Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 HizbutTahrir Canada:

Kutoka George Floyd hadi Malcolm X; Kwa Nini Uislamu ndiyo njia pekee ya Waamerika wenye Asili ya Kiafrika?

Kusimamisha nidhamu za Kiislamu ndiyo njia pekee ya ukombozi kwa watu wote, hususan Waamerika wenye asili ya Kiafrika, kwa kuonesha kwamba uraia wa daraja la pili ni wa kudumu. Suala hili litaangaziwa vizuri katika video kadhaa zifuatazo.

Ijumaa, 21 Shawwal 1441 H  -  12 Juni 2020 M

-Sehemu ya Kwanza-

Sehemu hii inaanzia kutoka utumwani hadi miaka ya sabiini ili kuonesha namna mfumo wa Kirasilimali wa Amerika ulivyo buni ubaguzi wa rangi ili kusababisha migawanyiko baina ya masikini, namna alivyo sema Martin Luther King kwamba harakati za haki za raia zinaweza kushindwa kuwakomboa watu weusi kwa sababu hazielezei umasikini wa watu weupe, na namna wana Republican walivyotumia ubaguzi wa rangi kushinda uchaguzi.

-Sehemu ya Pili-

Sehemu hii inaangazia namna ambavyo sheria za madawa ya kulevya zilivyo undwa kiubaguzi dhidi ya Waamerika wenye asili ya Kiafrika. Hususan vita dhidi ya madawa ya kulevya vilivyo buni vishajiisho vya utekelezaji sheria ili kuwalenga watu wenye rangi, Waamerika wenye asili ya Kiafrika na Wahispania.

-Sehemu ya Tatu-

Sehemu hii inaangazia namna ambavyo ulinzi unaotangazwa na nidhamu ya kidemokrasia kiuhalisia haupo kwa ajili ya Waamerika wenye asili ya Kiafrika. Mfumo umewaweka watu katika daraja la pili kwa kuwapachika jina la uhalifu kwa kufanya iwe vigumu kwao kupata kazi na kuwatenga katika kupata kuishi katika majumba ya ummah na misaada ya chakula.

-Sehemu ya Nne-

Mukhtasari: Katika mazungumzo haya, tunaangazia Uislamu kama ndiyo njia pekee ya kufanikiwa kwa Waamerika wenye asili ya Kiafrika. Tunaangazia maisha ya Malcolm X na kuona namna ambavyo Uislamu ulimbadilisha, sio tu kwa maisha yake bali pia namna alivyo utazama Uislamu, tofauti na Amerika yenye ubaguzi wa rangi, kama mfumo wa maisha wenye mageuzi unaoweza kutatua tatizo la tofauti ya rangi.

-Sehemu ya Tano-

Mukhtasari: Katika silsila zilizo tangulia, tuliangazia namna Uislamu ndio njia pekee kwa Waamerika wenye asili ya Kiafrika. Tuliangalia dhulma za mfumo ulioko sasa na kuangazia namna Malcom X alivyo tambua kwamba Uislamu ndio suluhisho sahihi kwetu sote. Katika video hii, tunapata mukhtasari wa ruwaza ya Kiislamu inapo kuja kadhia ya uchumi na jinsi gani ni muhimu kuwa na nidhamu adilifu ya kiuchumi ili kuwepo na udugu katika mujtamaa. 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu