Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan ilitoa hotuba ya kisiasa mbele ya Klabu ya Al-Shabiba katika Soko Kuu la Port Sudan, mnamo siku ya Jumatatu tarehe 7 Jumada al-Akhirah 1446 H, sawia na 9/12/2024 M, yenye kichwa: “Haki ya Kisheia ya Waislamu katika dhahabu, petroli na rasilimali nyenginezo”, ambapo Ustadh Ahmed Abkar, wakili, mjumbe wa baraza la Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan alizungumza, ambapo ilifafanua mali ya umma kuwa ni vitu vilivyoainishwa na sheria kwa ajili ya jamii, vinavyoshirikiwa kati yao, na kukatazwa kumilikiwa na mtu binafsi peke yake.