Jumanne, 24 Shawwal 1446 | 2025/04/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Unafiki wa Kisiasa katika Demokrasia Kamwe Hautaisha Mpaka Tuubadilishe kwa Siasa za Kiislamu

Mnamo tarehe 06/01/2025, rufaa ya aliyekuwa Waziri Mkuu wa Malaysia, Datuk Seri Najib Tun Razak kuhusu kuwepo kwa amri ya nyongeza ya Mfalme, inayomruhusu kutumikia kifungo chake kilichosalia chini ya kifungo cha nyumbani, imekubaliwa na mahakama kwa wingi wa 2-1. Majaji wa Mahakama ya Rufaa kisha wakaamuru kesi hiyo irudishwe katika Mahakama Kuu ili ombi la Najib la uhakiki wa mahakama lisikizwe na jaji mpya. Amri hii ya nyongeza, ambayo ni sehemu ya mchakato wa msamaha wa kifalme, imekuwa jambo la kawaida, ambalo halijawahi kutokea katika asili yake. Sambamba na hilo, kulikuwa na jambo jengine - mkusanyiko mkubwa wa kuonyesha mshikamano uliokusanyika nje ya mahakama, ulioandaliwa na vyama ambavyo hapo awali vilikuwa wapinzani wa kisiasa wa Waziri Mkuu huyo wa zamani.

Soma zaidi...

Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki: Amali Kubwa “Usiisahau Gaza wala Usikubali Kusahauliwa Kwake!”

Kwa kuzingatia mauaji ya kikatili ya halaiki ambayo yamekuwa yakiendelea kwa zaidi ya miezi kumi na tano, yanayofanywa na umbile halifu la Kiyahudi dhidi ya Waislamu wasio na ulinzi katika Ukanda wa Gaza, ambayo yamesababisha kuuawa shahidi na kujeruhiwa kwa Waislamu zaidi ya 170,000, wanaume na wanawake hadi sasa, Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Uturuki iliandaa amali kubwa kote nchini Uturuki chini ya Kichwa: “Usiisahau Gaza wala Usikubali Kusahauliwa Kwake!”

Soma zaidi...

Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir: Amali za Kilimwengu za Hizb ut Tahrir katika Kumbukumbu ya Kuvunjwa kwa Khilafah 1446 H – 2025 M

Katika mwezi wa Rajab Mtukufu mwaka huu 1446 H - 2025 M, tunakumbuka kumbukumbu mbaya ya miaka 104 ya kuvunjwa kwa Dola ya Kiislamu na wahalifu wa Waarabu na Waturuki, ambayo ilianzishwa na Bwana wa Mitume, Muhammad, rehma na amani ziwe juu yake, na Maswahaba zake watukufu na waliobarikiwa, Mwenyezi Mungu awe radhi nao, na kuondolewa kwa mfumo wa utawala wa Kiislamu (Khilafah) mnamo tarehe 28 Rajab Tukufu katika mwaka wa 1342 H sawia na tarehe 3 Machi 1924 M mikononi mwa mhalifu Mustafa Kemal. Kutokana na hili, Hizb ut Tahrir inaandaa amali mbalimbali za umma katika nchi zote ambazo inaendesha shughuli zake za kuwahamasisha Waislamu kufanya kazi kwa bidii ili kusimamisha Dola ya Kiislamu, Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume.

Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia: Matembezi ya Ukombozi: “Mapinduzi Yanaendelea Kujikomboa kutokana na Ukoloni na Kusimamisha Khilafah kwa Njia ya Utume.”

Matembezi ya 66 yalianzia mbele ya Msikiti wa Al-Fath katika mji mkuu wa Tunis, baada ya swala ya Ijumaa, mnamo tarehe 10 Januari 2025 yalioandaliwa na Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Tunisia kuwanusurur watu wa Palestina na Al-Aqsa iliyo mateka, na kichwa chake kilikuwa “Mapinduzi Yanaendelea Kujikomboa kutokana na Ukoloni na Kusimamisha Khilafah kwa Njia ya Utume”

Soma zaidi...

Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Pakistan: Utekaji nyara wa Naveed Butt Unathibitisha kwamba Watawala wa Waislamu Wanazuia Kuhisabiwa Kwao!

Kesi 379 za upotezwaji wa lazima ziliwasilishwa kwa Tume ya Uchunguzi juu ya Kupotezwa kwa Kulazimishwa (COIOED) mnamo 2024. Watawala wa Waislamu huwateka nyara wale wanaowawajibisha, ni wakali kwa Waislamu na wana huruma na maadui. Hawakumnyonga jasusi na muuaji wa Kihindi Kulbhushan Yadav. Walimwachilia huru jasusi na muuaji wa Kimarekani Raymond Davis. Hata hivyo, walimteka nyara Naveed Butt, msemaji rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Pakistan, mnamo Mei 11, 2012. Naveed Butt alitoa wito wa ukombozi kutokana na ukoloni wa Marekani na kusimamishwa kwa Khilafah Rashida. Baada ya zaidi ya miaka kumi na mbili, watawala wangali hawajamwachilia huru. Ni lazima kwa umma na majeshi yake kuwang’oa madhalimu miongoni mwa watawala na kusimamisha Khilafah Rashida.

Soma zaidi...

Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia: Matembezi ya Ukombozi: “Na Saidianeni katika Wema na UchaMungu wala Msisaidiane katika Uovu na Uadui”

Matembezi ya 65 yalianzia mbele ya Msikiti wa Al-Fath katika mji mkuu wa Tunis, baada ya swala ya Ijumaa, mnamo tarehe 3 Januari 2025 yalioandaliwa na Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Tunisia kuwanusurur watu wa Palestina na Al-Aqsa iliyo mateka, na kichwa chake kilikuwa “Na Saidianeni katika Wema na UchaMungu wala Msisaidiane katika Uovu na Uadui!”

Soma zaidi...

Hizb ut Tahrir / Wilayah Pakistan Umma Mmoja... Khilafah Moja

Katika kumbukumbu ya mwaka wa 104 H wa kuanguka kwa Khilafah mnamo tarehe 28 Rajab 1342 H sawia na tarehe 3 Machi 1924 M, Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir inafuraha kuwasilisha kwa wafuasi na wageni wa tovuti za Afisi Kuu ya Habari, silsila mpya inayoitwa: “Ummah Mmoja... Khilafah Moja” iliyotolewa na Afisi ya Habari wa Hizb ut Tahrir ya Wilayah Pakistan.

Soma zaidi...

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu