Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Yemen

H.  8 Rajab 1442 Na: HTY- 1442 / 25
M.  Jumamosi, 20 Februari 2021

Taarifa Kwa Vyombo vya Habari

Sifa ya Kuwa Taifa Bora la Umma wa Kiislamu Lazima Ifungamanishwe na Kusimamishwa Khilafah

(Imetafsiriwa)

Allah Azza Wa Jal asema:

(كُنتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ تَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَتَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ)

“Nyinyi mmekuwa bora ya umma walio tolewa watu, kwa kuwa mnaamrisha mema na mnakataza maovu.” [Al-i-Imran: 110].

Umma wa Kiislamu uliendelea na ufahamu wa aya hii na umeitekeleza kwa karne nyingi, mpaka Khilafah ilipovunjwa. Ilikuwa ni lazima kwa Umma bora kutii amri ya Mwenyezi Mungu (swt) katika aya hii kwa kupitia kuamrisha wema na kufanya kazi kutabikisha utawala wa Uislamu kupitia kusimamisha Khilafah na ulinganizi kwa Uislamu; na kwamba lazima uregeshe tena mamlaka yake na kumteua khalifa juu yake, ashughulike na mambo yake na Uislamu, aulinde, na aondolee matatizo yake. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alisema:

«كَانَتْ بَنُو إِسْرَائِيلَ تَسُوسُهُمْ الْأَنْبِيَاءُ، كُلَّمَا هَلَكَ نَبِيٌّ خَلَفَهُ نَبِيٌّ، وَإِنَّهُ لَا نَبِيَّ بَعْدِي، وَسَيَكُونُ خُلَفَاءُ فَيَكْثُرُونَ»، قَالُوا: فَمَا تَأْمُرُنَا؟ قَالَ: «فُوا بِبَيْعَةِ الْأَوَّلِ فَالْأَوَّلِ، أَعْطُوهُمْ حَقَّهُمْ، فَإِنَّ اللَّهَ سَائِلُهُمْ عَمَّا اسْتَرْعَاهُمْ»

“Wana wa Israel wanasiasa wao walikuwa ni mitume wao: kila mtume mmoja alipokufa, alikuja mtume mwengine. Na hakika yake hakutakuwa na mtume mwengine baada yangu, lakini kutakuwepo na makhalifa wengi." Watu wakauliza, "Je, watuamrisha (tufanye) nini Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu?" akasema, "Mpeni bay'ah mmoja baada mmoja, wapeni haki zao, kwani hakika Mwenyezi Mungu atawauliza juu ya wale waliopewa uchungaji juu yao.” [Imepokewa kwa itifaki].

Na kubeba ulinganizi kwa wale ambao Uislamu bado haujawafikia; kuwatoa kizani kuwaingiza kwenye nuru, haswa kwa kuwa nchi za makafiri za Magharibi, ambazo ziliivunja dola yao, kuondoa utawala wa Uislamu kutoka kwa Waislamu, na kuteua ruwaibidha (watawala wajinga) juu yao, ambao walitekeleza nidhamu za kikafiri juu yao. .

Hizb ut Tahrir iliasisiwa ili kuuamsha Umma wa Kiislamu kwa kuitikia amri ya Mwenyezi Mungu (swt) aliye sema:

(وَلْتَكُن مِّنكُمْ أُمَّةٌ يَدْعُونَ إِلَى الْخَيْرِ وَيَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ وَأُولَٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ)

“Na uwe kutokana na nyinyi umma unao lingania kheri na unao amrisha mema na unakataza maovu. Na hao ndio walio fanikiwa.” [Al-i-Imran: 104]. Mtume (saw) amesema:

«ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةٌ عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ» “Kisha itakuwepo Khilafah kwa njia ya Utume.”

Maimamu wameafikiana kwamba uongozi ni wajibu, kama vile al-Juwaini, Ibn Hazm, al-Mawardi, Ibn Hajar al-Asqalani, al-Haythami, Ibn Khaldun, al-Nasfi, al-Ghaznawi, al-Qurtubi, Ibn Taymiyyah, al-Shawkani, Ibn Ashur na al-Jaziri, na kwamba Waislamu lazima wawe na imamu ambaye anadumisha ibada za Dini, na kwa msingi kwamba Umma una mchungaji wa kuutunza.

Je! Sio wakati sasa wa wanachuoni wa Umma wa Kiislamu nchini Yemen katika siku hii na zama hizi, baada ya karne moja kamili ya Hijria kupita tangu kuvunjwa kwa Khilafah, kunyanyuka pamoja na Hizb ut Tahrir ili kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, kwa kuitikia amri ya Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume wake (saw), na kwa kuwafuata wanachuoni waliowatangulia?! Na kwamba vijana wa Yemen na wazee wao, wanaume na wanawake, wajiunge nao ili kusimamisha dola ya haki, serikali ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, na ili dola hii irudi katika njia iliyoanzia mjini Madina?! Waislamu na ulimwengu wana hamu ya kuiona bendera ya al-Uqab imeinuliwa juu na mikono ya mwanachuoni mkubwa Ata bin Khalil Abu Al-Rashtah kama ilivyokuwa hapo awali.

Ni nani mwengine ikiwa sio nyinyi atakayeisimamisha, Enyi Waislamu?!

Hii ndio kadhia yetu nyeti na ni wajib juu ya kila Muislamu mwanamume na mwanamke. Mtume (saw) amesema:

«وَمَنْ مَاتَ وَلَيْسَ فِي عُنُقِهِ بَيْعَةٌ مَاتَ مِيتَةً جَاهِلِيَّةً» “Yeyote anayekufa na hana ahadi ya utiifu (bay'ah) katika shingo yake amekufa cha Kijahiliya.”

Leo barakoa zimepomoka kutoka kwa vibaraka, nchi za Kiislamu zilipotezwa na kukiukwa, na makabiliano yakawa moja kwa moja kati ya Umma wa Kiislamu na makafiri, na sasa tunashuhudia kuyumba kwa mfumo wao na kufeli kwake kukabiliana na Uislamu, na sasa ni zamu yenu, Enyi Waislamu, kuufanya Uislamu kuwa mfumo mpya wa kiulimwengu unaosubiriwa na ulimwengu. Hivyo basi, isimamisheni enyi Waislamu baada ya kuitambua.

أقيموا_الخلافة#
#ReturnTheKhilafah
#YenidenHilafet
خلافت_کو_قائم_کرو#

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Yemen

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Yemen
Address & Website
Tel: 
E-Mail: yetahrir@gmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu