Gazeti la Al-Raya: Vichwa Vikuu vya Toleo 508
- Imepeperushwa katika Al-Rayah
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Mnamo Jumapili, Agosti 11, 2024, mikutano ya Jeddah ilikamilika kati ya wajumbe kutoka serikali ya Sudan na Mjumbe Maalum wa Marekani nchini Sudan, Tom Periello, bila kufikia maelewano yoyote kuhusu ajenda ya mazungumzo na waangalizi. Baada ya kuregea kwa wajumbe wa mazungumzo, serikali ilitoa taarifa ikibainisha kushindwa kwa ujumbe wa Marekani kuwasukuma wanamgambo wa waasi kujitolea kutekeleza Azimio la Jeddah.
Kisimamo cha Usiku “Kuna tofauti gani kati ya mshirika na mwongo mdanganyifu?!”
Enyi Wanajeshi wa Pakistan! Kutochukua hatua kwenu kumewafanya Waislamu kuwa shabaha ya makafiri. Kutochukua hatua kwenu kunakaribisha ghadhabu ya Mwenyezi Mungu, ambayo hapana pa kuepukana nayo.
Tunamuomba Mwenyezi Mungu (swt) Amkubali Ismail Haniyeh katika Mashahidi, wala hatumtakasi mtu yeyote kwa Mwenyezi Mungu, na yeye siye shahidi wa kwanza katika vita hivi wala hatakuwa wa mwisho.
Mnamo asubuhi ya tarehe 31 Julai 2024, umbile la Kiyahudi lilimuua shahidi kiongozi wa Hamas Ismail Haniyeh katika shambulizi la kombora jijini Tehran, mji mkuu wa Iran. Siku moja kabla, umbile hilo la Kiyahudi lilimuua shahidi kamanda wa Hezbollah kwa kushambulia jengo la makaazi jijini Beirut, Lebanon. Hapo awali, umbile la Kiyahudi lilishambulia vituo mbalimbali katika bandari ya Hodeida nchini Yemen kwa ndege za kivita. Hii ni huku Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina ikiwa imegeuzwa kuwa magofu katika kipindi cha miezi kumi iliyopita.
Sudan Tribune iliripoti jana, Jumamosi, Julai 27, 2024, ikinukuu taarifa iliyotolewa na Kamati ya Maandalizi ya Umoja wa Madaktari wa Sudan, iliyosema: “Kamati ya Maandalizi ya Umoja wa Madaktari ilisema katika taarifa iliyopokelewa na Sudan Tribune kwamba watu waliokimbia makaazi yao mjini Kassala wanaishi kwenye mahema yaliyochakaa na kuzungukwa na maji kila upande, na watoto wao wanalia kwa njaa. Iliongeza kuwa hali imekuwa mbaya zaidi, kwani watoto wawili walikufa kwa shoti ya umeme, na kuna vifo kutokana na kuumwa na nyoka na kesi zingine zisizojulikana.”