Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki

Halaqa ya Mjadala mjini Kahraman Marsh Kutafuta Suluhisho la Kiislamu kwa Mgogoro wa kiuchumi

Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki iliandaa halaqa ya mjadala katika mji wa Kahraman Marsh kama sehemu ya kampeni yake kwa anwani "Suluhisho la Kiislamu kwa Mgogoro wa Kiuchumi", ambayo inawasilisha masuluhisho msingi ya Kiislamu kwa mgogoro wa sasa wa kiuchumi nchini Uturuki, kwa kuwasiliana na mashirika yasiyo ya kiserikali, wawakilishi wa vyama na vyombo vya habari vya ndani na kujibu maswali yao.

Ndani ya wigo wa "suluhisho la kimsingi la Kiislamu kwa mgogoro wa kiuchumi", wawakilishi wa vyama vya kisiasa, mashirika yasiyo ya kiserikali, wawakilishi wa vyombo vya habari vya ndani na walezi walikusanyika katika mji wa Kahraman Marsh.

Mazungumzo hayo yaliyoanza na hotuba ya ufunguzi ya Ustadh Ahmed Saba yaliendelea na hotuba ya Ustadh Muhammad Hanafi Yaghmour. Baada ya uwasilishaji, awamu ya maswali na majibu ilianza na baadhi ya washiriki walitoa michango muhimu kwa maswali yao na wengine kwa maoni yao. Maustadh Eren, Abdullah Imamoglu, Musa Beyoglu na Mehmet Hanafi Yaghmur walijibu maswali yaliyoulizwa.

Katika mkutano wetu kulisisitizwa udharura wa kuweka masuluhisho na hukmu za Uislamu katika kila nyanja kwenye ajenda, na kwamba Uislamu una masuluhisho ya kina na halisi katika utawala, uchumi, elimu na nyanja za kijamii, na ikasisitizwa kuwa yaelezwe katika kila jukwaa.

Kwa Mengi zaidi Bonyeza Hapa

Jumapili, 27 Jumada al-Akhir 1443 H sawia na 30 Januari 2022 M

Kwa Maelezo Zaidi Zuru Mitandao ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki:

Tovuti Rasmi ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki

Ukurasa wa Facebook wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki

Ukurasa wa Twitter wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki

Akaunti ya Instagram ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki

Chaneli ya YouTube ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki

Tovuti ya Jarida la Kokludegisim

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu