Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Hizb ut Tahrir / Wilaya Tunisia:

Amali zilizo Andaliwa kipindi cha Kampeni ya Kiulimwengu, “Ukombozi wa Kostantinopol Bishara Njema ikatimia…ikifuatiwa na Bishara Njema”!

Chini ya muongozo wa Amir wa Hizb ut Tahrir, Mwanachuoni Mkubwa, Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah, Mwenyezi Mungu Swt Amuhifadhi, Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir imezindua kampeni pana ya kiulimwengu kuadhimisha tukio la Kumbukumbu ya Hijiria ya Ukombozi wa Kostantinopoli  #Kostantinopol, (mji wa mfalme Hirakila) ambao ulizingirwa kuanzia 26 Rabii’ al-Awwal hadi 20 Jumadal al-Awwal 857 H sawia na 5 Aprili hadi 29 Mei 1453 M, na hivyo basi bishara njema ya hadithi tukufu ya Mtume (saw) ikatimia:

 «لَتُفْتَحَنَّ الْقُسْطَنْطِينِيَّةُ فَلَنِعْمَ الْأَمِيرُ أَمِيرُهَا وَلَنِعْمَ الْجَيْشُ ذَلِكَ الْجَيْشُ»

Kwa yakini mtaifungua Kostantinopoli, na Amir bora ni Amir wake, na Jeshi Bora ni jeshi hilo.”

Hizb ut Tahrir Wilaya ya Tunisia imejitosa katika kampeni hii ya kiulimwengu. Sifa njema zote anastahiki Mwenyezi Mungu (swt)

Ijumaa, 15Jumada al-Awwal 1441 H - 10Januari 2020 M

Kalima na Dkt. Lassad Al-Ajeili

Mkuu wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Wilaya ya Tunisia

Katika kumbukumbu ya Ukombozi kwa Kontantinopol Bishara njema Ikatimia …Ikifuatiwa na Bishara Njema!

Jumanne, 19 Jumada al- Awwal 1441 H - 14Januari 2020 M

Kalima na Ustaadh Ahmed Ben Hussein

Mwanachama wa Hizb ut Tahrir Wilaya Tunisia

Jumanne, 19 Jumada al- Awwal 1441 H – 14 Januari 2020 M

Matukio yanayo adhimisha Kumbukumbu ya Mapinduzi inayo yakisadifiana na Kumbukumbu ya Ukombozi wa Kostantinopoli

Jumanne, 19 Jumada al- Awwal 1441 H - 14 Januari 2020 M

Kwa wiki ya pili mfululizo, mashabab wa Hizb ut Tahrir katika eneo la Sfax, wamefanya amali ambazo ziliingiliana na ujumbe wa Amir wa Hizb ut Tahrir, Sheikh Ata Abu al-Rashta, Mwenyezi Mungu amuhifadhi, kuhusu kumbukumbu ya Ukombozi wa Kostantinopoli. Wakati huu walijumuika pamoja na waumini wa Msikiti wa Sidi Lakhmi katika mji wa Sfax, baada ya swala ya Ijumaa, ambapo Ndugu Mohamed Kechid alitoa ujumbe ambao unaamsha azma na kuwakumbusha Waislamu kuhusu kumbukumbu hii kubwa, akigusia kwamba taarifa hizi nzuri ambazo zilipatikana, zinafuatiwa na ishara nyingine, ikianza na kusimamishwa kwa Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume ili kuikomboa Jerusalem kutokana na uovu wa Mayahudi na kisha kuifungua Roma, kama ilivyo thibitishwa na Hadith za Mtume kipenzi Muhammad (saw).

Huku Takbeer zikiwa zimetanda na kuinuliwa juu bendera za Uqab na Raya za ukombozi wa Kiislamu, ndugu Mohamed Kechida hakusahau kuwakumbusha Waislamu kwamba ni muhimu kufanyakazi ili kuregesha mamlaka ya Kiislamu na kuhuisha maisha kamili ya Kiislamu yaliyo sambamba na maamrisho ya Mwenyezi Mungu (swt), na kutimiza ahadi Yake ya izza kwa Ummah huu ya ukhalifa na tamkini, na bishara njema ambazo zinafuata bishara njema ya ukombozi wa Kostantinopoli.

Vilevile ujumbe maalum ulielekezwa kwa vikosi vya majeshi kambini mwao, kutekeleza wajibu katika mchakato wa mabadiliko kwa misingi ya Kiislamu, kama alivyofanya kiongozi mwenye ushawishi Muhammad al-Fateh, Mwenyezi Mungu (swt) amrehemu, kwa sababu alfajiri ya Khilafah imesha chomoza na ishara zake zipo wazi. Alhamdulillah Rab Alameen.

Ijumaa, 22 Jumada al-Awwal 1441 H sawa na 17 Januari 2020 M

Kutoka Sfax

Bishara Njema ya Mtume saw Ikatimia … na Bishara nyingine zinafuatia.

Jumapili, 17 Jumada al-Awwal 1441H   - 12 Januar 2020M

Kwa habari zaidi, tafadhali zuru mitandao ya Hizb ut Tahrir / Wilaya Tunisia:

Ukurasa Rasmi wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia
Ukurasa wa Facebook wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia

Alama Ishara za Kampeni

#فتح_القسطنطينية

#القسطنطينية

#İstanbulunFethi

#istanbul

#ConquestofIstanbul
#Constantinople

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumatano, 20 Mei 2020 19:59

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu