Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Hizb ut Tahrir / Wilayah Pakistan:

Maoni ya Habari 07/08/2024

Maoni ya habari ya Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan.

Kwa Mabadiliko ya Kweli… Kataeni demokrasia... Simamisheni Khilafah.

Ewe Mwenyezi Mungu, irudishe ngao yetu, Khilafah Rashida... Allahuma Ameen.

#BringBackKhilafah

Jumatano, 03 Safar Al-Khair 1446 H sawia na 08 Agosti 2024 M

Kuuawa shahidi Ismael Haniya ni Ukumbusho kwa Ummah Kukusanya Majeshi Yake.


Umbile la Kiyahudi lilimuua shahidi Ismael Haniya nchini Iran mnamo Julai 30, katika ukaidi mkali wa Umma na majeshi yake. Kuuawa kwake kishahidi ni ukumbusho kwa Umma na majeshi yake juu ya wajibu wa kuukomboa Al-Masjid Al-Aqsa. Umma lazima uyatake majeshi yake yawang'oe watawala wahalifu wanaozuia vita vya wazi dhidi ya umbile la Kizayuni. Majeshi lazima yatoe Nusrah yao kwa Hizb ut Tahrir kwa ajili ya kusimamisha tena Khilafah Rashida, ambayo italipa kisasi cha damu ya Waislamu iliyomwagika huko Gaza, Yemen, Syria na Iran. Amesema Mwenyezi Mungu (swt): وَلَا تَحْسَبَنَّ الَّذِينَ قُتِلُوا فِي سَبِيلِ اللَّهِ أَمْوَاتًا بَلْ أَحْيَاءٌ عِنْدَ رَبِّهِمْ يُرْزَقُونَ “Wala kabisa usiwadhanie walio uliwa katika Njia ya Mwenyezi Mungu kuwa ni maiti. Bali hao ni wahai, wanaruzukiwa kwa Mola wao Mlezi.” [Surah Aali Imran 3:169]

Khilafah Itauokoa Ulimwengu wa Kiislamu kutokana na Madeni kwa Kuifuta Riba


Mnamo tarehe 28 Julai 2024, Waziri wa Fedha alisema, “Hatuna chaguo zaidi la kufanya kile ambacho tumekuwa tukifanya hapo awali kwa unafuu na malengo ya muda mfupi.” Kilichofanyika siku za nyuma hakijafanya kazi, kwa sababu Riba inahakikisha Pakistan inasalia kwenye mtego wa madeni. Jumla ya deni lililobaki kati ya 1990-2000 lilikuwa dolari bilioni 15,451, ingawa katika kipindi kama hicho jumla ya kiasi kilicholipwa kilikuwa $36,111 bilioni. Kufikia Disemba 2023, jumla ya deni la nje la Pakistan lilikuwa $131.159 bilioni. Jumla ya deni la Pakistan lilifikia kiwango cha rekodi kufikia Mei 2024. Ni wazi kwamba malipo ya riba katika kulipa deni hayaruhusu Pakistan kuepuka deni linaloongezeka. Hata hivyo, kuna chaguo. Waislamu lazima wasimamishe tena Khilafah Rashida itakayoondoa dhambi la Riba.

Khilafah Rashida Itawalipiza Kisasi Mashahidi wa Ardhi Zilizobarikiwa


Mnamo tarehe 31 Julai 2024, Wizara ya Mambo ya Nje ya Pakistan ilisema, “Pakistan inalaani mauaji ya Ismail Haniyeh, Mkuu wa Afisi ya Kisiasa ya Hamas jijini Tehran.” Watawala wa Waislamu wanatoa shutuma zisizo na maana, huku adui Mzayuni anakiuka kikamilifu ardhi, damu na heshima ya Waislamu. Mtume (saw) alikusanya nguvu za kijeshi kulifukuza kabila la Kiyahudi la Qaynuqa, baada ya kumvunjia heshima mwanamke mmoja wa Kiislamu na kumuua shahidi mwanamume mmoja Muislamu. Khilafah kwa Njia ya Utume itakusanya majeshi na mujahidina kupigana na makafiri hadi Fitna yao iondolewe. Amesema Mwenyezi Mungu وَقَـٰتِلُوهُمۡ حَتَّىٰ لَا تَكُونَ فِتۡنَةࣱ وَیَكُونَ ٱلدِّینُ كُلُّهُ لله “Na piganeni nao mpaka isiwepo fitna na mateso, na Dini yote iwe kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. [Surah Al-Anfaal 8:39]

Serikali Haitafuta Makubaliano na Wazalishaji Huru wa Umeme (IPPs) Hata Inasababisha Kuyumba Kisiasa


Mnamo tarehe 31 Julai, 2024, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Shirikisho alisema, “Kila mtu ana kutoridhishwa kuhusu IPPs na Waziri Mkuu ameanzisha mchakato wa mashauriano ili kusuluhisha suala hili.” Serikali inashughulikia tatizo la umeme ndani ya muundo wa mfumo wa kibepari. Katika ubepari, wakati sehemu ya kipote cha mabepari inakusanya utajiri mkubwa, suluhisho ni kugawanya upya baadhi ya faida zake kwa umma, ama kwa kupunguza faida zake kwa muda au kwa kutoa ruzuku. Mbinu hii inaruhusu mfumo wa kibepari kubakia hai na kuendelea. Hakuna haja ya kushauriana kwa kuwa Uislamu unatoa hukmu ya wazi ya Shariah kuhusu kawi, ikiiweka kama mali ya umma itakayosimamiwa na serikali. Kwa mujibu wa hukmu hii ya Shariah, mapato kutoka sekta ya kawi lazima yatumike kwa mahitaji ya umma pekee, na ubinafsishaji wake ni kinyume cha sheria.

Ukombozi wa Kashmir Inayokaliwa ni Wajibu wa Sharia kwa Wanajeshi wa Pakistan


Miaka mitano baada ya kubatilishwa hadhi maalum ya kujitawala ya Kashmir inayokaliwa kimabavu mnamo tarehe 5 Agosti 2019, vikosi vya usalama vya India vinaendelea kutekeleza sera za ukandamizaji, ikiwa ni pamoja na kuwekwa kizuizini kiholela, mauaji ya kiholela, na ukiukwaji mwengine mkubwa. Hata hivyo, kwa mujibu wa amri za mabwana zao wa Kimarekani, watawala wa Pakistan wanazuia majeshi yetu, wakiwapa askari waoga wa Kibaniani fursa ya kueneza Fitna kwenye Ardhi ya Kiislamu. Amesema Mwenyezi Mungu ﷻ وَٱقۡتُلُوهُمۡ حَيۡثُ ثَقِفۡتُمُوهُمۡ وَأَخۡرِجُوهُم مِّنۡ حَيۡثُ أَخۡرَجُوكُمۡۚ وَٱلۡفِتۡنَةُ أَشَدُّ مِنَ ٱلۡقَتۡلِۚ “Na wauweni popote mwakutapo, na muwatoe popote walipo kutoeni; kwani fitina ni mbaya zaidi kuliko kuuwa.” (Sura al-Baqarah 2:191). Ummah na majeshi yake lazima wawang'oe watawala vibaraka na kusimamisha Khilafah Rashida. Khilafah Rashida itakusanya majeshi na mujahidina kukomboa ardhi zote zinazokaliwa kwa mabavu.

Marekani Yafanya Vita dhidi ya Gaza kwa Usaidizi wa Viabaraka wake Miongoni mwa Watawala wa Mayahudi na Waislamu


Mnamo tarehe 2 Agosti 2024, Wizara ya Ulinzi ya Marekani ilitangaza kupelekwa kwa manuari za Marekani katika Mashariki ya Kati, ikisema ni, “kuongeza uungaji mkono kwa ulinzi wa 'Israel,” na kuhakikisha Marekani iko tayari kukabiliana na dharura mbalimbali.” Vita huko Gaza sio kati ya Waislamu wa Palestina na umbile la Kiyahudi peke yao. Marekani hulipatia umbile la Kiyahudi silaha na ufadhili, pasi kwazo ingeshindwa. Marekani inawaamuru watawala wa Waislamu kuzuia majeshi na mujahidina kutokana na kulishinda umbile la Kiyahudi. Marekani huongeza uwepo wake wa kijeshi pindi inapohisi tishio kwa vibaraka wake. Ni juu ya majeshi ya Waislamu, na mujahidina wao, kutoa Nusrah yao kwa Hizb ut Tahrir kwa ajili ya kusimamisha tena Khilafah Rashida ili kuwashinda wapiganaji wa msalaba wa Marekani.

Funzo kwa Waislamu wa Pakistan kutokana na Mabadiliko nchini Bangladesh


Mnamo tarehe 5 Agosti 2024, Waziri Mkuu wa Bangladesh alikimbilia India kwa helikopta, baada ya wiki kadhaa za maandamano mabaya ya umma, yaliyoungwa mkono na baadhi ndani ya vikosi vya jeshi. Lau kama maafisa wa jeshi hawakuwaunga mkono waandamanaji wa kiraia, kungekuwa na umwagaji mkubwa wa damu. Waislamu wa Pakistan wanakabiliwa na ukandamizaji, taabu na fedheha zile zile wanazokabiliwa ndugu zao Waislamu nchini Bangladesh. Raia wa Kiislamu lazima wapaze sauti zao kwa ajili ya kukomesha dhulma, kwa kuasisi hukmu kwa yale yote aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu ﷻ. Maafisa wa kijeshi wa Kiislamu lazima watoe msaada wao wa kimada kwa ajili ya kusimamishwa Khilafah Rashida. Ni lazima watoe Bayah yao ya Nusrah kwa Hizb ut Tahrir, ili hatua za mabadiliko ya kweli ziweze kupangiliwa, kwa kufuata nyayo za wapiganaji wa Answaar, chini ya imarah ya Mtume ﷺ.

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu