Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Hizb ut Tahrir / Wilaya Pakistan:

Kwa Kubinafsisha Nishati na Madini, Serikali ya PTI inawapora Waislamu Utajiri Wao na Kukiuka Sunnah ya Mtume (saw)!

Japokuwa chini ya Ubepari, Pakistan ina uzito mdogo sana kiulimwengu kuliko vidola vidogo vyenye maliasili kidogo, kiasili imebarikiwa na Mwenyezi Mungu (swt) kwa rasilimali za nishati na Madini ya kutosha.

Hata hivyo, neema hizi za Mwenyezi Mungu (swt) zimefilisiwa kupitia kujisalimisha kwa PTI kwa Benki ya Dunia na Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF) na kutabikisha kwake Ubepari. Ubepari unasisitiza katika kukuza uhuru wa kumiliki, ambao hufungua milango kwa umiliki binafsi wa rasilimali nyingi za ummah, ambazo kimsingi hutegemewa na jamii nzima, kama vile nishati na madini.

Kwa miongo mingi ya ubinafsishaji wa sekta ya nishati, kampuni binafsi zinaendelea kujipatia faida kubwa, wakati viwanda vya ndani vinakufa na kilimo kina kwama kufikia uwezo wake kamili, ukosefu wa ajira unaongezeka na migongo ya watu inavunjika kwa gharama za matumizi zinazo endelea kuongezeka.

Enyi Waislamu wa Pakistan!

Sio tu kwamba ubinafsishaji wa nishati na madini unakandamiza jamii pekee, unakinzana na Sunnah ya Mtume (saw) na ni dhambi lenye kuadhibiwa na Mwenyezi Mungu (swt). ‘Amru bin Qays amesimulia,

اسْتَقْطَعْتُ رَسُولَ اللهِ صلى الله عليه و سلم مَعْدِنَ المِلْحِ بِمَأْرِبَ فَأَقْطَعَنِيهُ فَقِيلَ يَا رَسُولَ اللهِ إِنَّهُ بِمَنْزِلَةِ الْمَاءِ الْعَدِّ يعني أنه لا ينقطع فَقَالَ رَسُولُ اللهِ صلى الله عليه و سلم فَلاَ إِذَنْ

“Nilimuomba Mtume (saw) anipatie sehemu ya ardhi ambayo inachumvi na alinipatia. Ikasemwa, Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (saw), ina cheo cha maji yasiyo idadi - yaani kwa maana nyengine ni kwamba hayamaliziki – hivyo Mtume (saw) akasema, فَلاَ إِذَنْ kwa hali hiyo basi hapana”  [ Imesimuliwa na Al- Nasa’i].

Hivyo, kwa upekee kabisa Sunnah ya Mtume (saw) imeweka hukmu ya mali ya ummah, ambayo inatekelezeka kwa rasilimali za madini mengi mno. Mali ya ummah haiwezi kamwe kumilikiwa na aidha kibinafsi wala na serikali, manufaa ya mali ya ummah kwa jumla, ima kutoka katika mali ya ummah yenyewe au kutokana na thamani yake baada ya mauzo, ni kwa kuzingatia maslahi ya jamii.

Jumamosi, 30 Ramadhan 1441 H - Mei 23, 2020 M

#KataaUbepariSimamishaKhilafah

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu