Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan:

Ugawanyaji kwa Mara ya Pili, wa Karatasi zenye Kupinga Mfumo wa Makubaliano!

Katika muendelezo wa kampeni inayofanywa na Hizb ut Tahrir/Wilayah ya Sudan dhidi ya mfumo wa makubaliano, hizb iligawanya karatasi kwa mara ya pili mnamo Jumanne tarehe 3/1/2023 M katika Msikiti Mkuu wa Khartoum, kuonyesha ufisadi wa kile kilichoelezwa katika makubaliano hayo, na miongoni mwa yaliyoelezwa ndani yake: Tukatae mfumo wa makubaliano hayo na tuyapinge... ndugu Muislamu ni kwa nini ni wajibu juu yako kisheria kukataa mfumo wa makubaliano hayo na kuyapinga? Kwa sababu yanabainisha katika ibara ya kwanza/6: [Kudhamini uhuru, na kuzingatia mikataba ya kimataifa ya haki za binadamu, hasa mikataba ya haki za wanawake], na hii ni kinyume na Aqida ya Kiislamu, kwani uhuru na mikataba yote ya kimataifa zinaruhusu uasi, na kutukana heshima ya Mtume (saw), upotovu, ulawiti, kumiliki mali kwa njia za haramu, na mengineyo katika maovu. Muislamu, awe mwanamume au mwanamke, ni mja wa Mwenyezi Mungu (swt), ambaye anasimama na maamrisho na makatazo ya Mwenyezi Mungu. Kadhalika, hairuhusiwi kushiriki katika mashirika ambayo yameegemezwa juu ya msingi usiokuwa Uislamu, na wala haijuzu kufuata mikataba yao.

Kwa fadhila za Mwenyezi Mungu (swt), waumini waliingiliana na karatasi hizi pamoja na kutoa dua za kufaulu na malipo kwa ajili ya jitihada hii adhimu ambayo hizb inaifanya katika Ummah ya kusimamisha Dola ya Kiislamu, Khilafah Rashida, kwa njia ya Utume.

Mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

katika Wilayah Sudan

- Ripoti ya Picha juu ya Ufanisi wa Amali ya Ugawanyaji Karatasi -

Kwa Maelezo Zaidi Zuru Mitandao ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan:

Tovuti Rasmi ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan

Ukurasa wa Facebook wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan

Chaneli ya YouTube ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan

Ukurasa wa Mashababu wa Hizb ut Tahrir katika Vyuo Vikuu vya Sudan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu