kwa miongo kadhaa, zikiwa harakati hizi zimebaki zikikingwa chini ya kivuli cha tawala za kimabavu za kikoloni. Watetezi wa haki za wanawake katika Misri (Kinanah), kwa mfano, wamekuwa mahodari kudai utekelezwaji wa mipango ya mikataba ya kimataifa juu ya haki za kibinadamu, na hufanya kazi kupitia Kituo cha Kitaifa cha Wanawake, ambacho kinajulikana kwa uungaji mkono wake kwa utawala unaotawala kwa kuwakandamiza wanawake na wanaume. Hudai kufanya kazi kuwakomboa wanawake huku wanafumbia macho wafungwa wenye fikra tofauti ambao hawakubaliani nao.

Watetezi wa haki za wanawake wanatoa wito kwa Wamagharibi kulazimisha fikra ya kijinsia na utandawazi wake na kukubali dhulma na udhalilishaji wa wanawake kote duniani, chini ya mwamvuli wa mapato ya kuhodhi mfumo unao tawala sasa wa kiulimwengu, ambapo wasichana na wanawake huzuiwa kutokana na masomo na kutokana na kufanya kazi katika afisi za serikali endapo watashikamana na haki zao za kiasili kwa wanawake kuvaa mavazi yoyote wanayotaka.

Ili kulazimisha mamlaka ya kifikra, nchi za Magharibi zimeweka masuala ya wanawake chini ya mwamvuli wa haki za kibinadamu, kuepuka mivutano migumu baina ya utandawazi wa mapambano ya wanawake wa Magharibi kwa karne kadhaa ili kupata baadhi ya haki na ubainifu wa tukio hili la kihistoria katika nchi za Magharibi, na ukweli wa wanawake kote duniani. Hivyo historia ya Magharibi imekuwa ni historia ya wanaadamu wote, na faida ya mapambano ya wanaharakati wa haki za wanawake wa Magharibi yamekuwa ni ushindi kwa wanawake na hata kwa walimwengu. Hivyo, kigezo maalum kwa masuala ya wanawake kimetambuliwa na kimechukuliwa kama ni kiwango cha kimataifa kwa kutathmini nchi na mataifa.

Mataifa makubwa yamehalalisha msimamo wao juu ya masuala ya wanawake kama ni sehemu muhimu ya masuala ya haki za binaadamu, na hivyo basi wanajipa uhalali juu ya uingiliaji makini na mpana katika ubwana wa nchi nyengine. Kwa kuhofia vitisho hivi, nchi nyingi zimeanza kupitisha sheria na mipango itakayo kwenda sambamba na dhana ya fikra ya watetezi wa haki za kibinadamu ambazo zinaungwa mkono na kutawaliwa na utaratibu wa kisiasa wa Kimagharibi: ni ukoloni kama tuujuavyo na ni fikra iliyo mbali na usahihi pamoja na sehemu zake nyingi ziilizo kusanywa na Francis Fukuyama katika The End of History and the Last man (Mwisho wa Historia na Mtu wa Mwisho) kuwa ni wakati wa utawazwaji picha ya fikra za kiliberali za Wamagharibi na kwamba ndio ya kiwango cha juu kabisa kinachoweza kufikiwa na wanadamu katika maendeleo yao ya ubwana wa kimaumbile juu ya fikra nyengine yoyote. Hili linatoa ufafanua wa mtazamo jumla ambao ajenda ya kimataifa imeutabanni kuhusiana na masuala ya wanawake ambayo inagongana na fikra ya tamaduni nyingi mbali mbali wanayo ipigia debe.     

Wahudhuriaji wapendwa,

Umoja wa mataifa umenyanyua mwito wa kizazi  cha usawa cha kusherehekea miaka 25 ya Mkutano wa Beijing, kana kwamba udada unawakana mamia ya mamilioni ya wasichana ulimwenguni ambao hawakukulia na fikra ya usawa na hawakushughulika na usawa pamoja na wanaume kwa kadiri ya usawa wao pamoja na wasichana katika kizazi cha usawa katika maeneo ya Magharibi.

Mwito wa “kizazi cha usawa” ulio nyanyuliwa na Umoja wa Mataifa katika kumbukumbu ya Beijing haukuweka usawa baina ya wafanyakazi katika nyanja za utengezaji nguo nchini Bangladesh, wakiwa wanafanyakazi katika hali za unyanyaswaji kwenye maduka, ambayo kimajazi huitwa  viwanda, wakishona nguo na kupata kichache kama malipo yao, ili nguo hizo kuweza kusafirishwa na kuuzwa katika maduka ya fesheni ya Kimagharibi kwa idadi kubwa mno. Ndio, kizazi cha usawa katika Magharibi huota kuhusu usawa kwa haki za wafanyakazi wa viwandani na maslahi ya wakulima wanawake… tunaona kizazi cha usawa katika nchi za Waislamu katika mashua za wahamiaji na katika picha za wasichana wakibeba watoto wao ndani ya mashua za vifo ili kupata maisha mazuri. Na vipi basi Umoja wa Mataifa hudai kuwa kuwawezesha wanawake kunachochea uzalishaji na ukuaji wa uchumi wakati uchumi umeharibika ndani ya uchumi wa nchi dhaifu zinazo dhibitiwa na taasisi za kimataifa baada ya kujazwa madeni ya riba na kutomwezesha yeyote kuzalisha au kusaidia nchi katika uchumi uhuru halisi ambao utaweza kuleta ustawi na kujitosheleza?! Kiko wapi kizazi cha usawa ili kudai usawa wa kweli mbali na mijadala ya jinsia za kiume na za kike na ghilba za mfumo mgumu wa kutatiza?

Wapendwa Wanawake,

Ni maajabu ya mshangao kwa dunia kusherehekea siku zifuatazo (kama ni mfano):

March 8th: Siku ya Kimataifa ya Wanawake

Oktoba 11th: Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike

Oktoba 15th: Siku ya KImataifa ya Wanawake wa Vijijini

Novemba 25th: Siku ya Kimataifa kwa Ajili ya Uondoshaji wa Utumiaji nguvu dhidi ya Wanawake

Kwanini wizara zinazojishughulisha na masuala ya wanawake zinajiunga kusherehekea siku hizi? Na kwanini, kama watu, tunalazimishwa kupumua sana juu ya usawa, licha ya kuwa usawa huo unaotamaniwa haujapatikana bado katika nchi za Magharibi, na wanawake wa Kimagharibi bado wanaota kupata malipo sawa kama wanaume kwa kazi aina moja? Kwa nini tumelazimishwa kusherehekea miaka 25 ya Mkutano wa Beijing japo kuwa unaubagua utamaduni wa Kiislamu na Uislamu kama Mfumo, na kuufanya msamiati wa kigeni katika nchi za Waislamu kuwa ndicho kipimo cha maendeleo?

Wamagharibi wamelazimisha mtazamo wa upande mmoja wa suluki ya mwanadamu na kuwaorodhesha wote wanaokataa fikra zao katika kiwango cha chini cha watu walioendelea. Kama ambavyo kukataa amani na umbile vamizi la Kiyahudi hakumaanishi kukataa amani kabisa, japo kuwa fikra ya amani ya dunia ni fikra dhaifu ambayo haipatikani na haitopatikana katika ulimwengu halisi. Ukataaji wa fikra ya usawa haimaanishi kukubali unyanyasaaji wa wanawake na kuwanyima haki zao, kama ambavyo kukataa kuweka ajenda kwa watu wa ulimwengu hakumaanishi kujitenga.

Hata hivyo, Wamagharibi wamechukua masuala ya wanawake kuwa ni moja ya kigezo kinachoamua mahusiano ya nchi za Magharibi pamoja na watu wa ulimwengu na kuwafanya wao ni miongoni mwa sababu mashuhuri za uingiliaji wa mambo ya nchi na kigezo cha kukubaliwa nchi katika jamii ya kimataifa chini ya utawala wa mfumo wa sasa wa kiulimwengu. Hivyo suala la wanawake linashikilia nafasi ya juu katika majukwaa ya kisiasa na kiuchumi.

Na masuala ya wanawake yanayo shughulikiwa katika mpangilio wa kiulimwengu haimaanishi ndio matatizo halisi ya wanawake wanayo hangaika nayo katika nchi zinazo endelea, bali ni utekelezaji tu wa fahamu ya kimfumo inayo husiana kifikra na masuala ya wanawake ambayo ina maalumati na msamiati maalum kama mpangilio ulio unganishwa pamoja kwa ajili ya masuala ya wanawake kote duniani bila kujali tofauti za kidini na kitamaduni za mujtamaa. Wamagharibi wametabanni istilahi ya jinsia ili kuwafafanua wanadamu katika maana pana na wametabanni istilahi ya mwenza kuangamiza mahusiano baina ya wanaume na wanawake katika muktadha wa ndoa na familia.

Utamaduni wa Magharibi hivi sasa unaonyeshwa kama ni utamaduni mjumuisho kwa wanaadamu wote unaowapa wao njia za kufikia maendeleo na ustawi, na chengine chochote kisichokuwa huu ni fikra kali, ya kigaidi, hasa ikiwa chimbuko lake likiwa ni Uislamu. Hazina nafasi kwao katika ulimwengu wa leo. Mabudha, Wahindu, na wanawake wengine wanatengwa katika jamii za Wamagharibi, lakini hawalengwi wala kubaguliwa. 

Wanawake Wapendwa,

Sisi tunakabiliana na pweza ambaye anawaziba pumzi wanawake wa makoloni ya zamani… Tunakabiliana na pweza ambaye anamikia katika mikutano ya kimataifa inayo shughulikia wanawake na matokeo yake, na katika taasisi za kijamii za kiraia, majukwaa ya kijinsia na vituo vya kitaifa vya wanawake, ambaye anasukuma utamaduni ambao haukusimama kutoka kwenye Itikadi ya Ummah, fikra, na urithi wa tamaduni, na ni mwenye kichwa cha kisiasa ambacho kinakazania ukoloni pamoja na aina zake na kuunga mkono utawala wa Kimagharibi. Pweza ambaye hajali kuhusu masuala yetu na hatilii maanani kabisa juu ya mateso ya wanawake wakimu wa familia, wafungwa wa kisiasa, na Murabitat (Wanawake wa Quds waliowekwa katika hifadhi) ya Msikiti wa Al-Aqsa, na hajali juu ya wanawake katika makambi ya wakimbizi na wanaopigwa mabomu ya utawala wa Bashar Al-Asad – na vipi mkoloni ataweza kujali huzuni na vilio vya wanawake katika ardhi za Waislamu wakati yeye ndiye aliye sababisha hayo kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni?! – Mazingatio yake yote na dhamira ni kuwapurukusha watu kutokana na sababu hizo na kuangazia baadhi tu ya ishara.

Wanamtaka mwanamke mkimu wa familia katika maeneo ya mbali ya vijiji vya Morocco kuzifupisha fikra zake kwenye mzozo na wana familia yake juu ya kinachoitwa “usawa”, mapambano yenye kuchukua istilahi ambayo inazuzua hisia. Ni mazigazi ambayo mwenye kiu hufikiri ni maji! Serikali inayo tawala imempora haki zake za kisheria na kuzuia sharia za Mwenyezi Mungu ambazo zinampatia haki zake bila ya mvutano. Imempa ya mkimu familia (mwenye kumsimamia) na kumuondoshea mzigo wa kujisimamia mwenyewe, achilia mbali familia nzima. Usawa huu ni tofauti mno na usimamizi wa wanaume juu ya wanawake, ambao umewekwa na Uislamu katika kuangazia maumbile ya mwanadamu ambayo yameumbwa kwa wote wanaume na wanawake.

[الرِّجَالُ قَوَّامُونَ عَلَى النِّسَاءِ بِمَا فَضَّلَ اللَّـهُ بَعْضَهُمْ عَلَى بَعْضٍ وَبِمَا أَنفَقُوا مِنْ أَمْوَالِهِمْ]

“Wanaume ni wasimamizi wa wanawake, kwa kufadhliwa na Mwenyezi Mungu baadhi yao juu ya baadhi na kwa mali yao wanayoyatoa.” [An-Nisa’: 34]

Mwanamke wa Kiislamu huepuka mapambano pamoja na wanaume ili afikie ukombozi kamili, kutafuta ukombozi bandia humvunjia familia yake na humfanya kutengwa zaidi na asiye na uthabiti! Mapambano rahisi yanayo washughulisha wanawake kutokana na uhalisia wao uchungu na kutokana na kutawaliwa na vyombo vya kiuchumi vya Kimagharibi juu ya nchi zao, ambayo yanapoteza nguvu, kuvuruga juhudi, na yasiyo na mafanikio yoyote.

Utetezi wa wanawake wa Kimagharibi na madai yake ya utetezi huo wa wanawake katika ardhi za Waislamu chini ya ukoloni, na fikra ya utetezi wa wanawake yamebaki kuwa chini ya ajenda za kisiasa, zinazo tumika kupitisha baadhi ya ajenda na hutumika ili kulazimisha mtazamo finyo wa watu wa ulimwengu. Msomi wa lugha Noam Chomsky amesema, “Kama unahitaji kuwadhibiti watu, basi wafanye wafikiri kuwa wao ndio sababu ya kuwa nyuma kwao.”

Madai ya haki za wanawake katika nchi za Waislamu si chochote isipokuwa ni mikutano ya matabaka ya wenye fursa na ajenda za watu wenye athari, ambazo hazikukisi msisimko wa wanajamii mitaani na yanayo washughulisha wanawake na wasichana. Haikuwa chochote isipokuwa ni utetezi wa dola wa wanawake katika muundo wake muovu, unaoegemea juu ya mfumo uliofeli na kuishi kama vimelea vya maradhi vinavyo eneza madhara na visivyo na faida. Wito wa kipuuzi wa usawa si chochote isipokuwa ni kutotiliwa maanani akili za wanawake na kukuuza mjadala tasa ambao haukumsaidia mwanawake na haukufanikisha heshima na utu wake, bali ni udanganyifu wa makusudi ili kuchafua hukumu za Uislamu katika mioyo na akili za Waislamu. Wanawake wa Kiislamu hawahitaji uadilifu kutoka kwa usawa uliosafirishwa kutoka kwa Wamagharibi, kwani Uislamu, umeziweka haki zao zote ambazo zilichukuliwa kutoka kwake chini ya ujinga wa Waarabu na ujinga wa hadhara nyenginezo, zilizo ubaguzi kati yake na mwanamme kuwa ndio uadilifu, kwa sababu Uislamu umezingatia maumbile, tabia na thamani ya kila mmoja wao, Mwenyezi Mungu (swt) anasema:

[وَلَا تَتَمَنَّوْا مَا فَضَّلَ اللَّهُ بِهِ بَعْضَكُمْ عَلَى بَعْضٍ لِّلرِّجَالِ نَصِيبٌ مِّمَّا اكْتَسَبُوا وَلِلنِّسَاءِ نَصِيبٌ مِّمَّا اكْتَسَبْنَ وَاسْأَلُوا اللَّهَ مِن فَضْلِهِ إِنَّ اللَّهَ كَانَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيماً]

“Wala msitamani alichowafadhili Mwenyezi Mungu baadhi yenu kuliko wengine. Wanaume wana fungu katika walio vichuma, na wanawake wana fungu katika walio vichuma. Na muombeni Mwenyezi Mungu fadhila zake. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu.” [An-Nisa’: 32]

Mwenyezi Mungu (swt), aliye umba jozi, mwanamume na mwanamke, amewaangalia kwa usawa, kuwa ni wanaadamu, lakini kuumbwa kwao hakukuwa sawa katika maumbile na uwezo, na hivyo haiwezekani kwao kuwa sawa katika haki na majukumu, na wito wa usawa baina yao ni uadilifu usio wa kweli. Ni hekima ya Mwenyezi Mungu (swt) kuwa ameziumba hizi tofauti katika maumbile ya kimwili na kisaikolojia baina ya mwanamke na mwanamme, tofauti ya kukamilishana na sio tofauti ya mgongano, wote wana thamani katika majukumu na kazi,  kinyume na miito ya usawa katika mtazamo wa kisekula inayo yafanya mahusiano baina yao kuwa ni mahusiano ya ushindani.

Historia imethibitisha makosa na mapungufu wa madai ya Fukuyama: mivutano ya kifikra baina ya mataifa ni ya kimaumbile tokea Mwenyezi Mungu (swt) alipoumba dunia na vilivyomo ndani yake, na pindi mtu anapofikia hatua ambapo huhisi kuwa amemshinda mwengine huja kuchukua nafasi… na mizunguko hii inaendelea baina ya mataifa hadi Mwenyezi Mungu (swt) atapoirithi ardhi na vilivyomo dani yake. Mwenyezi Mungu (swt) anasema:

[وَتِلْكَ الأَيَّامُ نُدَاوِلُهَا بَيْنَ النَّاس]

“Na siku za namna hii tunawaletea watu kwa zamu” [Al-Imran: 140].

[فَعَسَى اللَّهُ أَن يَأْتِيَ بِالْفَتْحِ أَوْ أَمْرٍ مِّنْ عِندِهِ]

 “Na huenda Mwenyezi Mungu akaleta ushindi au jambo jingine litokalo kwake” [Al-Ma’ida: 52]

Kufuatilia ukurasa kamili wa kampeni na kusoma kalima nyenginezo: Bonyeza Hapa

#GenderEqualityUnmasked                        #CinsiyetEşitliğiMaskesiDüştü

#BarakoaYaUsawaWaKijinsiaImevuliwa                          سقط_قناع_المساواة#

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumapili, 10 Mei 2020 11:10

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu