Afisi ya Habari
Wilayah Yemen
H. 28 Rajab 1444 | Na: HTY- 1444 / 13 |
M. Jumapili, 19 Februari 2023 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Katika Kumbukumbu ya Kuvunjwa Khilafah, Yemen na Nchi Zote za Kiislamu zimo katika Misiba. Kumbukumbu Hii na iwe ni Kichocheo cha Hatua ya Kuisimamisha
(Imetafsiriwa)
Katika siku hii, tarehe ishirini na nane ya mwezi wa Rajab al-Khair katika mwaka wa 1342 H, sawia na tarehe tatu ya mwezi Machi mwaka wa 1924 M, uhalifu mkubwa zaidi dhidi ya Waislamu ulifanyika, wakati Magharibi kafiri, ikiongozwa na Uingereza, iliweza kuivunja dola ya Kiislamu. Majeshi ya Waingereza waliokuwa wakiikalia kwa mabavu hawakutoka nje kwenda kwenye Mlango-Bahari wa Bosphorus na Istanbul, mji mkuu, isipokuwa baada ya kuhakikishiwa mafanikio ya kibaraka wake, Mustafa Kamal, kwa kuiondoa Khilafah, kuanzisha jamhuri ya kisekula kwenye magofu yake, na kumfukuza khalifa kutoka nchini. Hapana shaka kwamba tukio hili kubwa linachukuliwa kuwa ni nukta hatari ya mabadiliko katika maisha ya Umma wa Kiislamu, kwani Waislamu kabla ya hapo waliishi kwenye kivuli cha makaazi ya Uislamu. Yeyote ambaye hakuishi katika kivuli cha Dola ya Kiislamu angeweza kuhamia huko ili kuishi kama mmoja wa raia wake, kufurahia maisha ya Kiislamu, na kuondolewa wajibu shingoni mwake wa kuweka kiapo cha utiifu kwa Khalifah, kwa kufuata kauli yake (saw):
«وَمَنْ مَاتَ وَلَيْسَ فِي عُنُقِهِ بَيْعَةٌ مَاتَ مِيتَةً جَاهِلِيَّةً»
“Na atakaye kufa akiwa hana shingoni mwake kiapo cha utiifu (bay’ah), basi atakufa kifo cha Jahiliya (siku za ujahiliya).” Hata hivyo, baada ya kuvunjwa dola na kuondolewa Khilafah, hakuna Muislamu yeyote aliyeweza kushikamana na wajibu wa kuishi katika nyumba ya Uislamu. Kwa hiyo, tukio hili la huzuni lilistahiki kutafakariwa kutokana na hatari yake kwa mustakbali wa Umma wa Kiislamu. Kutokana na hayo, kumbukumbu ya kuvunjwa Khilafah ilikuwa tofauti na ya kipekee na si kama kumbukumbu zote. Sio kumbukumbu chungu tu, bali ni msukumo wa ulazima wa kufanya kazi ya kuiregesha ili kutabikisha sheria ya Mwenyezi Mungu juu ya watu, na hiyo ni katika muktadha wa “chochote kinachopelekea kwenye wajibu hicho chenyewe pia ni wajibu”. Wala sio kumbukumbu ya kusherehekea kama kumbukumbu zengine za kawaida, bali ni ufufuo wa maana za kumbukumbu hii - hata kama sio maarufu miongoni mwa Waislamu wengi - na ulinganizi wake unaibua ndani ya Waislamu kishajiisho cha hatua sahihi ya kisiasa, na dhamira kwa ajili ya umoja wa kisiasa wa haraka wa Umma wa Kiislamu. Kwa kurudi kwa Khilafah, Dini inahifadhiwa na kulindwa, na kupitia kwayo Uislamu unalindwa, na matukufu na ardhi zote za Kiislamu zinazokaliwa kwa mabavu hukombolewa, washambuliaji hunyamazishwa, Huduud (adhabu) husimamishwa, matukufu hayatakiukwa, heshim huhifadhiwa, hivyo basi nasaba huhifadhiwa kutokana na kuchanganyika, na mipaka huimarishwa kutokana na mashambulizi.
Tangu kuvunjwa Khilafah miaka mia moja na mbili Hijria iliyopita, Waislamu hawajaonja ladha ya ushindi, izza, na hadhi hata mara moja. Hawajawahi kushinda mapigano, na hawajawahi kushinda vita. Vita vyao baada ya zama za Khilafah havikusababisha chochote ila kushindwa, vikwazo, na balaa. Ama amani yao, wanayoiitisha na kuikuza, haikuwa chochote ila kujisalimisha kikweli kwa mgeni, na ilisababisha tu kuvunjwa moyo, mangati na udanganyifu. Kwa hiyo, ilikuwa ni lazima kwa kila Muislamu, bila ya kujali uanachama wake, na kwa chama chochote ambacho utiifu wake uko, kwa kumbukumbu hii kumzuia kutafakari upya hesabu zake, afikiri kwa makini na kisha ashiriki na kile anacho miliki katika nguvu ili kufanya uregeshaji wa dola ya Khilafah iwe ndio hamu yake ya kwanza, kuondoa dhambi shingoni mwake la kukosekana faradhi hii kubwa, na kujiunga na wanaofanya kazi kwa mgao wa fadhila hii kubwa, ambayo, Mwenyezi Mungu akipenda, itawaenea wanadamu kwa mwanga na nuru yake. Fikra ya Khilafah ambayo Hizb ut Tahrir inaifanyia kazi kuisimamisha imekuwa hitajio la umma linalolazimu mwamko wa Kiislamu na wimbi la kisiasa la Kiislamu ambalo limeenea na kusambaa katika nchi za Kiislamu katika siku za hivi karibuni, kiasi kwamba Magharibi inaogopa kurudi kwake, kutimiza bishara njema ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw):
«ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةً عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ»
“Kisha itakuwepo Khilafah kwa njia ya Utume.”
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Yemen
Fuatilia na Usambaze Alama Ishara za Kampeni:
#Time4Khilafah |
#EstablishKhilafah |
#ReturnTheKhilafah |
#TurudisheniKhilafah |
#KhilafahBringsRealChange |
#بالخلافة_يحصل_التغيير_الحقيقي |
أقيموا_الخلافة# |
كيف_تقام_الخلافة# |
#YenidenHilafet |
#HakikiDeğişimHilafetle |
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Yemen |
Address & Website Tel: 735417068 http://www.domainnomeaning.com |
E-Mail: yetahrir@gmail.com |