Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Modi Atafuta Ushindi wa Uchaguzi kupitia Mateso ya Waislamu na Kuvunja Misikiti yao na Nyumba zao
Na Musab Umair – Wilayah Pakistan

(Imetafsiriwa)

Wahindi walipiga kura katika awamu ya mwisho ya uchaguzi wa kushangaza wa nchi mnamo tarehe 1 Juni 2024, katika zoezi la uchaguzi lililoanza mnamo tarehe 19 Aprili 2024. Modi ni waziri mkuu wa sasa wa serikali ya chama tawala cha Muungano wa Kitaifa wa Kidemokrasia (NDA), inayoongozwa na chama chake, Chama cha Bharatiya Janata (BJP). Upinzani ni Muungano wa Kitaifa wa Maendeleo ya Kitaifa wa India (I.N.D.I.A) unaoongozwa na chama kikuu cha upinzani nchini India, Indian National Congress, ambacho hapo awali kilitawala siasa na kutawala kwa miongo kadhaa, hadi kuibuka kwa BJP.

Siasa za uchaguzi za Modi zinaegemea kueneza chuki za kidini dhidi ya Waislamu, katika maisha yake yote ya kisiasa. Wakati alipokuwa ni Waziri Kiongozi wa Gujrat mnamo 2002, Narendra Modi, alisimamia mauaji ya Waislamu zaidi ya elfu mbili. Mnamo tarehe 1 Machi 2002, katika kilele cha uchinjaji Modi alidai kwamba, “Kila kitendo kina majibu sawa na majibu ya kinyume yake (Har kriya ki pratigriya hoti hai).” Baadaye, akiwa waziri mkuu amesimamia uharibifu wa misikiti, ubomoaji wa nyumba za Waislamu na mashambulizi ya makundi ya watu dhidi ya jamii za Waislamu.

BJP ya Modi inatumia chuki ya kidini kuficha tofauti kubwa ya utajiri na umaskini mkubwa nchini India. Katika Faharasi ya Njaa Ulimwenguni ya 2023, inaelezwa kuwa, “India inashika nafasi ya 111 kati ya nchi 125 zenye data ya kutosha kukokotoa alama za GHI za 2023. Ikiwa na alama 28.7 katika Faharasi ya Njaa Ulimwenguni ya 2023, India ina kiwango cha njaa ambacho ni kibaya.” [1]. Ama kuhusu pengo kati ya matajiri na maskini, kwenye waraka wa utafiti wa tarehe 12 Machi 2024 wenye kichwa, “Kukosekana kwa Usawa wa Mapato na Utajiri nchini India, 1922-2023: Kuongezeka kwa Bilionea Raj,” inaangazia kwamba ukosefu wa usawa “ulianza kuongezeka na umeongezeka sana tangu mwanzoni mwa miaka ya 2000,” huku akiongeza, “Kufikia 2022-23, asilimia 1 ya juu ya mapato na hisa za utajiri (22.6% na 40.1%) ziko katika viwango vyao vya juu zaidi vya kihistoria na sehemu ya juu ya mapato ya 1% ya India ni miongoni mwa za juu zaidi ulimwenguni.” [2]

Ingawa muungano wa upinzani unatarajua kufeli kwa Modi kwa maskini, na mateso yake kwa wachache kushinda, una nafasi ndogo ya kufanya hivyo. Kando na siasa zake za mgawanyiko, Modi anaungwa mkono kamili na Marekani. Kwa njia ambayo ni sawa na msimamo wake pamoja na Netanyahu, utawala wa Biden unasimama kulaani ukandamizaji wa Modi, huku ukitoa nafasi ya kutosha kwa Modi kuendeleza vita vyake dhidi ya Waislamu. Mnamo tarehe 20 Mei 2024, wakati Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, Mark Miller, alipoulizwa kuhusu hadithi ya uchunguzi ya New York Times yenye kichwa “Wageni katika Ardhi Yao Wenyewe: Kuwa Muislamu katika India ya Modi”, ambayo inaeleza jinsi Waislamu wanavyolea familia zao na watoto wao kwa hofu na kutokuwa na uhakika, alijibu, “Tumeshirikisha nchi nyingi, ikiwemo India, juu ya umuhimu wa kuamiliana kwa usawa kwa washiriki wa jumuiya zote za kidini.” [3]

Kwa hakika, Modi amepata kuungwa mkono na Wamarekani, kwa kupata maslahi muhimu ya Marekani katika eneo hilo. Licha ya umaskini uliokithiri katika nchi yake na ukosefu wa mshikamano wa kijamii, Modi ameiingiza India katika mapambano ya gharama kubwa na China, ili kupata maslahi ya Marekani kudhibiti na kukabiliana na China. Kwa mujibu wa sera ya Marekani, na kwa uratibu na vibaraka wa Marekani ndani ya uongozi wa Pakistan, Modi anafanya kazi kikamilifu kuunda kambi ya kieneo dhidi ya China, huku India ikiwa kama kiongozi na Pakistan kama wanachini mdogo. Kwa upande wao, watawala wa Pakistan wanafanya kazi mkono kwa mkono na Modi, licha ya vita vyao vya maneno. Kwa hivyo, watawala wa Pakistan waliwazuia wanajeshi wa Pakistan, wakati Modi alipoiunganisha kwa nguvu Kashmir Inayokaliwa kimabavu mnamo Agosti 2019. Walitangaza hata Jihad kuwa usaliti, wakiwadunga kisu mujahidina wa Kashmir mgongoni, na kulipa jeshi oga la Dola ya Kibaniani afueni iliyohitajiwa sana. Sasa wanalitia mtegoni Jeshi la Pakistan katika vita vya muda mrefu na Waislamu katika maeneo ya kikabila wanayoshirikiana Pakistan na Afghanistan, na kutoa hata afueni zaidi kwa India. Inatarajiwa kwamba baada ya uchaguzi, kibaraka wa Marekani Modi, pamoja na vibaraka wa Marekani nchini Pakistan, wataongeza mafungamano ya kiuchumi, chini ya uhalalishaji mahusiano.

Enyi Waislamu wa Pakistan, Afghanistan, India na Kashmir! Ni juu yetu kusitisha udhalimu wa Modi na mpango wa Marekani kukandamiza Waislamu na Uislamu. Kwa nini ni lazima tukiuke Dini yetu, tukisalimisha matukufu yetu yasiyoweza kukiukwa, ili kutoa nafasi kwa watu wa Batili na Upotofu? Sisi ni watu wa heshima ambao ni warithi wa urithi wa ajabu. Ni urithi wa Kiislamu ambao ulianza wakati wa Khilafah Rashida, ukiishia katika kutawala kwa Uislamu katika Bara Dogo la India. Ilikuwa katika enzi ya utawala wa Uislamu ambapo hisa ya Bara Ndogo la India ya uchumi wa dunia ilikuwa asilimia 23, sawa na Ulaya yote ikijumuishwa, ikipanda hadi asilimia 27 mnamo 1700, wakati wa Aurangzeb Alamgir. Karne za utawala wa Kiislamu zilihakikisha ustawi na usalama kwa wakaazi wa eneo hilo, bila kujali rangi au dini zao, kupata utiifu wao, wakiwemo Mabaniani. Hakika, zama za Kiislamu zilikuwa zama za dhahabu ambazo ziliangaza nuru yake kwa ulimwengu wote, zikivuta hisia zisizohitajika za ulafi za dola za kikoloni, ambazo zilipanda mbegu za migawanyiko ya jamii ili kugawanya na kutawala. Hivyo basi, hebu sote natufanye kazi kwa bidii ili kusimamisha tena Khilafah kwa Njia ya Utume ili Bara Dogo la India liweze kunyanyuka tena chini ya rehma ya Uislamu.

Maregeleo

[1] https://www.globalhungerindex.org/india.html

[2] https://wid.world/wp-content/uploads/2024/03/WorldInequalityLab_WP2024_09_Income-and-Wealth-Inequality-in-India-1922-2023_Final.pdf

[3] https://www.state.gov/briefings/department-press-briefing-may-20-2024/#post-560886-India

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu