Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir: Kalima ya Ustadh Abdul Halim Zalloum kwa Anwani "Je, Kuna Urongo Mwengine Zaidi Baada ya Urongo Huu?!"

Kalima ya Ustadh Abdul Haleem Zalloum (Abu Al-Waleed) Mwanachama wa Hizb ut Tahrir kuhusu Urongo wa Wazi Kabisa unao zunguka kwa kunasibishwa na Jina Lake na Kun'ya yake katika Mitandao ya Kijamii

Jumanne, 22 Shaaban 1441 H sawia na 14 Aprili 2020 M

Je, Kuna Urongo Mwengine Zaidi Baada ya Urongo Huu?

(Imetafsiriwa)

Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu Mola wa walimwengu, na swala na salamu zimshukie bwana wa Mitume wote, mkweli na mwaminifu, aliye sema, kama ilivyo simuliwa na Bukhari kutoka kwa Mansur kutoka kwa Abu Wa'il kutoka kwa Abdullah, Mwenyezi Mungu awe radhi naye, kutoka kwa Mtume (saw) kwamba yeye (saw) amesema:  «إِنَّ الصِّدْقَ يَهْدِي إِلَى الْبِرِّ وَإِنَّ الْبِرَّ يَهْدِي إِلَى الْجَنَّةِ، وَإِنَّ الرَّجُلَ لَيَصْدُقُ حَتَّى يَكُونَ صِدِّيقاً، وَإِنَّ الْكَذِبَ يَهْدِي إِلَى الْفُجُورِ وَإِنَّ الْفُجُورَ يَهْدِي إِلَى النَّارِ، وَإِنَّ الرَّجُلَ لَيَكْذِبُ حَتَّى يُكْتَبَ عِنْدَ اللَّهِ كَذَّاباً» "Hakika ukweli unapelekea katika wema, na hakika wema unapelekea katika Pepo. Na hakika mtu hatawacha kusema ukweli mpaka atakuwa mkweli. Na urongo unapelekea katika uovu (Fujur), na uovu unapelekea katika Moto (wa Jahannam), na hakika mtu hatawacha kusema urongo mpaka atakuwa mrongo mbele ya Mwenyezi Mungu."

1- Hakika Abu Iyas, ambaye ameadhibiwa kwa uzembe kamili (Ihmaal Tamm) pamoja na adhabu hii jumla, ameendelea kueneza katika kurasa zake makala ya uzushi yanayo nasibishwa nami na jina langu; yote yaliyomo ndani yake si lolote ila ni urongo na uzushi. Ima katika kule kuyanasibisha nami au yaliyomo ndani yake. Pindi Abu Iyas alipo ulizwa Abdullah Abdullah ni nani, aliwaambia: "Yeye ni Abu Al-Waleed", na huu ni urongo na uzushi. Mnamo 10 Februari 2020 M nilitoa nakala ya sauti na video ambazo nilithibitisha ndani yake kuwa kila kitu kilicho chapishwa na Abdullah Abdullah, aliye chukua jina langu, ni urongo na uzushi.

2- Baada ya mimi kutoa nakala zilizo tangulia, Abu Iyas alichapisha makala katika ukurasa wake, yaliyo ambatanishwa waziwazi na jina langu na mmoja wa maswahiba zangu akawasiliana nami kuhusu uhalali wa makali haya, hivyo nilikana kujua kuyahusu, na nikasema kuwa mimi kamwe sikuchapisha makala hayo ya uzushi. Hivyo akenda akamzuru Abu Iyas, na kumwambia: "Nimemuuliza Abu Al-Waleed kuhusu makala ambayo umeyachapisha katika ukurasa wako kwa jina lake, na Abu Al-Waleed akaniambia hajui kuhusu makala haya na kwamba kamwe yeye hakuyachapisha." Lakini Abu Iyas akasisitiza kuwa makala haya kwa hakika yanatoka kwa Abu Al-Waleed, na kwamba yeye (Abu Iyas) anawasiliana na Abu Al-Waleed kila siku. Tambua kwamba kwa zaidi ya miaka saba sasa mimi sijawasiliana naye si kwa mdomo wala kwa maandishi. Je, kuna urongo mwengine zaidi baada ya urongo huu?

Kutokana na haya, makala yote haya yaliyo chapishwa na kutiwa saini kwa jina la Abdullah Abdullah au kwa jina la Abdul Halim Zalloum ni ya urongo na uzushi dhidi yangu, na mimi sina uhusiano nayo, sio kwa karibu wala kwa mbali, na yote yaliyomo ndani yake katika maalumati na mashambulizi kwa Hizb na uongozi wake na baadhi ya wanachama wake yote ni uzushi na yasio na ukweli. Na kwa hakika mimi namshtaki Abu Iyas kwa Mwenyezi Mungu pamoja na kundi lake na wale walio nyuma yake kwa Mwenyezi Mungu Al-Muntaqim Al-Jabbar (Mwenye nguvu Mlipaji kisasi). Na hata kama hatutaichukua haki yetu kutoka kwao hapa duniani, tutaichukua kutoka kwa Mwenyezi Mungu (swt) Siku ya Kiyama ambayo itawakusanya mahasimu kwake. 

إِنَّ اللَّهَ يُدَافِعُ عَنِ الَّذِينَ آمَنُوا إِنَّ اللَّهَ لَا يُحِبُّ كُلَّ خَوَّانٍ كَفُورٍ﴿

“Hakika Mwenyezi Mungu huwakinga walio amini. Hakika Mwenyezi Mungu hampendi kila khaini mwingi wa kukanya mema.” [Al-Hajj: 38]

21 Sha`ban 1441 H sawia na 14/4/2020 M

Ustadh Abdul Halim Zalloum (Abu Al-Waleed)

Mwanachama wa Hizb ut Tahrir

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumamosi, 01 Agosti 2020 12:43

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu