Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

  Hizb ut Tahrir/ Wilayah Pakistan:

Mabango ya Ramadhan 1443 H - 2022 M

Hizb ut Tahrir / Wilayah Pakistan inaendesha kampeni ya mitandao ya kijamii katika mwezi mtukufu wa Ramadhan. Nyenzo za kampeni zina mafunzo muhimu kwa Waislamu kuhusu Imani yao, matendo yao, historia yao tukufu na wajibu wao wa kusimamisha tena Uislamu kama mfumo kamili wa maisha. Mwenyezi Mungu (swt) atukubalie matendo yetu ya utiifu.

#RamadhanDemandsAction

#Time4Khilafah

Jumamosi, 1 Ramadhan 1443 H - 2 Aprili 2022 M

Namna ya Kupata Uchamungu (Taqwa)

Taqwa ni kukinga Ghadhabu ya Mwenyezi Mungu (swt). Taqwa haiwezekani bila ya kutimiza maamrisho ya Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume wake (saw). Ni kujidanganya kungoja hadi Taqwah ijitokeze kwa ghafla, na matendo mema yajitokeze yenyewe. Uchamungu ni tunda la Imani. Kuzitafakari Alama za Mwenyezi Mungu (swt) na kuikumbuka Siku ya Kiyama kunatilia nguvu utiifu kwa Mwenyezi Mungu (swt). Basi ni jambo lisilokuwa na budi kufanya amali kivitendo, kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu (swt). Kwa hivyo, enyi Waislamu, tuzingatie Imani yetu Ramadhan hii, ili tutembee kwa uthabiti katika kumcha Mwenyezi Mungu (swt).

Jumapili, 2 Ramadhan 1443 H - 3 Aprili 2022 M

Maana ya Iman kwa Mitume (as)

Iman kwa Mitume (as) sio Imani tu katika utakatifu wa viumbe fulani pekee. Iman kwa Mitume (as) inathibitisha kwamba akili ya mwanadamu haina uwezo wa kupata tiba sahihi ya matatizo ya maisha. Mwanadamu anahitaji mwongozo wa Wahyi katika mambo ya maisha. Mfumo wowote unaoipa akili ya mwanadamu mamlaka ya kuamua sheria za maisha, moja kwa moja unakinzana na kanuni msingi za Uislamu. Tafakari, je huo sio uhalisia wa demokrasia?!

Jumatatu, 3 Ramadhan 1443 H - 4 Aprili 2022 M

Mwezi Mtukufu wa Ramadhan Huzuia Iman Kumomonyoka

Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesama, «إنَّ الإيمانَ لَيَخْلَقُ في جَوْفِ أحدِكُمْ كَما يَخلَقُ الثّوبُ» "Hakika, Iman huchakaa katika kifua cha mmoja wenu, kama inavyochakaa nguo." [At-Tabarani]. Mwezi mtukufu wa Ramadhan ni fursa kutoka kwa Mwenyezi Mungu (swt) ya kujadidisha Iman yetu kupitia Kufunga, Qiyam ul Layl, kukumbuka Akhera na kutafakari Wahyi kutoka kwa Mwenyezi Mungu (swt). Waislamu wenye uchamungu (Taqwa) hutaraji Usaidizi na Nusra ya Mwenyezi Mungu (swt). Waislamu wachamungu hawako tayari kulegeza msimamo katika hukmu yoyote ya Uislamu, wala kupuuza jukumu la kuwahisabu watawala madhalimu.

Jumanne, 4 Ramadhan 1443 H - 5 Aprili 2022 M

Kuamrisha Mema na Kukataza Maovu Huzuia Ufisadi wa Jamii

Kama ambavyo Mwenyezi Mungu (swt) amewajibisha Waislamu Swalah, Saumu na Zakah, pia (swt) ameamrisha kuamrisha mema na kukataza maovu katika dhurufu zote bila ya kujali matokeo yake. Mwenyezi Mungu (swt) amesema:

  [وَلْتَكُنْ  مِّنْكُمْ  اُمَّةٌ  یَّدْعُوْنَ  اِلَى  الْخَیْرِ وَ یَاْمُرُوْنَ بِالْمَعْرُوْفِ وَ یَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنْكَرِؕ وَ اُولٰٓىٕكَ هُمُ الْمُفْلِحُوْنَ]

"Na uwe kutokana na nyinyi umma unao lingania kheri na unao amrisha mema na unakataza maovu. Na hao ndio walio fanikiwa." [Surah Aali Imran 3:104]. Licha ya kuishi chini ya kivuli cheusi cha mfumo wa kikafiri na kustahamili uvamizi wa kithaqafa wa Makafiri kwa miongo kadhaa, kuamrisha mema na kukataza maovu kumehakikisha kwamba maovu bado yangali yanazingatiwa kuwa maovu, huku wema yakizingatiwa kuwa mema, katika Ulimwengu wa Kiislamu mpaka leo. Na ni amri hii ambayo hatimaye itapelekea kusimamishwa dola kwa msingi wa Uislamu.

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu