Afisi ya Habari
Wilayah Yemen
H. 8 Jumada I 1442 | Na: HTY- 1442 / 13 |
M. Jumatano, 23 Disemba 2020 |
Taarifa Kwa Vyombo vya Habari
Serikali Mpya ya Moein Abdel-Malek Haitawapa Watu wa Yemen Chochote Wala Kuakhirisha Chochote
(Imetafsiriwa)
Siku ya Ijumaa, 12/18/2020, ilitangazwa kuwa serikali itaundwa chini ya uongozi wa Moein Abdel-Malek, yenye mifuko 24, iliyogawanyika kwa usawa kati ya Kaskazini na Kusini. Mifuko mitano, miongoni mwao fungu la mpito.
Uundaji huu wa serikali unajiri baada ya Abd Rabbu Hadi kutoa uamuzi wa kuiunda kutoka Riyadh. Mipango inafanywa ya kurudi kwa serikali jijini Aden, na maagizo ya mawaziri kula viapo na kukubali uteuzi wao mbele yake, ili kuanza kazi yao mara moja kuanzia nukta hiyo, kwa kujibu ombi la vyama vingine lenye kutaka kurudi kwa Abd Rabbo na serikali iliyoundwa hadi Aden, badala ya kuishi jijini Riyadh.
Uundaji wa serikali ulitangazwa huko Riyadh, na kwa hiyo dolari, ambayo ilizidi 900, ilipungua hadi 760 riyals. Na ikawa wazi kuwa Riyadh ilikuwa ikijitahidi kuunda serikali hiyo, na ilikuwa imesisitiza kumteua Abdul-Malik kama mkuu wa serikali iliyoundwa. Balozi wa Riyadh nchini Yemen, Muhammad Al Jaber, alitangaza wiki moja kabla ya serikali kutangaza kukamilisha mipango ya kijeshi inayohusiana na makubaliano ya Riyadh, na kuondolewa kwa Hadi na vikosi vya mpito kutoka pande za mapigano huko Abyan, kama ombi la Waziri wa Ulinzi wa Riyadh Khalid bin Salman katika mkutano wake wa mwisho na Abd Rabbu Hadi mnamo 26/11/2020 M kutangaza kuunda serikali. Na pia iliibuka kutoka kwa taarifa ya Mu'in Abdul Malik, akisema, "Tuna hakika kwamba serikali mpya itaunga mkono na kushiriki katika nguvu za kisiasa na kijamii, na kuwaunga mkono ndugu katika muungano huo ili kusaidia uhalali unaoongozwa na Ufalme wa Saudi Arabia ...".
Uundaji wa mawaziri wa Baraza Kuu la Jumuiya ya Harakati ya Mapinduzi ya Kusini, mrengo wa Ba'um, haukuwepo.
Kwa wale ambao walipigana jana na Hadi na Mpito: Damu yenu ilikwenda wapi?! Damu yaenu ni ya bei rahisi kwao na haina utakatifu, na msifikirie kuwa wameacha mapigano, wakihakikisha kutomwagika kwa damu yenu! Na kusitisha vita sio kwa ajili yenu, hivyo msikilizeni Martin Griffiths wakati anapokuambieni, "Mjumbe wa UN anakaribisha uundaji, na anauchukulia kama hatua ya kuelekea suluhisho la kisiasa."
Hakika Salman bin Abdulaziz na mfalme wake mtarajiwa, mwanawe, Muhammad, wanafanya kazi nchini Yemen kwa manufaa ya Amerika, huku Mohammed bin Zayed anafanya kazi kwa manufaa ya Uingereza, kwa hivyo hawatambui kwenu udugu wala ahadi, na hamtaona mema kutoka kwao na hawawezi kukuongozeni kwenye njia sahihi, kwa sababu wao si chochote ila vibaraka tu katika mchezo wa chesi. Wao sio wachezaji halisi.
Hizb ut-Tahrir hapo awali ilitangulia kuwasilisha machapisho kadhaa juu ya Yemen; Kuanzia na lile lililokuwa likikuonyeni kuhusu mzozo juu ya Yemen kati ya Uingereza na Amerika mnamo 2008 M, kisha maendeleo katika uwanja wa Yemen baada ya mapinduzi ya Februari 2011, na wakati muungano ulipoingia vitani mnamo Machi 2015 M, na Mkataba wa Riyadh uliosainiwa mnamo Novemba 2019 M, yenye kuwaonyesha watu wa Yemen wachezaji halisi wa kisiasa wa kimataifa wanaozozania; Yemen Uingereza na Amerika, na inakufuchulieni uongo wa wanasiasa wa hapa wanaokufadhilini, na kukuongozeni jinsi ya kujidanganya kwa msingi wa itikadi yenu, ili mchukue hatua na mpate heshima ya ulimwengu huu na akhera kwa kufanya kazi ya kusimamisha dola ya Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume, kama walivyo fanya watangulizi wenu Maanswar mjini Madina Al-Munawwara. Mtume (saw) amesema:
« ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةٌ عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ»
“Kisha itakuwepo Khilafah (Caliphate) kwa njia ya Utume.” (Imesimuliwa na Ahmad).
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Yemen
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Yemen |
Address & Website Tel: 735417068 http://www.domainnomeaning.com |
E-Mail: yetahrir@gmail.com |