- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan:
Mkutano na Waandishi wa Habari “Makubaliano ya Entebbe, Bwawa la Al-Nahdha, na Kupuuza kwa Watawala Maslahi Muhimu ya Umma”
Hizb ut-Tahrir / Wilayah Sudan ilifanya mkutano na waandishi wa habari mnamo siku ya Jumamosi tarehe 23 Rabi’ al-Akhir 1446 H sawia na 10/26/2024 M katika afisi yake mjini Port Sudan, wenye kichwa: “Mkataba wa Entebbe, Bwawa la Al-Nahdha, na watawala kupuuza maslahi muhimu ya Umma”, ambapo msemaji rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Sudan, Ustadh Ibrahim Othman (Abu Khalil), alisema katika hotuba yake kwamba kuzungumzia mikataba ya maji na mabwawa ni jambo muhimu na la hatari, kwa kuzingatia kwamba maji ni jambo muhimu, na umo ndani yake uhai wa watu, bali uhai wote, Mwenyezi Mungu Mtukufu asema:
﴿وَجَعَلْنَا مِنَ الْمَاءِ كُلَّ شَيْءٍ حَيٍّ﴾
“Na tukajaalia kwa maji kila kilicho hai” [Al-Anbiya: 30]
Aligusia mikataba iliyohitimishwa kati ya nchi za Bonde la Mto Nile na jinsi mikataba hii ilivyobatilishwa kwa makubaliano mpya kama hayo yaliofanyika huko Entebbe nchini Uganda mwezi Mei 2010.
Abu Khalil alibainisha kwamba masharti hatari zaidi ya Makubaliano ya Entebbe ni haya yafuatayo:
1- Kukomesha hisa za kihistoria za Misri na Sudan, yaani mita za ujazo bilioni 55.5 kwa Misri, na bilioni 18.5 mita za ujazo kwa Sudan...
2- Makubaliano hayo pia yaliweka masharti ya kuundwa kwa tume, baada ya angalau nchi 6 kuridhia makubaliano hayo kupitia Mabunge yake...
Abu Khalil aliweka wazi njama dhidi ya haki za maji za Misri na Sudan, kiwango cha uzembe wa watawala wao, na msimamo wao dhaifu kuhusu njama zinazofanyika.
Pia alitaja miradi ya umbile la Kiyahudi ya kupata sehemu ya maji ya Mto Nile, yanayosafirishwa kwa mabomba, ila isipokuwa rai jumla nchini Misri ilikataa kabisa hili... na kueleza jinsi Rais wa zamani wa Misri Sadat alivyojaribu kudhibiti rai jumla ya watu wa Misri kwa hili, kwani ilisemwa kwamba “Anaota siku ambayo maji ya Nile yatafika Jerusalem.” Ili Waislamu wapate kutawadha kutoka humo na kuswali katika Msikiti wa Al-Aqsa.” Abu Khalil alisisitiza kuwa nchi zinazoitwa Mabonde ni zana tu zinazotumiwa kuweka shinikizo kwa Misri na Sudan katika maudhui ya Bonde la Mto Nile.
Abu Khalil alihitimisha hotuba yake kwa kusema: Lau Sudan na Misri zingekuwa sehemu ya Khilafah Rashida, zisingethubutu nchi duni, mabwana wa ukoloni na zana zake kutishia maslahi muhimu ya Khilafah, kama njama ovu dhidi ya Uislamu na Waislamu. Dola ya Khilafah ni dola ya kimfumo inayotaka kuchukua uongozi katika msimamo wa kimataifa, hivyo orodha ya maslahi muhimu ya Khilafah Rashida hudumu muda mrefu zaidi wala hayapungui, na kwanza hakuna nchi inayosubutu kutishia maslahi haya. Ni lazima kwa kila Muislamu kufanya kazi na wale wanaofanya kazi ya kuisimamisha kwa ajili ya maisha mazuri ya kumtii Mwenyezi Mungu, ambayo wakaazi wa mbinguni na ardhini wataridhika nayo.
Mwisho kulikuwa na maswali kadhaa ufafanuzi na mijadala kuhusu mada ya mkutano na yalijibiwa na Abu Khalil kwa njia ya kina na maridadi. Kuhitimisha mkutano na waandishi wa habari, mwendesha mkutano huo, Ustadh Yakub Ibrahim, aliwashukuru waliohudhuria kwa kuhudhuria na kushiriki.
Mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari
katika Wilayah ya Sudan
23 Rabi’ al-Akhir 1446 H sawia na 26/10/2024 M
- Video ya Mkutano na Waandishi wa Habari -
- Video Kamili ya Amali ya Mkutano na Waandishi wa Habari -
- Angazo la Chaneli ya Al-Hakim la Amali ya Mkutano na Waandishi wa Habari -
https://domainnomeaning.com/sw/index.php/dawah/sudan/4316.html#sigProIdc70651cf89
Kwa Maelezo Zaidi, Tafadhali Zuru Tovuti za Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan:
Tovuti Rasmi: Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan
Facebook: Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan
Youtube: Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan
Ukurasa wa Mashababu wa Hizb ut Tahrir katika Vyuo Vikuu vya Sudan