Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Hizb ut Tahrir/ Wilayah Pakistan: Maoni ya Habari 03/03/2023

Maoni ya Habari ya Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan.

Kwa Mabadiliko ya Kweli... Kataeni demokrasia... Simamisheni Khilafah.

Ewe Mwenyezi Mungu, irudishe ngao yetu, Khilafah Rashida... Allahuma Ameen.

#BringBackKhilafah

Ijumaa, 11 Shaaban 1444 H sawia na 03 Machi 2023 M

Uongozi wa Pakistan Unatoa Msaada Muhimu wa Kijeshi kwa Ukraine, Huku Ukiitelekeza Kashmir Iliyokaliwa Kimabavu na Al-Masjid Al-Aqsa kwa Makafiri Wavamizi

Balozi na Mkuu wa Ujumbe wa Muungano wa Ulaya nchini Pakistan, Dkt Riina Kionka, alisisitiza mnamo 21 Februari 2023 kwamba, "Pakistan imetoa misaada ya kibinadamu pamoja na usaidizi wa kijeshi kwa Ukraine." Licha ya kukataa kwa Afisi ya Mambo ya Nje, inajulikana kuwa amri iliyotolewa na Pakistan sasa iko katika orodha ya kijeshi ya Ukraine. Kikundi cha Mawasiliano cha Ulinzi cha Ukraine huratibu usaidizi wa kijeshi kutoka kwa dola muhimu za vibaraka wa Marekani. Ilhali, watawala wa Pakistan wanazuia majeshi yetu yaliyo tayari kutokana na ukombozi wa Al-Aqsa na Kashmir Iliyokaliwa kwa mabavu. Khilafah itakata misaada yote ya kijasusi na kijeshi kwa miradi ya Magharibi. Badala yake, itapeleka jeshi kukomboa Srinagar na Al-Quds.

Jumatatu, 29 Rajab 1444 H - 24 Februari 2023 M

Kusawazisha Kati ya Marekani na China ni Juhudi za Ovyo. Uunganisheni Ulimwengu wa Kiislamu chini ya Khilafah ili iwe Dola Yenye Nguvu, Inayojitegemea

Uongozi wa Pakistan uko chini ya shinikizo kubwa kuisaidia Marekani, katika mzozo wake wa kimataifa na China. Marekani inaitaka Pakistan izuie mahusiano na China, huku ikiunda kambi ya kupambana na China, pamoja na India, Korea Kusini, Taiwan na Japan. China imeiingiza Pakistan katika mtego wa madeni yenye riba, huku ikitoa fedha za kigeni zinazohitajika zaidi. Dola kubwa za kikoloni zinahakikisha makubaliano makubwa kutoka kwa nchi kama Pakistan, Bangladesh, Afghanistan na India, na sio usawa. Mfumo  wa kilimwengu wa kiliberali, wa kikoloni huwadhuru Waislamu kila wakati. Khilafah itatutia nguvu, kwa kuunganisha rasilimali kubwa na mbalimbali za Ummah, hivi karibuni inshaa Allah. Hapo ndipo Uislamu utatawala ulimwengu, tena, kama ulivyokuwa kwa karne nyingi nyuma.

Jumamosi, 05 Sha'aban 1444 H - 25 Februari 2023 M

Marekani Haijali Kuhusu Malalamiko ya Pakistan Dhidi ya India. Khilafah Pekee ndiyo Inayoweza Kukabiliana kwa Ufanisi na Muungano wa Kimkakati wa Marekani na India

Marekani inataka India kuinuka katika utawala wa kikanda ili kukabiliana na China na Waislamu. Inaunda mzozo wa kiuchumi ili kupunguza ufadhili wa jeshi la Pakistan, huku ikifadhili na kuipa India silaha. Inawataka wanajeshi wa Pakistan kubaki kwenye mpaka wa Magharibi, katika mzozo na Afghanistan, huku wakiiacha Kashmir Iliyokaliwa kimabavu na India. Inaruhusu India kujenga mabwawa kwenye vyanzo vya maji vya Pakistan, huku ramani za Pakistan zikizunguka bila Azad (Iliyo kombolewa) Kashmir. Hali imekosa matumaini, ikiwa hatutajifunza somo letu na kuugeukia Uislamu. Ni Khilafah pekee ndiyo itakayounganisha Pakistan, Afghanistan, Asia ya Kati, Bangladesh na Ghuba, kuwa dola yenye nguvu, kupata utawala wa Uislamu.

Jumapili, 06 Sha'aban 1444 H - 26 Februari 2023 M

Baada ya Mistari Mekundu ya Kashmir Iliyokaliwa kimabavu, Afghanistan na Uchumi Kuvukwa, Je, Maji Yetu Yanafuata?

Serikali ya India inafanya ujenzi kwenye usambazaji wa maji wa Pakistan, huku ukiomba mazungumzo juu ya Mkataba wa Maji wa Indus. Kama vile wale wanaoikalia kimabavu Al-Quds wanavyofanya, Wahindi wanabadilisha hali halisi iliyoko, kabla ya mazungumzo, kwa msaada wa wakoloni. Tayari, kwa utiifu mpofu kwa taasisi za kikoloni, uongozi wa Pakistan umesimamia kupotea kwa Kashmir Inayokaliwa kimabavu, mafungamano na Afghanistan na ustawi wa kiuchumi. Sasa, huku tukidumisha imani katika zana za wakoloni, inaruhusu kuhujumiwa kwa usalama wetu wa maji. Ni Khilafah pekee ndiyo itakayoikomboa Kashmir Inayokaliwa kimabavu na kulinda usambazaji wa maji, kabla ya kuregesha utawala wa Uislamu juu ya Bara Ndogo zima la India.

Jumatatu, 07 Sha'aban 1444 H - 27 Februari 2023 M

Ni Mfumo wa Kiuchumi wa Wakoloni ndio Ambao Uliharibu Uchumi Wetu. Uchumi wa Kiislamu wa Khilafah Unahakikisha Ufanisi

Pakistan kamwe haitawahi kuepuka mtego wa madeni ya wakoloni. Sehemu kubwa ya kodi inatumika kulipa riba, lakini deni la taifa linaendelea kukua. Mnamo 1971, deni la Pakistan lilikuwa rupia bilioni 30. Sasa, ni zaidi ya rupia bilioni 50,000. Wakoloni wananyonya uchumi wetu, hivyo wawekezaji wa madeni wanakuwa matajiri wakubwa. Kisha wanaweka masharti ya IMF ambayo yanaharibu uchumi wetu na kijeshi. Khilafah ndiyo itakayondoa riba, na kuzikamata mali za mafisadi, ili kumaliza deni. Khilafah itaanzisha viwanda vizito ili kukomesha utegemezi wa bidhaa ghali kutoka nje. Itaunganisha Ardhi za Waislamu ili kawi iwe bidhaa ya ndani, sio bidhaa ya gharama kubwa kutoka nje.

Jumanne, 08 Sha'aban 1444 H - 28 Februari 2023 M

Matumaini katika Mfumo Dhalimu wa Kiliberali wa Kiulimwengu ni Mabaya. Hebu na tuweke Matarajio Yetu katika Hukmu kwa yale YoteAliyoyateremsha Mwenyezi Mungu

Ni kwa nini ni lazima tuwe na tumaini katika mfumo wa kiulimwengu wa kiliberali? Ni mfumo wa kiulimwengu ulioundwa na dola kubwa za kikoloni, ili kunyonya ulimwengu mzima. Umezitumbukiza nchi nyingi za dunia katika madeni makubwa yasiyoepukika, huku zikinyonya rasilimali zao. Hali sasa ni mbaya zaidi kuliko hapo awali. Marekani yenyewe iko katika hali tete ya kiuchumi. Sasa inakabidhi miradi yake kwa watawala wa Waislamu, huku ikisisitiza walipe kutoka mifukoni mwa Waislamu. Ni wakati sasa wa kuweka matumaini pale panapobidi kuwekwa, kwa Mwenyezi Mungu ﷻ na Dini tukufu aliyotuchagulia. Simamisheni tena Khilafah Rashida, ili hatimaye tuhakikishe rehema kwa wanadamu, kama tulivyofanya kwa karne nyingi zilizopita.

Alhamisi, 10 Sha'aban 1444 H - 02 Machi 2023 M


Mnamo Tarehe 3 Machi 1924, Makafiri Wakoloni Waliweza Kuiondoa Dola ya Kiislamu ya Khilafah

Hapo ndipo historia ya Ummah ilipotiwa giza. Hapo awali, Khilafah ilikuwa dola ya Ummah, iliyosimama juu ya haki na uadilifu. Lakini sasa Ummah una zaidi ya vipande hamsini kama dola, na madhara makubwa kutoka kwa watawala wao. Hapo awali, makafiri wakoloni walikuwa wakijua kwamba ukiukaji wowote wa matukufu ya Uislamu na Waislamu, ungekabiliwa na kukatwa ndimi na kuvunjwa viungo... Hata hivyo, leo hii, Quran Tukufu, Mtume (saw) na Ardhi za Waislamu zinashambuliwa, huku uchokozi huu ukiwa haulipizwi! Hii ni kwa sababu tu hakuna Imam, Khalifa Rashid (Khalifa Aliyeongoka), ambaye anaulinda Ummah kutokana na shari za maadui.

Ijumaa, 11 Sha'aban 1444 H - 03 Machi 2023 M

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu