- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia:
Matembezi ya Ukombozi: “Enyi Waislamu, Je, Mtawaacha Watu wa Palestina peke yao na Hali Umma una Majeshi yenye Nguvu?”
Baada ya Swala ya Ijumaa, katika mji mkuu, Tunis, yalifanyika matembezi ya hamsini yaliyoitishwa na Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia, kwa watu wa Zaytouna, kwa ajili ya kuwanusuru watu wa Ardhi Iliyobarikiwa (Palestina) na Msikiti uliobarikiwa wa Al-Aqsa ulio mateka, na kichwa chake kilikuwa, “Enyi Waislamu, je, mtawaacha watu wa Palestina peke yao na hali Umma una majeshi yenye Nguvu?!” matembezi hayo yalianza mbele ya msikiti wa Al-Fath na kufikia katika barabara ya Al-Thawra ambapo yalizunguka katika barabara kuu za mji mkuu, wakati ambapo uwepo mkubwa wa watu wa Zaytouna waliimba kauli mbiu zilizoyakusudia moja kwa moja majeshi ya Waislamu, miongoni mwazo ni: “Enyi majeshi, vunjeni mipaka ili tuweze kupigana na Mayahudi,” na “Majeshi yako tayari kwa ajili ya ushindi wako, ewe Mola Mlezi wa waja.” na kauli mbiu nyenginezo zilizoelekezwa kwa watu wa Ardhi Iliyobarikiwa (Palestina), zikiwemo “Kutoka Tunisia hadi Ash-Sham, miadi yetu ni Dola la Uislamu,” “Kutoka Tunisia hadi Palestina, Umma ni mmoja, sio Umma mbili.” “Ewe Gazawi (mtu wa Gaza), damu yako ni damu yangu,” “Ewe Gazawi (mtu wa Gaza), vita vyako ni vita vyangu,” ambapo mabango yaliinuliwa na kichwa cha maandamano hayo kiliandikwa kwenye bango kuu na mabango mengine takwimu za mashahidi na watu waliopotea na bango kubwa zaidi liliandikwa juu yake “Gaza inawaita nyinyi, enyi majeshi ya Waislamu, tunapigana hadi tutakapojumlishwa.” Maandamano hayo yalihitimishwa kwa hotuba iliyotolewa na mmoja wa mashababu wa Hizb ut Tahrir/Wilayah ya Tunisia akiyakumbusha majeshi Waislamu wajibu wao wa kisheria kuelekea Gaza na hadithi ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) isemayo: "مَا مِنِ امْرِئٍ يَخْذُلُ مُسْلِماً فِي مَوْطِنٍ يُنْتَهَكُ فِيهِ حُرْمَتُهُ ، وَيُنْتَقَصُ فِيهِ عِرْضُهُ إِلا خَذَلَهُ اللَّهُ فِي مَوْطِنٍ يُحِبُّ فِيهِ نُصْرَتَهُ، وَمَا مِنِ امْرِئٍ يَنْصُرُ مُسْلِماً فِي مَوْطِنٍ يُنْتَقَصُ فِيهِ مِنْ عِرْضِهِ وَتُنْتَهَكُ فِيهِ حُرْمَتُهُ إِلا نَصَرَهُ اللَّهُ عَزَّ وَجَلَّ فِي مَوْطِنٍ يُحِبُّ فِيهِ نُصْرَتَهُ" “Hakuna yeyote anayemtelekeza Muislamu mwengine mahali ambapo utukufu wake unakiukwa na heshima yake inavunjwa isipokuwa Mwenyezi Mungu atamtelekeza katika mahali ambapo angependa nusra yake ndani yake, na hakuna Muislamu atakayemnusuru Muislamu mwengine katika mahali ambapo heshima yake inavunjwa na utukufu wake kukiukwa, isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu atamnusuru mahali anapopenda nusra yake.”
Sisitizo la Hizb ut Tahrir/Wilayah Tunisia kuendelea kuandaa matembezi haya ya kila wiki na kuyataka majeshi ndani yake kuwanusuru ndugu zao katika Ardhi Iliyobarikiwa (Palestina) kwa takriban mwaka mmoja, yaani tangu kuzuka kwa Kimbunga ch Al-Aqsa, ni kwa kufuata amri ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake Mtukufu, ambaye alisema: "مثل المؤمنين في توادهم وتراحمهم وتعاطفهم مثل الجسد إذا اشتكى منه عضو تداعى له سائر الجسد بالسهر والحمى" “Mfano wa Waumini katika kupendana kwao, kuhurumiana kwao na kuoneana upole kwao ni kama mfano wa mwili, kiungo chochote kikishitakia maumivu mwili mzima hujibu kwa kukosa usingizi na homa.” Na watu wa Gaza na mujahidina wake hawatazuia jinai za Mayahudi dhidi yao isipokuwa nguvu ndiyo itakayowazuia, na nguvu hii ni majeshi ya Waislamu na pindi watakaposonga watu wenye ikhlasi miongoni mwao, umbile la Kiyahudi litakwisha na itakuwa ni athari kwenye jicho... amesema Mwenyezi Mungu (swt):
"ادْخُلُوا عَلَيْهِمُ الْبَابَ فَإِذَا دَخَلْتُمُوهُ فَإِنَّكُمْ غَالِبُونَ ۚ وَعَلَى اللَّهِ فَتَوَكَّلُوا إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ"
“Waingilieni kwa mlangoni. Mtakapo waingilia basi kwa yakini nyinyi mtashinda. Na mtegemeeni Mwenyezi Mungu ikiwa nyinyi ni Waumini.” [Al-Maida: 23]
Mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Tunisia
Ijumaa, 17 Rabi’ ul-Awwal 1446 H sawia na 20 Septemba 2024 M
Sehemu ya Amali za Matembezi
https://domainnomeaning.com/sw/index.php/dawah/tunisia/4213.html#sigProId2c9e3fce67
Alama Ishara za Amali
#طوفان_الأقصى
#الجيوش_إلى_الأقصى
#الأقصى_يستصرخ_الجيوش
#AksaTufanı
#OrdularAksaya
#ArmiesToAqsa
#AqsaCallsArmies
Kwa maelezo zaidi tafadhali zuru mitandao ya Hizb ut tahrir / Wilayah Tunisia:
Tovuti Rasmi ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia
Ukurasa wa Facebook wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia