Afisi ya Habari
Wilayah Yemen
H. 23 Rajab 1445 | Na: 1445 / 20 |
M. Jumapili, 04 Februari 2024 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
China Haijatia Madoa Mikono yake kwa Damu ya Waislamu huko Palestina,
Lakini Imejaa Madoa na Damu ya Waislamu wa Uighur
(Imetafsiriwa)
Gazeti la Al-Thawra, lililotolewa jijini Sanaa mnamo Jumanne, Januari 29, 2024, lilikuwa na kichwa cha habari kutoka kwenye jukwaa "China huko Arabia: Meli za China zakwepa haki ya Yemen kwa sababu China haikutia madoa mikono yake kwa damu ya Wapalestina na haikushiriki katika uharibifu uliotokea kwa Yemen." Gazeti hilo lilisema, "Tafsiri ya Amerika ya Magharibi inachukuliwa kuwa mbaya na ya kupotosha katika ukweli wa kijiografia. Ukweli ni tofauti kabisa. Meli za China zilikwepa haki ya Yemen haswa kwa sababu China haijatia madoa mikono yake kwa damu ya mauaji ya halaiki ya Wapalestina na haijafanya uharibifu nchini Yemen!"
Ghafla na bila ya utangulizi, China ilificha vitendo vyake vya kutisha dhidi ya Waislamu, ikianza na ushirikiano wake na Urusi katika mauaji ya mtawala wa Turkestan, baada ya kuanguka kwa Khilafah, na kuruhusu kugawanya Turkestan ya Mashariki yenye utajiri wa mafuta kati yao, huku Urusi ikichukua Turkestan Magharibi (Jamhuri za Asia ya Kati) baada ya kuporomoka kwa Khilafah Uthmaniya!
Turkestan Mashariki ni nchi ya Waislamu wa Uighur, ambao misikiti yao China imeibomoa kwa zaidi ya thuluthi mbili. China imewakandamiza, kuwazuia kutekeleza ibada za Kiislamu kwa karibu karne moja, yenye lengo la kufuta kitambulisho chao, kuwatenganisha watoto na baba zao katika "vituo vya malezi na ukarabati," na kuwalazimisha wanawake kuwakubali wanaume wa Kichina wa Han majumbani mwao kama sehemu ya Mradi wa "Kuwa Familia"! Waliwadhalilisha katika miaka ya 2019-2022, wakitumia visingizio mbali mbali, wakiukashifu Uislamu kwa kisingizio cha kupambana na "ugaidi," na wakaunda Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai na Urusi mnamo 1995. Je, Beijing imesahau haya yote ili kujifanya kwa ulimwengu kwamba mikono yake haijatiwa madoa na damu ya Wapalestina?
Mtume Muhammad (saw) amesema: «الْمُسْلِمُونَ تَتَكَافَأُ دِمَاؤُهُمْ...» “Damu ya Waislamu wote ni sawa”. Damu inayotiririka Turkestan Mashariki ni sawa na damu inayotiririka katika nchi iliyobarikiwa ya Palestina. Je, ni lipi umbile la mahusiano ya kidiplomasia ambayo serikali ya Beijing inaanzisha na umbile nyakuzi la Kiyahudi nchini Palestina, na kisha wanaonesha huruma kwa watu wa Palestina?
Tunawaambia wale wanaotazama matukio na vitendo kijuujuu kwamba wachunguze kwa undani zaidi na kuangaza fikra zao. Wanapaswa kuangalia matukio kwa mtazamo wa itikadi ya Kiislamu, si kwa mtazamo wa matumizi, utaifa, au ukabila - yote haya ni ujinga wa kifisadi. Mtazamo sahihi kwa Waislamu ni kuchunguza vitendo vya China dhidi ya Waislamu kwa ujumla wake, na sio tu dhidi ya watu wetu wa Palestina. Je, mtu anayedai kufuata njia ya Quran anawezaje kuyatazama matukio vyenginevyo?
Uislamu, kama kanuni, ni kanuni ya kisiasa, na Aqida yake ni Aqida ya kisiasa, na Sharia yake ni ya kisiasa, kwani inatawala mambo ya binadamu kama mtu binafsi katika jamii. Inafafanua mtazamo wake katika maisha, viwango vyake, imani, na maadili ya juu zaidi. Inasimamia tabia yake kulingana na Aqida yake. Uislamu unahitaji dola kuutabikisha. Hata hivyo, tangu kukosekana kwa Dola hii, Umma wa Kiislamu umepotea miongoni mwa mataifa bila mlinzi. Kwa hiyo, kufanya kazi ya kuiregesha dola ya Kiislamu, Khilafah, ambayo iliondolewa na Wamagharibi makafiri katika mwezi kama huu, tarehe 28 Rajab, ni faradhi kubwa. Hizb ut Tahrir imejitolea kusimamisha faradhi hii ili Umma uweze kutekeleza tena nafasi yake katika kuwaongoza wanadamu kwa njia inayomridhisha Mwenyezi Mungu Mtukufu, chini ya uongozi wa Khilafah Rashida ya pili, kwa njia ya Utume. Ni alfajiri ambayo hakuna yeyote kutoka katika viumbe anayeweza kuzuia kuja kwake. Yeye (saw) amesema: «ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةً عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ» “Kisha itakuwepo Khilafah kwa njia ya Utume.”
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Yemen
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Yemen |
Address & Website Tel: 735417068 http://www.domainnomeaning.com |
E-Mail: yetahrir@gmail.com |