- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan:
Ripoti ya Habari 16/04/2022
Mnamo tarehe 15 Ramadhan 1443 H, katika Ukumbi wa Jiji la Dosa, Hizb ut Tahrir/Wilayah Sudan ilifanya iftar ya Ramadhan ya kila mwaka, iliyohudhuriwa na mkusanyiko mkubwa wa wanasiasa, wanahabari, wanazuoni, viongozi wa taasisi za kiraia, na wengineo wanaohusika na mambo ya umma, pamoja na mashababu wa Hizb ut Tahrir. Baada ya kufuturu na kuswali swala ya Maghrib, hafla ya kisiasa iliyopewa anwani
“Handaki la Mgogoro wa Kisiasa nchini Sudan, Lango Pekee la Kutokea ni Khilafah”
ikaanza. Hafla hii ilianza kwa kisomo cha Quran Tukufu na Sadiq Qasam Al-Sayyid – mwanachama wa Hizb ut Tahrir. Kisha Msaidizi wa Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan, akachukua usukani; Mzungumzaji wa kwanza, Mhandisi Basil Mustafa, aliwasilisha waraka wenye kichwa: "Mamlaka Iliyonyakuliwa ya Ummah ni chombo cha ushawishi wa kisiasa kwa ukoloni" ambayo Mhandisi Basil aliwasilisha maelezo kamili ya jinsi mamlaka yalivyo nyakuliwa na kafiri mkoloni, tangu kuvunjwa kwa dola ya Khilafah hadi leo, ambapo nchi za Magharibi zimekuwa zikinyakua mamlaka ya umma kwa kutumia zana.
Mhandisi Basil Mustafa
Mamlaka Iliyonyakuliwa ya Ummah ni chombo cha ushawishi wa kisiasa kwa ukoloni
Kisha waraka wa pili ulikuwa na kichwa: “Hadhara ya Magharibi Kafiri... mangati ambayo mwenye kiu kudhani kuwa ni maji,” ambapo wakili Ustadh Hatim Jaafar (Abu Awab) – mwanachama wa Hizb ut Tahrir, alieleza kwamba Umma wa Kiislamu umeishi katika kivuli cha hadhara ya kikafiri ya Magharibi kwa zaidi ya miaka mia moja hadi vizazi vikaibuka.
Ustadh Hatim Jaafar (Abu Awab)
Hadhara ya Magharibi Kafiri... mangati ambayo mwenye kiu kudhani kuwa ni maji
Kisha waraka wa tatu na wa mwisho ulikuwa na kichwa: "Khilafah... Lango la Kutoka Salama kutoka kwenye Handaki la Giza", ambao uliwasilishwa na Ustadh Ibrahim Othman (Abu Khalil), msemaji rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Sudan, akionyesha kwamba mfumo wa utawala katika Uislamu ni Khilafah, na ni uongozi mkuu kwa Waislamu wote duniani, ni faradhi, na ni dola ya kipekee katika umbo lake, vyombo na vifungu yake.
Ustadh Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Khilafah... Lango la Kutoka Salama kutoka kwenye Handaki la Giza
Ushiriki wa Hadhira
Kipindi cha Maswali na Majibu
Mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan
- Click to open image! Click to open image!

https://domainnomeaning.com/sw/index.php/dawah/sudan/2285.html#sigProId26cdd3b24a