Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan:

Ripoti ya Habari 19/02/2021

Mwendelezo wa amali za umma zinazofanywa na Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan katika majimbo na mikoa mbalimbali nchini ili kujenga rai jumla ambayo inajua tiba na hukmu za kisheria zinazohusiana na hali mbaya ambazo watu wanaishi, zikiwakilishwa na mbinyo wa bei ya juu inayotokana na bajeti iliyoidhinishwa kwa mwaka 2021 kulingana na maagizo ya Mfuko wa Fedha wa Kimataifa, na ukosefu wa usalama na mapigano kati ya makabila tofauti tofauti ... Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan - eneo la Khartoum walifanya muhadhara wa kisiasa mnamo Jumatatu, 18 Januari 2021, chini ya anwani: "Bajeti ya mwaka 2021 inasababisha umaskini na inaua masikini", ambapo Ustadh Fadlallah Ali Suleiman aliyeizungumzia, ambaye aliregelea bajeti zilizopita, ikiwemo bajeti ya 2018 ambayo ilisababisha kuanguka kwa serikali ya Al-Bashir na jinsi ilivyotegemea zaidi ushuru na forodha na moja ya matokeo yake ilikuwa kuondolewa kwa ruzuku ambayo ilisababisha kuanguka kwa serikali ya Bashir.

Chini ya anwani: "Bei za Juu, Sababu na Suluhisho," Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan katika mji wa Gadharef walifanya muhadhara wao wa kila wiki mnamo Alhamisi 21 Januari 2021, ambapo Ustadh Maysara Yahya alizungumza, akielezea sababu za bei ya juu, ambayo ilikuwa ndio sababu ya watu kuiacha serikali iliyopita wakitarajia kuibadilisha.

Katikati ya umati mkubwa wa watu, Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan - Jimbo la Al-Abyadh ilifanya muhadhara wa kisiasa mnamo Jumatano, 20 Januari 2021, yenye anwani: "Kumhisabu mtawala kwa udhalimu wake ni wajibu kwa Muislamu." Akifafanua hayo kwa ushahidi kutoka kwa Qur’an na Sunnah na kutaja mifano kutoka kwa Seerah. Ustadh Al-Nazir Muhammad alizungumza juu ya ukandamizaji wa watawala leo, akiwa na jukumu hilo.

Katikati ya umati mkubwa, Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilaya ya Sudan - eneo la Khartoum walifanya muhadhara wa kisiasa mnamo Jumatatu, 25 Januari 2021, chini ya anwani: "Mgogoro wa Mkate, mateso makali kwa sababu ya kufeli kwa serikali ya mpito, suluhisho ni nini? " Ustadh Ahmed Abakar Adam alizungumzia juu yake, ambaye alirejelea mgogoro huo wa mkate na kiwango cha mateso ambayo watu wanapata.

Katika mwendelezo wa suala la bajeti, na chini ya anwani: "Bajeti ya serikali ya kulipiza kisasi ya mwaka 2021 imegeuza maisha ya watu kuwa jahanamu," Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan - raia wa eneo hilo alifanya muhadhara wa kisiasa mnamo 25 Januari 2021 katika kituo cha basi, ambapo Ustadh Abdel Aziz alizungumza akielezea kupitishwa kwa bajeti kutoka mifuko ya maskini na wale wanaohitaji kulipa ada na ushuru ni haramu, ambapo ilisababisha kupanda kwa bei kwa kupitiliza.

Mnamo siku ya Jumatano, 27 Januari 2021, Hizb ut Tahrir / Wilaya ya Sudan - eneo la Al-Dukhainat ilifanya muhadhara wake wa kisiasa wa mara kwa mara katika soko la Al-Kalakila Al-Lafah kwa anwani: "Je! Khilafah Rashidah kwa njia ya Utume inashughulikia vipi migororo?" Ustadh Abdullah Hussein alizungumzia jinsi inavyoshughulikia migogoro ya nchi kama mkate, mafuta na mgogoro wa gesi ya kupika na bei kubwa za bidhaa na huduma.

Chini ya anwani: "Mgogoro wa Kiuchumi nchini Sudan, Sababu na Tiba," mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan katika eneo la Kosti, mnamo Jumatatu, 1 Februari 2021 katika Soko Kuu, walifanya muhadhara wa kisiasa ambapo Ustadh Musa Abkar alizungumzia juu ya mgogoro wa kiuchumi na sababu zake. Hii ni kama matokeo ya utegemezi wa serikali mtawalia juu ya kutawala nchi, wa sera na maagizo ya Mfuko wa Fedha wa Kimataifa na Benki ya Dunia.

Katika muktadha huo huo, Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan - eneo la Omdurman, magharibi mwa Omdurman, ilifanya muhadhara wa kisiasa Jumanne, 2 Februari 2021 chini ya anwani: "Bei za Juu, Sababu na Suluhisho," ambapo Ustadh Ishaq Muhammad Hussein alizungumza , ambaye alihakikia baadhi ya bei za bidhaa ambazo zilifikia idadi kubwa kupita kiasi.

Chini ya anwani: "Miaka Mia Bila ya Khilafah", Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan - eneo la Magharibi mwa Omdurman, baada ya alasiri ya Jumanne 19 Januari 2021, kusini mwa Hospitali ya Ombada, walifanya muhadhara wa kisiasa ambapo Sheikh Babiker Mahdi aliongea.

"Khilafah ilivunjwa vipi na Waislamu walipoteza nini kwa kuvunjwa Khilafah?!" Chini ya anwani hii, Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan - eneo la Al-Abyadh ilifanya muhadhara wa umma mnamo  Jumanne, 4 Rajab 1442 H – 16 Februari 2021, kwa mujibu wa kampeni ya mwezi wa Rajab 1442 Hijria, ambapo Ustadh Muhammad Quni alizungumza , akielezea mipango ya wakoloni na kulazimisha kuvunja Khilafah na kukatizwa na mgawanyiko ambao uliukumba Umma. Wakati mwingine ulitenganishwa na utaifa na mwingine na uzalendo, kama ambavyo Umma ulipoteza heshima na hadhi yake. Maingiliano yalikuwa mazuri kutoka kwa hadhira.

Na amali nyingi nyenginezo zilifanyika katika mwezi mzima wa Februari, zikipata mapokezi na maingiliano mazuri kutoka kwa watu.

And many more events took place throughout the month of February, receiveing a warm reception and interaction from the masses.

Mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan

Mkusanyiko wa Picha

Click to enlarge image 01_02_2021_SD_Pics_25.jpg

Click to open image!

 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu