Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Hizb ut Tahrir / Wilayah Pakistan:

Maoni ya Habari 14/06/2023

Maoni ya Habari ya Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan.

Kwa Mabadiliko ya Kweli... Kataeni demokrasia... Simamisheni Khilafah.

Ewe Mwenyezi Mungu, turegeshee ngao yetu, Khilafah Rashida... Allahumma Ameen.

#BringBackKhilafah

Jumatano, 25 Dhul Qa'adah 1444 H sawia na 14 Juni 2023 M

Khilafah Pekee Inaweza Kuwaokoa Waislamu kutoka kwa Raj Mkoloni wa Kibaniani Anayekua

Mnamo tarehe 5 Juni 2023, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani alitangaza, "Ushirikiano wetu na India ni mojawapo ya muhimu zaidi." Marekani inaijenga India kukabiliana na China na Waislamu. Marekani inatumia muungano wake na Pakistan kuiondoa kama kikwazo. Waislamu kutoka Burma hadi Kandahar lazima waokolewe kutoka kwa utiishaji wa India. Uislamu pekee ulihakikisha kwamba Waislamu wanatawala kwa karne nyingi katika eneo hili. Khilafah ndiyo itakayounganisha rasilimali na nguvu za Waislamu ili kukabiliana na maadui zao.

19 Dhul Qa'adah 1444 H sawia na 08 Juni 2023 M

Bila ya Kukomeshwa kwa Riba, Pakistan Haiwezi Kuepuka Mtego wa Madeni


Jumla ya deni liliongezeka kwa asilimia 34.1 mwaka hadi mwaka, hadi trilioni 58.6, mwishoni mwa Aprili, kulingana na data iliyotolewa na Benki Kuu ya Pakistan mnamo tarehe 5 Juni 2023. Mfumo wa uchumi wa Kibepari huongeza tu deni kwa sababu ya riba. Nchi yenye uchumi mkubwa zaidi wa kibepari duniani, Marekani, daima huwapandisha kiwango cha madeni. Suluhisho sio kuongeza Pato la Taifa, kuongeza mauzo ya nje au kuongeza uwiano wa kodi kwa Pato la Taifa. Riba lazima ikomeshwe na ni Khilafah pekee ndiyo itakayofanya hivyo.

20 Dhul Qa'adah 1444 H sawia na 09 Juni 2023 M

Kukuza Uzalishaji Viwandani kunahusiana na Ufadhili, sio tu Mafunzo ya Uzalishaji


Mnamo tarehe 6 Juni 2023, serikali ilitangaza Shirika la Uzalishaji wa Kitaifa (NPO). Inalenga "kuboresha ushindani kupitia uzalishaji endelevu wa kitaifa." Uzalishaji unahusu kuongeza faida kwa kulinganisha na gharama za uzalishaji. Walakini, mpango huo utafeli. Serikali imeongeza ushuru kwa viwanda, ili kukidhi malipo ya riba kwa mikopo. Serikali imeruhusu kudhoofika kwa Rupia, ambayo imeongeza mfumko wa bei na gharama ya uzalishaji viwandani. Ni Khilafah ndiyo itakayoimarisha viwanda, kupitia ufadhili usio na riba na sarafu thabiti ya dhahabu na fedha.

21 Dhul Qa'adah 1444 H sawia na 10 Juni 2023 M

Ruwaza ya Jeshi la Kiislamu haikufungika na Mipaka ya Kitaifa


Mnamo 7 Juni 2023, mkuu wa majeshi alitangaza “Jeshi la Pakistan litaendelea kujitolea katika majukumu yake ya kitaifa ya kulinda hadhi na ubwana wa eneo lake.” Baada ya kuvunjwa Khilafah, ulimwengu wa Kiislamu uligawanyika dola za kitaifa hamsini na tano. Kila jeshi lilijifunga binafsi kuhami mipaka ya dola yake. Hata hivyo, Uislamu unakataa utaifa na dola ya kitaifa. Unaamrisha dola moja ya Khilafah kwa Waislamu wote. Majeshi yake hayafungiki na mipaka ya kitaifa katika kuzikomboa ardhi zinazokaliwa kimabavu na kuzifungua ardhi mpya katika Uislamu.

22 Dhul Qa'adah 1444 H sawia na 11 Juni 2023 M

Ziunganisheni Dola 55 za Waislamu kuwa Khilafah Moja kwa Ustawi wa Kiuchumi


Mnamo tarehe 8 Juni 2023, Pakistan ilitia saini "Mpango wa Utekelezaji wa Bomba la Gesi wa TAPI (JIP)" pamoja na Turkmenistan. Hakika Mwenyezi Mungu ﷻ ameujaalia Ulimwengu wa Kiislamu nishati na rasilimali nyingi za madini. Hata hivyo, rasilimali hizo zimegawanywa kati ya mataifa hamsini na tano, na kudhoofisha kila moja yao. Khilafah ilikuwa na uchumi imara zaidi duniani kwa karne nyingi. Moja ya mambo ni kwamba Uislamu unawajibisha umoja kwa Waislamu. Khilafah itakusanya rasilimali zote za Umma wa Kiislamu tena. Itakuwa na hazina moja ya dola kuwasimamia Waislamu.

23 Dhul Qa'adah 1444 H sawia na 12 Juni 2023 M

Bajeti ya Serikali ya Majimbo ya Pakistan Inaubadilisha Uchumi kuwa Mashini ya Pesa kwa Wawekezaji katika Madeni.


Matumizi ni Rupia bilioni 13,320, huku malipo ya riba ni Rupia bilioni 7,303, ambayo ni ongezeko la 85% kutoka mwaka jana. Malipo ya riba ni ya juu kuliko nakisi jumla ya bajeti, bilioni 6,923. Ili kukidhi malipo ya riba, IMF inadai ongezeko la ushuru, ambalo litaunyonga uchumi hata zaidi. Hakuna njia ya kuokoka ila kusimamisha tena Khilafah (Ukhalifa) kwa Njia ya Utume. Khilafah ndiyo itakayoondoa riba na kukomesha ufujaji fedha kutoka kwa maafisa na watawala wafisadi.

24 Dhul Qa'adah 1444 H sawia na 13 Juni 2023 M

Khilafah Kamwe Haitakabidhi Wanajeshi Wake kwa Umoja wa Mataifa


Mnamo tarehe 10 Juni 2023, Misheni ya Kudumu ya Pakistan katika Umoja wa Mataifa ilithibitisha kwamba zaidi ya Wapakistani 200,000 wamehudumu katika Misheni 46 za Umoja wa Mataifa, kote duniani katika miongo sita, na kupoteza askari wetu 171. Watawala wa Pakistan hutuma wanajeshi wetu kutekeleza mipango ya wakoloni kote ulimwenguni ili kuchuma dolari. Walakini, wanawazuia wanajeshi wetu kuikomboa Kashmir na Palestina. Khilafah itakata mafungamano na Umoja wa Mataifa, itazikomboa ardhi zinazokaliwa kwa mabavu na kufungua ardhi mpya kwa Uislamu.

25 Dhul Qa'adah 1444 H sawia na 14 Juni 2023 M

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu