Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Miaka 25 ya kidonda cha Srebrenica ambacho kingali hakijapona

Na: Bilal Al-Muhajer – Pakistan
(Imetafsiriwa)

Wanadamu hawajapatapo kushuhudia uhalifu mbaya zaidi katika zama hizi za sasa kuliko ule uhalifu uliofanywa na Waserbia nchini Yugoslavia ambako walitekeleza uhalifu wa kinyama tofauti tofauti dhidi ya Waislamu unaoufanya kuwa mbaya zaidi katika historia. Uhalifu huu ulifanyika chini ya macho ya jamii yote ya kimataifa, huku picha na video zikipeperushwa katika runinga na kuchapishwa magazetini kila siku. Jamii ya kimataifa haikufanya lolote kuwasaidia waliokandamizwa nchini Bosnia na Herzegovina inayoifanya jamii yote ya kimataifa, ikiwemo dola vibaraka zilizoko sasa katika ulimwengu wa Kiislamu kuwa wapangaji njama na washirika wa uhalifu huu. Mwenyezi Mungu (swt) anasema (katika hadith Qudsi):

«وعِزَّتِي وجلالِي لَأنْتقِمَنَّ من الظَّالِمِ في عاجِلِهِ وآجِلِهِ، ولأَنْتَقِمَنَّ مِمَّنْ رَأَى مَظلُومًا فقَدَرَ أنْ يَنصُرَهُ فلمْ يفعلْ»

“Na kwa nguvu zangu na utukufu wangu, kwa yakini nitalipiza kisasa kwa dhalimu kwa haraka au kwa kuchelewa, na kwa yakini nitalipiza kisasi kwa yule anayemuona mtu anadhulumiwa na akawa na uwezo wa kumnusuru na asifanye.”

Uhalifu wa Waserbia ulianza nchini Bosnia na Herzegovina kufuatia kuvunjwa kwa Muungano wa Kisovieti, wakati ambapo Macedonia, Slovenia, na Croatia zilipotangaza uhuru wao. Lakini Waserbia, waliokuwa wanasaidiwa na Urusi na Kruseda wa Ulaya, walinyanyua mwito wa kuijenga upya Yugoslavia mpya ili kuhakikisha udhibiti wao juu ya mataifa mwengine yaliyokuwa yameishi chini ya mipaka ya Shirikisho la Yugoslavia tangu kumalizika kwa Vita vya Kwanza vya Dunia. Katika muktadha huu, Waislamu nchini Bosnia walitamani uhuru kama mataifa mwengine. Lakini, Ulaya na Urusi pamoja na Waserbia waliona hili kuwa zito kwao kwa kisingizio kuwa dola tarajiwa ya Waislamu itaasisiwa kinyume na mapendeleo ya uwepo muhimu wa Waserbia nchini Bosnia. Hawangeruhusu kuasisiwa kwa umbile la Kiislamu katikati mwa ulimwengu wa Makruseda. Vita vya umwagikaji damu vikazuka kuanzia 1992 hadi 1995. Kwa mujibu wa Tarakimu za Umoja wa Mataifa, zaidi ya watu laki tatu waliuwawa na maelfu kutawanyika na kukosa makao huku wengi wao zaidi wakiwa ni Waislamu katikati ya kimya cha jamii ya kimataifa, iliyo ongozwa na Amerika, Ulaya na Urusi.

Makafiri daima wamekuwa wakipatiliza fursa dhidi ya Waislamu kila wanapoipata kwa kuwa hakuna kizuizi chochote cha kimfumo wala cha kiakhlaqi, wala hata kizuizi cha kibinadamu miongoni mwa makafiri. Hivyo basi, hupitiliza mipaka zaidi katika uhalifu wao. Mauwaji ya Srebrenica ndio yaliyokuwa mauwaji ya kutisha zaidi ya mauwaji yote. Imeripotiwa kuwa majeshi ya Serbia yaliyo ongozwa na Ratko Mladic yaliingia mji wa Srebrenica mnamo Julai 11, 1995, baada ya kutangazwa kuwa eneo salama na Umoja wa Mataifa. Katika kipindi cha mauwaji hayo ya halaiki, majeshi ya Serbia yaliwauwa maelfu ya Waislamu ambao umri wao ni kati ya miaka saba na sabiini. Na hilo ni baada ya majeshi ya Kiholanzi, yaliokuwa yanahudumu huko, kuwakabidhi maelfu ya Wabosnia kwa majeshi ya Serbia ili kuchinjwa.

Baya zaidi kuliko kuua ilikuwa ni ubakaji kwani heshima ndio kipaumbele kwa Waislamu kuliko nafsi na damu. Na makafiri walilijua hilo vyema. Hivyo basi vita vya Bosnia havikuwa tu ni vita dhidi ya ubwana wa maamuzi pekee, bali kwanza vilikuwa ni vita vya kihadhara baina ya Uislamu na Ukafiri. 

Hivyo basi Waserbia, wakisaidiwa na Kruseda wa Ulaya na Tsar Urusi, walichafua kimakusudi heshima za Waislamu katika hali ya kuogofya mno. Vitendo vya ubakaji na mateso vilivyo tekelezwa dhidi ya wagonjwa wa kike wa Kiislamu ndani ya hoteli na hospitali za Bosnia na Herzegovina ni ushahidi wa uhalifu huu. Wanajeshi walitumia ubakaji na aina tofauti tofauti za mateso kama silaha za vita. Mmoja wa wahanga aliyekuwa anazuiliwa katika hospitali kutokana na maradhi makali mnamo 1999 alisema: "Nilibakwa kila usiku, na hii ilichukua muda wa zaidi ya mwezi mmoja."  

Alisema: "Nilibakwa na wanajeshi sita au saba kila usiku kwa mpigo, wakati mwengine katika kitanda changu cha hospitali. Nilipitia mambo yote haya ya kuogofya, walining'oa maneno yangu, wakanipiga, na usiku ulipofika nilijua fika kile kitakacho nitokea." Uhalifu huu ulirudiwa, kwa uchache, kwa zaidi ya wanawake 70,000 wa Kiislamu.

Kama ambavyo tumeweka uaminifu wetu kwa jamiii ya kikrusedi ya kimataifa, ambao hawazingatii mkataba wala udugu wala ahadi ya ulinzi kwa muumini na kudai tu kuregelea na kulinda haki za kibinadamu, jamii ya kimataifa ililazimika kuwatoa wahanga kafara ili kuwaadhibu mbele ya rai jumla ya kiulimwengu ili kujitakasa kutokana na dhambi la kimya chake na kupanga njama ya uhalifu pamoja na Waserbia. Kejeli yake ilikuwa ni utoaji hukumu ya kifungo cha maisha kwa kamanda wa zamani wa jeshi la Waserbia wa Bosnia, Jenerali Ratko Mladic miaka miwili kabla ya Mahakama ya Kimataifa ya Jinai kwa uhalifu wa kivita jijini Hague katika iliyokuwa Yugoslavia na kulaani kwake uhalifu huo kama mauwaji ya halaiki dhidi ya Waislamu wa Bosnia. Na mauwaji haya ya kutisha yalidunishwa na kuwa ni mashtaka ya kejeli ambapo wahalifu hawaadhibiwi, wala walioadhibiwa hawafiki ushuri ya idadi ya wahalifu, ambapo ni sambamba na uhalifu wao. Hivyo basi, wahalifu wangali wako huru, wala hawajawasilishwa kwa mashtaka, hawajaadhibiwa na hawajatekelezewa Hudud za Kiislamu hadi leo.

Uhalifu huu na uhalifu mwengineo ambao makafiri wakoloni wameutenda hautaachwa upite kwa kupita wakati kama ambavyo baadhi ya wanasheria ya Kimagharibi wanavyo dhani. Bali uhalifu wa Ufaransa barani Afrika, uwe mpya au wa zamani, uhalifu wa Italy nchini Libya, uhalifu wa Amerika nchi Iraq na Afghanistan, uhalifu wa China katika mashariki mwa Turkestan, na wa Mabudha nchini Burma, uhalifu wa Mayahudi katika Ardhi Iliyo Barikiwa ya Palestina na pia uhalifu wa Waserbia nchini Bosnia na Herzegovina, uhalifu wote huu umehifadhiwa katika kumbukumbu za Ummah huu bila ya kuzingatia ima ni wa zamani sana au wa hivi punde. Ummah utawahesabu wauwaji wake, na wale waliowabaka wanawake wao kwa kipimo kilicho nyooka na utasimamisha hudud za kisharia juu yao wote, ambazo kwazo nyoyo za waumini zitatosheka. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) aliwauwa washirika wote wa uhalifu waliofichua uchi wa mwanamke mmoja tu wa Kiislamu miongoni mwa kabila la Banu Qaynuqa na kuwafurushwa wengine waliosalia katika wao kwa kunyamazia kwao kimya uhalifu huo. Huu ni mfano mwepesi tu katika upande wa adhabu ambayo itawaangukia Waserbia, wafuasi wao na wale walio nyamazia kimya uhalifu wao.

Uhalifu mwingi wa kinyama uliofanywa katika maeneo ya Waislamu ulikuwa katika zama za sasa, tangu kuanguka kwa Khilafah Uthmani miaka mia iliyopita. Pengine, matukufu ya Waislamu ni hizaya kwa makafiri iliyo wafanya kupitiliza na kuyachafua matukufu haya hadi leo. Sababu ya hilo ni mporomoko wa kimfumo na kifikra wa makafiri na kubeba imani na fikra batili zilizo fisidika. Hivyo uharibifu wao na imani na fikra zisizo za kinyama huwafanya wao kutekeleza kila aina ya uhalifu dhidi ya wanadamu na hususan Waislamu.

Hivyo basi, hakuna kikwazo chochote kwao isipokuwa nguvu itakayo wawekea mipaka na kuwafanya wasahau wanaomuabudu shetani. Hivyo basi ufaradhi wa kusimamisha mamlaka ya Uislamu na Waislamu ni miongoni mwa faradhi kubwa mno baada ya kutamka shahada mbili (yaani kushuhudia kwamba Mwenyezi Mungu Ndiye Mola wa haki pekee na Muhammad (saw) ni Mtume Wake). Vipi hili litawezekana bila ya mamlaka ya Uislamu yenye kulinda msingi (بيضة) wa Waislamu na vitu vya thamani mno miongoni mwa vitu wanavyo miliki katika damu, mali na heshima, imesema kweli hadith ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw)

«إِنَّمَا الْإِمَامُ جُنَّةٌ يُقَاتَلُ مِنْ وَرَائِهِ وَيُتَّقَى بِهِ»

“Hakika Imam ni ngao, watu hupigana nyuma yake na hujihami kwayo” (Muslim).

* Imeandikwa kwa Ajili ya Gazeti la Ar-Rayah – Toleo 295

#Srebrenica25YearsOn   #Srebrenitsa25Yıl  #SrebrenicaMiaka25Baadaye سربرنيتشا_جرح_لم_يندمل#

 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu