- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia:
Matembezi “Ramadhan ni mwezi wa Jihad na Ufunguzi, basi Songeni, Enyi Majeshi ya Waislamu, kwa ajili ya Kuinusuru Gaza”
Hizb ut-Tahrir / Wilayah ya Tunisia iliandaa matembezi yenye kichwa “Ramadhan ni mwezi wa Jihad na Ufunguzi, basi Songeni, Enyi Majeshi ya Waislamu, kwa ajili ya Kuinusuru Gaza” baada ya swala ya Ijumaa kutoka Msikiti wa Al-Fatah katika mji mkuu hadi barabara ya Al-Thawra ambayo ni matembezi ya 23 mfululizo, na kama kawaida, matembezi hayo yaliyohudhuriwa na umati mkubwa wa watu walikuwa na mabango yenye maandishi la kwanza likiandikwa kichwa cha matembezi hayo, na kwenye bango kuu liliandikwa (siku 160 za vita dhidi ya Palestina. Enyi majeshi ya Waislamu, umewadia wakati wenu kurudisha utukufu wa Vita vya Hattin ili kuinusuru Gaza na kuikomboa Palestina) na bango la tatu liliandikwa (Mtume wa Mwenyezi Mungu (swt), anasema: “Hakika umekujieni Mwezi wa Ramadhan...basi muonyesheni Mwenyezi Mungu wema kutoka nafsini mwenu...”) na bango la nne liliandikwa (Takwimu za mashahidi na majeruhi..).
Maandamano hayo pia yalijumuisha kauli mbiu zilizokuwa zikiimbwa na umati, kama vile (Enyi wanazuoni wa Waislamu, zifanyeni fatwa zenu kutokana na damu ya Waislamu), (Ndani ya Ramadhan, ndani ya Ramadhan, inusuru Gaza, Ewe Mwingi wa Rehema), (Enyi Majeshi ya Waislamu, uko wapi uungwana, iko wapi dini), (Enyi askari wa Kiuthmani, Gaza na Palestina zinaita), (Watu wa Gaza watashinda kwa majeshi ya Waislamu), (Hala, hala kwenye jihad, enyi majeshi ya Waislamu), (Semeni Mwenyezi Mungu, semeni Mwenyezi Mungu kuhusu Gaza, hatutaiacha).
Matembezi hayo yalihitimishwa kwa hotuba mbili, ya kwanza iliyotolewa na shab mmoja miongoni mwa mashababu wa Hizb, ambapo alizungumzia ushindi wa Waislamu katika mwezi wa Ramadhan, na ulazima wa majeshi kusonga mbele katika mwezi huu uliobarikiwa kuinusuru Gaza na kuikomboa Palestina. Hotuba ya pili ilitolewa na shabat mmoja wa Hizb, ambapo aliwataka wanazuoni wa Waislamu kusema neno la haki kuhusiana na kile kinachotokea Palestina. Majeshi yanabeba jukumu la kuwanusuru ndugu zetu wa Gaza na kuinusuru Hizb ut Tahrir ili isimamishe Khilafah Rashida kwa njia ya Utume.
Hivyo basi, Hizb ut Tahrir inaendelea bila kuchoka kutoa wito kwa Waislamu na wanazuoni wao kuinusuru Gaza, na kila wakati inayawajibisha majeshi ya Waislamu udharura ulio thabiti wa kuinusuru Palestina, usiobadilika tangu kuasisiwa kwake.
Mwakilishi wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Tunisia
Ijumaa, 05 Ramadhan 1445 H sawia na 15 Machi 2024 M
- Sehemu ya Amali za Matembezi -
https://domainnomeaning.com/sw/index.php/dawah/tunisia/3831.html#sigProId9a85ad7652
- Alama Ishara za Amali -
#طوفان_الأقصى
#الجيوش_إلى_الأقصى
#الأقصى_يستصرخ_الجيوش
#AksaTufanı
#OrdularAksaya
#ArmiesToAqsa
#AqsaCallsArmies
Kwa maelezo zaidi tafadhali zuru mitandao ya Hizb ut tahrir / Wilayah Tunisia: