Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Hizb ut Tahrir / Wilaya Pakistan:

Video fupi kuhusu Virusi vya Korona

Ama kuhusu kutoa pesa za kutosha kukabili milipuko kama hii, Uislamu umeuzidi sana Urasilimali, mfumo uliopo kwa sasa ulioundwa na mwanadamu ambao unatawala ulimwengu. Hakika, kulipuka kwa ugonjwa wa virusi vya Korona (Covid-19) umedhihirisha maumbile dosari na dhaifu ya uchumi wa kirasilimali.

Urasilimali huhakikisha kwamba sehemu kubwa ya utajiri wa nchi inakusanyika mikononi na kikundi cha watu wachache. Ni ukweli huu ndio uliozifanya dola za kirasilimali za Kimagharibi kushindwa kutekeleza wajibu wao kwa raia wao, na hali hii ikiwa ni mbaya zaidi nchini Pakistan. Hakika, Urasilimali wenyewe ni mzigo kwa wanadamu, ukiwalazimisha watu wachague baina ya njaa na virusi.

Mwenyezi Mungu (swt) Anasema, كَيْ لاَ يَكُونَ دُولَةً بَيْنَ الأَغْنِيَاءِ مِنْكُمْ وَمَا آتَاكُمْ “ili yasiwe (mali) yakizunguka baina ya matajiri tu miongoni mwenu.” [Al-Hashr 59:7]

Kwa kipekee kabisa Uislamu unapinga muundo wa kirasilimali wa ukuaji wa uchumi, ambao huangazia juu ya uzalishaji, kupitia muundo wa kiuchumi, unao angazia juu ya usambazaji na mzunguko wa utajiri.

Jumatano, 27 Ramadhan 1441 H  - 20 Mei 2020 M

#Covid19    #Korona     كورونا#

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumatano, 27 Mei 2020 15:32

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu