Afisi ya Habari
Wilayah Yemen
H. 25 Dhu al-Qi'dah 1444 | Na: HTY- 1444 / 26 |
M. Jumatano, 14 Juni 2023 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kama Matokeo ya Kutekeleza Kanuni ya Kisekula ya Kibepari, Makampuni ya Hisa Yanaiba Pesa za Wanachi wa Kawaida wa Yemen
(Imetafsiriwa)
Mnamo siku ya Jumatano, tarehe 18 Dhu al-Qa`adah 1444 H sawia na 07 Juni 2023, Mahakama ya Fedha za Umma katika Manispaa ya Mji mkuu ilitoa uamuzi wake katika kesi ya kile kinachojulikana kama Kampuni ya Sultana Palace, ambapo iliwatuhumu watu 82 kwa kuwalaghai watu 110,000 katika kipindi cha kati ya Januari 2016 na Julai 15, 2020 na tarehe ya baadaye, kupitia hilo, walipata makadirio ya riyal 66,314,405,000. Mahakama iliamua kutaifisha mali zinazohamishika na zisizo hamishika zilizonaswa kusubiri kesi hiyo. Mwendesha Mashtaka wa Fedha za Umma aliwaonya watu dhidi ya kuamiliana na mashirika kwa jina la makampuni haramu, na yasiyotambulika ya hisa, na kutoingizwa ndani yake, kuamiliana nayo na miradi yao feki ambayo wanaikuza ambayo kwayo inalenga kuwatapeli na kuwapora fedha na akiba zao kwa dhulma. (Shirika la Habari la Saba).
Hivi ndivyo mateso yanavyoendelea kutokana na kuondolewa kwa utawala wa Kiislamu kwa kupinduliwa dola yake na wasaliti wa Kiarabu, na Kituruki, na kupanga njama za Magharibi Kafiri, ambapo mfumo wa kibepari wa kisekula ulitawala ulimwengu, na watu walionja janga la migogoro mfululizo. Kanuni hii sio tu ilipora mali ya watu na kuwafanya watumwa, lakini pia ilichukua pesa zao na akiba kwa kuwaburuza katika kununua hisa za kampuni za hisa ili kuwaahidi mgao wa faida. Makampuni haya yanafanya kazi ya kuchukua pesa za watu kwa ulaghai, na yamepewa leseni ya kufanya shughuli zao na serikali, kwa sababu hayatawaliwi na Sharia ya Mwenyezi Mungu, bali na mfumo wa kibepari ulioleta katika nchi zetu za Kiislamu aina za makampuni ya Kimagharibi ambayo ni ngeni kwa thaqafa yetu ya Kiislamu na urithi wetu wa Sharia.
Ile inayoitwa Kampuni ya Sultana Palace imejinufaisha na hitaji la watu la kutafuta chanzo cha mapato, kwani vita na mzozo vilisababisha maelfu ya watu kupoteza kazi zao au kupata kazi kwa mapato duni, na kuwalazimu watu wengi kuuza mali zao na akiba ili kujikimu mahitaji yao ya maisha. Wazo la kampuni lilitegemea faida ya haraka na ya uhakika ya wale ambao iliwaita wenye hisa kwa kuwadanganya kuwa kampuni inafanya kazi katika miradi mingi ya uwekezaji ndani na nje ya nchi, ikipitisha asilimia maalum kwa wenye hisa, na iliahidi wenye hisa mapato ya juu ya hadi 100% katika baadhi ya hali, na kuwapa vyeti na nyaraka zinazothibitisha upatikanaji wao wa hisa. Kampuni hiyo ilikuwa ikitangaza hisa hizi kupitia mitandao ya kijamii na matangazo ya kulipia, na ilifanya kazi kati ya watu kupitia wawakilishi wake kwa zaidi ya miaka minne, na kuweka pesa zake za ajabu kwenye benki na makampuni ya kubadilisha fedha mbele ya macho ya asasi za serikali ambazo hazikunyosha hata kidole kimoja hadi baadhi ya wenye hisa wakaudhika na kuchelewa kupokea faida zao mwezi Julai. 2017, na asasi husika kuhama baada ya utajiri wa kampuni kufikia makumi ya mabilioni. Na hii sio kampuni pekee inayofanya kazi kwa njia hii, kwani kampuni zengine zilionekana, kama vile Tihama Flavour na Kampuni ya Asali ya Al Hani na zote hizo zilisababisha wenye hisa kupoteza pesa zao nyingi, na kupunguza uwezo wao wa kutumia na kuweka akiba.
Kutokana na ukweli kwamba sisi ni chama cha kisiasa ambacho mfumo wake ni Uislamu, tunapaswa kuufafanua uhalisia wa makampuni haya na hukmu juu ya kuamiliana nayo:
Kampuni hizi za hisa ni zao la kanuni ya kibepari inayotenganisha dini na maisha. Baadhi ya watu hawajui uhalisia wake kwa sababu ya uhadaifu unaofanywa na serikali kupitia zana zake mbalimbali na ukweli kwamba makampuni haya yanafanya kazi ndani ya nchi za Kiislamu kwa leseni na ufadhili kutoka kwa nchi zilizopo Qatar leo. Nchini Yemen, Sheria Na. 22 ya 1997 kuhusu makampuni ya kibiashara na marekebisho yake yaliyotajwa katika Kifungu cha 9 makampuni halali, ikiwemo makampuni ya hisa.
- Aina hii ya kampuni iliibuka ili kuwawezesha wamiliki wa fedha kudhibiti fedha za umma na kulinda mali zao kutokana na wadai na wenye haki wengine katika biashara zao endapo baadhi yao yatafeli. Wenye haki ndani yake hawana madai yoyote kwa wenye hisa kwa chochote, na hawana chochote isipokuwa kile kinachobaki katika mali ya kampuni baada ya kufilisika kwake.
- Kampuni za kibepari ni kampuni za maumbo na aina nyingi, lakini licha ya wingi wao, ziko chini ya aina mbili za kampuni:
Makampuni ya mitaji: kwa mfano, makampuni ya hisa, makampuni ya ushirika yaliyofungwa kwa hisa, na makampuni ya ushirika wa watu; pia, makampuni ya ushirika na makampuni ya ya ushirika ya kawaida.
- Kampuni hizi za hisa ni miongoni mwa kampuni zisizokubalika kwa mujibu wa Sharia na miongoni mwa shughuli ambazo Muislamu haruhusiwi kuzifanya.
1- Ushirika katika Uislamu ni mkataba baina ya watu wawili au zaidi wanaokubaliana juu ya biashara ya fedha kwa nia ya kupata faida, hivyo idhini ya ushirika ni lazima ipatikane kutoka pande zote mbili. Katika makampuni ya hisa, hili halifanyiki, washirika hawajuani, na hakuna kuridhika na kukubaliana kati yao. Mkataba katika kampuni lazima uelekezwe katika kufanya kazi za kifedha kwa nia ya kupata faida, kwa hivyo, haifai kuzingatia kulipa pesa tu, lakini kufanya kazi za kifedha ndio msingi, na hili halifanyiki katika makampuni ya hisa.
2- Kampuni ni mkataba wa utumizi wa pesa na kukuuza pesa kupitia uendelezaji wa mali, na ukuzaji wa pesa ni moja ya utumiaji halali. Katika makampuni ya hisa, washirika hawana haki ya matumizi, hivyo mtu hawezi kuchukua pesa zake kutoka kwa kampuni (thamani ya hisa), na hawezi kumzuia mtu yeyote asiyetakiwa kununua hisa za kampuni, kwani kampuni inachukuliwa kuwa mtu kisheria na hili ni batili.
3- Kampuni ya hisa ni ya kudumu na hii ni kinyume na Sharia. Kampuni ni mojawapo ya mikataba inayoruhusiwa kisheria, na hubatilika kwa kifo cha mshirika mmoja, uwendawazimu wake, au kuzuiwa kwake, au kwa kuvunjwa na upande wa mmoja wa washirika. Kuwa ni ya kudumu kunaifanya kuwa kampuni ya kimakosa.
Taarifa hii ni kwa ajili yenu kutambua kuwa nchi hizi zilizopo hazitabikishi Uislamu, bali sheria zao zinatokana na katiba ya Ufaransa, na kwamba kuondoa dhulma iliyowapata watu kwa kuchukua fedha zao kinyume cha sheria sio kwa kuyashtaki makampuni ya ushirika yasio na leseni, bali ni kwa kuung'oa mizizi wa mfumo wa kibepari kutoka katika mizizi yake kwa sababu ni kanuni potofu inayozalisha migogoro, na hata mabwana zake Marekani na Ulaya hawakuepushwa nayo, na juu ya hili ni kwamba, utekelezaji wake ni dhambi hapa duniani na adhabu kali kesho Akhera. Inashangaza jinsi gani wakati Muislamu ambaye ana mtazamo mpana na mkamilifu wa kiungu wa maisha anabadilisha kile kilicho duni kwa kilicho bora zaidi! Ameipoteza dunia hii na Akhera.
Jambo la kusikitisha ni ukimbiliaji wa watu kuwa sehemu ya makampuni haya, kuyachangia, na hata kuyaanzisha bila ya kutafiti au kuchunguza umbile lao ili kuona kiasi cha makubaliano yake au ukiukaji wake wa hukmu za Sharia, kwa kuzingatia uwepo wa wasomi wa mahakama karibu na watawala vibaraka ambao hawaongoi watu kwenye njia ya haki na wema, lakini badala yake wanapigana na kila mtu mkweli na mwaminifu. Na wanafanya kazi ya kuufanya ummah kuwa wajinga kupitia mielekeo iliyo dhidi ya Sharia inayomfanya mtafutaji elimu kusema maneno yake na kuwaongoza kwa uwongofu wao ili kuwaweka mbali na Waislamu kuifahamu dini yao ipasavyo. Ijapokuwa ruhusa na upigiaji debe wa makampuni haya ni mapana kiasi gani, vishawishi vya faida zao ni vikubwa, na uwepo wao umeenea katika nchi yetu, hii haiwaondoi Waislamu katika faradhi ya kuijua Sharia inayowatawala na kuamiliana nao. Ni njia ya kukuza pesa, ndio, lakini ni njia iliyo kinyume na Sharia, na faida yake, hata ikiwa ina dhamana, ni haram. Je, kuna tatizo gani kwa Waislamu wanaofumbia macho mambo haya na kujishughulisha na mikataba hii batili, je, ni tamaa ya dunia na mapambo yake, au kutojua hukmu za Sharia ya kweli, au kpuuza makatazo ya Mwenyezi Mungu?!
Wallahi inahuzunisha nafsi kuona taasisi hizi za kibepari zikidhibiti masoko ya biashara na fedha katika nchi za Kiislamu katika mfumo wa makampuni ya uwekezaji, benki na vyama vya ushirika. Taasisi zote hizi ni kampuni za hisa ambazo kiasili sio kampuni, na bado Waislamu wanashughulika nazo kwa ujinga na kwa kutojua hukmu zao, na kwamba hakuna udhuru kwa wajinga katika kujua hukmu za Sharia. Kwa sababu kanuni ya msingi katika matendo ya Muislamu ni kushikamana na hukmu ya Sharia, na hili linahitaji kuzijua hukmu za vitendo kabla ya kuvitekeleza. Hivi ndivyo alivyotuwajibisha Muumba na Al-Muddabir (Msimamizi wa wote), na Mtume Mtukufu (saw) akatufafanulia na maswahaba watukufu wakatufundisha.
Enyi Watu wetu wa Yemen, Enyi Watu Wenye Nguvu na Ustahimilivu, Enyi Watu wa Nusra: Tunawalingania nyinyi kuupindua mfumo huu wa kisekula wa kibepari ambao Marekani inauongoza, na mfanye kazi ya kusimamisha dola ya Kiislamu, Khilafah inayowaunganisha Waislamu na kutabikisha mfumo mtukufu wa Uislamu mahali pake ili kujiokoa sisi wenyewe na wanadamu wote kutokana na janga la ubepari mlafi. Sisi katika Hizb ut Tahrir tunafanya kazi baina yenu na pamoja nanyi, na tumetayarisha mwelekeo mpana na kamili, ikiwemo mfumo wa kiuchumi, na hii hapa ni link ya kitabu:
Kiarabu: https://www.domainnomeaning.com/ar/index.php/resources/hizb-resources/48.html
Kiingereza: https://www.domainnomeaning.com/en/index.php/literature/hizb-resources/1737.html
Magharibi inafanya inajikusanya dhidi ya Umma wa Kiislamu na kueneza sumu yake kwa msaada wa vibaraka katika ardhi za Kiislamu, hivyo ni lazima kwa waumini wenye ikhlasi kusimama kuinusuru dini hii kwa kuitekeleza kwa upana na ukamilifu. Matokeo ya mwisho ni kwa Waumini, na hii ni Sunnah ya Mwenyezi Mungu katika ardhi yake, na sisi katika Hizb ut Tahrir tunakualikeni kufanya kazi nasi ili kusimamisha dola ya Uislamu unaotekelezwa ndani ya Dola hiyo na kubeba ujumbe wa uongofu na nuru kwa ulimwengu.
[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا للهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللهَ يَحُولُ بَيْنَ الْمَرْءِ وَقَلْبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ]
“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye tu mtakusanywa.” [Al-Anfal 8:24]
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Yemen
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Yemen |
Address & Website Tel: |
E-Mail: yetahrir@gmail.com |