Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Hizb ut Tahrir / Malaysia (HTM)

Ripoti Maalum juu ya Maandamano na Kukabidhi Risala kwa Ubalozi wa Uswidi na Uholanzi

Kufuatia matukio mawili tofauti yaliyohusisha kitendo cha kinyama na cha uoga cha kutusi kupitia kuchoma moto nakala ya Quran, Hizb ut Tahrir/Malaysia (HTM) ilifanya maandamano ya amani na kuwasilisha risala za maandamano kwa Balozi za Uswidi na Uholanzi jijini Kuala Lumpur.

Maandamano kuelekea ubalozi wa Uswidi yalifanyika mnamo Ijumaa, 27 Januari 2023 M ambapo takriban watu 80 walikusanyika mbele ya ubalozi huo kulaani kitendo cha kinyama cha uchomaji Quran cha Rasmus Paludan. Ambapo Ustadh Umar Hussein alitoa kalima na kisha ujumbe wa Hizb ut Tahrir / Malaysia kuwasilisha risala ya kulaani kwa Bw. Robert Lejon aliyeipokea kwa niaba wa ubalozi huo.

Baada ya swala ya Ijumaa, maadamanano yalifanyika kuanzia Msikiti wa Tabung Haji hadi ubalozi wa Uholanzi jijini Kuala Lumpur kulaani kitendo cha kioga cha Edwin Wagensveld cha kuichana na kuikanyaga Qur’an. Baada ya kuwasili, ujumbe wa HTM uliwasilisha risala kwa Bi. Eva Oskam, mwakilishi wa ubalozi wa Uholanzi.

Mbali la kulaani vitendo vya kuitusi Qur’an, HTM pia ilikashifu qaida ya uhuru wa kuzungumza inayobebwa na Magharibi vitendo vya kinyama kama hivi kutokea na kusisitiza umuhimu wa mapambano ya kuregesha Khilafah kwa njia ya Utume itakayohami utukufu wa Qur’an na kuwalinda Waislamu kutokana na kutusiwa kwa namna hii.

Katika maandamano haya, mamia ya watu walijitokeza huku wakipaaza miito na mabango ya kulaani vitendo hivyo.

Mashababu waandamana kuelekea Ubalozi wa Uholanzi baada ya swala ya Ijumaa.

Ustadh Muhammad akikabidhi risala kwa Bi. Eva Oskam mwakilishi wa Ubalozi wa Uholanzi.

Ustadh Umar Hussein akiongoza maandamano huku wakitamka na kulaani serikali ya Uswidi na Uholanzi kwa kuruhusu kitendo kama hicho cha kinyama.

Ustadh Mu’az Abu Talhah akitoa hotuba ya wazi baada ya kupeana risala katika Ubalozi wa Uholanzi.

Ustaz Mu’az Abu Talhah akitoa hotuba ya wazi baada ya kupeana risala katika Ubalozi wa Uswidi.

Mashababu wakiwa mbele ya Ubalozi wa Uswidi

Mashababu wakilaani mbele ya Ubalozi wa Uswidi

Ripoti maalum juu ya maandamano na uwasilishaji wa risala kwa balozi za Uswidi na Uholanzi

Katika ripoti yake, kituo cha runinga cha serikali kiliangazia maandamano mithili ya haya ya mashirika mengine yasiyo ya kiserikali lakini kilionyesha mabango yetu nyuma yake

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Malaysia

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu