- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia:
Matembezi ya Ukombozi: “Enyi Majeshi (Mna nini mnapo ambiwa: Nendeni katika Njia ya Mwenyezi Mungu, mnajitia uzito katika ardhi?”
Matembezi yalitoka katika mji mkuu wa Tunis, baada ya swala ya Ijumaa, mnamo tarehe 28 Machi 2025 sawia na tarehe 28 Ramadhan 1446 kuanzia Msikiti wa Al-Fath yalioandaliwa na Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Tunisia kuinusuru Gaza dhidi ya uadui wa Marekani Mzayuni, ambayo yaliitishwa na watu wa Zaytouna Tunis na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa watu kutoka Tunisia ya kijani. Mabango yaliinuliwa, bango kuu likisomeka, “Enyi majeshi! (Mna nini mnapo ambiwa: Nendeni katika Njia ya Mwenyezi Mungu, mnajitia uzito katika ardhi?)” ... Katika kulaani kitendo cha mahakama ya kijeshi kumkamata mwanachama wa Hizb ut Tahrir/WilayahTunisia, Ustadh Muhammad al-Nasser al-Shuwaikha, ambaye alikosoa miondoko ya kijeshi iliyofanyika Tunisia pamoja na adui Marekani. Mabango mawili yaliinuliwa, la kwanza, “Kwa Mahakama ya Kijeshi nchini Tunisia: Kukosoa miondoko ya kijeshi pamoja na adui Marekani sio tuhuma.” Jengine lilisomeka, “Kwa Mahakama ya Kijeshi nchini Tunisia: Waachilieni huru wale wanaoinusuru Gaza.” Makumi ya mabango pia yaliinuliwa, yakitoa wito kwa majeshi ya Waislamu katika nchi za Kiislamu kuwanusuru ndugu zao nchini Palestina. Matembezi hayo yaling’oa nanga kwa takbir na tahlil na kuzunguka barabara kuu za mji mkuu zinazoelekea Barabara ya Al-Thawra. Yalimalizika kwa hotuba iliyotolewa na mmoja wa mashababu wa Hizb ut Tahrir, ambapo aliyakumbusha majeshi ya Waislamu juu ya udharura wa kuwanusuru ndugu zao wa Palestina baada ya kuviangusha viti vya watawala madhalimu.
Maandamano haya yanajiri baada ya kuregea vita vya maangamizi dhidi ya ndugu zetu wa Gaza, ili kuthibitisha kwamba Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Tunisia imejitolea kwa ajili ya watu wa Palestina na kwamba itaendeleza ulinganizi wake wa kusimamisha utawala wa Uislamu kupitia kusimamisha dola ya Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume, ahadi ya Mwenyezi Mungu (swt) na bishara njema ya Mtume Wake Mtukufu (saw).
Mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Tunisia
Ijumaa, 28 Ramadhan Al-Mubarak 1446 H sawia na 28 Machi 2025 M
- Sehemu ya Amali ya Matembezi -
https://domainnomeaning.com/sw/index.php/dawah/tunisia/4621.html#sigProId44c1e0ad7d
- Alama Ishara za Amali -
#طوفان_الأقصى
#الجيوش_إلى_الأقصى
#الأقصى_يستصرخ_الجيوش
#AksaTufanı
#OrdularAksaya
#ArmiesToAqsa
#AqsaCallsArmies
Kwa maelezo zaidi tafadhali zuru mitandao ya Hizb ut tahrir / Wilayah Tunisia:
Tovuti Rasmi ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia
Ukurasa wa Facebook wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia
Tovuti Rasmi ya Jarida la Tahrir
Ukurasa wa Facebook wa Jarida la Tahrir