Afisi ya Habari
Wilayah Yemen
H. 25 Rabi' II 1442 | Na: HTY- 1442 / 11 |
M. Alhamisi, 10 Disemba 2020 |
Taarifa Kwa Vyombo vya Habari
Serikali ya Aden Haijali ... Ni Nani Atakomesha Maafa ya Uvujaji wa Mafuta Huko Shabwa?
(Imetafsiriwa)
Gazeti la kila siku la Al-Thawra linalochapishwa jijini Sanaa mnamo tarehe 09/12/2020 lilichapisha ripoti iliyoungwa mkono na picha za kuvuja kwa kila siku kwa idadi kubwa ya mafuta ghafi kwa miezi kadhaa iliyopita kutoka kwa bomba lililobeba mafuta ghafi hao kutoka Sekta ya 4 katika uwanja wa mafuta wa Ayyad magharibi hadi bandari ya Nashima kwenye Bahari ya Arabia kupitia wilaya za Lahiya, Ghayl bin Habtoor, Timur katika jimbo la Shabwa katikati mwa Yemen.
Kuvuja kwa mafuta kulisababisha madoa makubwa kutokana na kuzorota kwa bomba la mafuta ambalo lilianzishwa mnamo 1987 M, pamoja na mashambulizi yaliyolenga kuiba mafuta ghafi, huku kampuni ya mafuta ikisimama na kutazama, kwani haikuchukua hatua zozote kuzuia kuvuja na kuondoa kile kilichovuja kutokana na athari zake hatari kwa wanadamu, wanyama, mimea na maji na mchanga.
Haya ndii matokeo ya makosa yaliyotekelezwa na Wizara ya Mafuta nchini Yemen baada ya kutia saini makubaliano ya utafutaji, uchimbaji na uuzaji wa mafuta kutoka kwa viwanja vya Yemen pamoja na kampuni za mafuta za kigeni, kwani wizara haikupata tu hisa ya zaidi ya asilimia 50 ya ushirika pamoja na wizara kutokana na umiliki wa umma pekee, bali ilipuuzia kuchomwa kwa gesi ya mafuta inayohusiana nayo na haikuikusanya na kuifanya majimaji ili kunufaika nayo, na kampuni za mafuta hazilazimiki kutekeleza viwango vya usalama katika kuondoa majimaji yenye sumu yanayotokana na uchimbaji, na haziwajibiki kwa kufukia majimaji ya uchimbaji karibu na uso wa ardhi, na kwa hivyo uchafuzi wao wa moja kwa moja wa uso wa ardhi na athari zao mbaya kwa aina ya maisha katika maeneo ya karibu. Ukiukaji wa Wizara ya Mafuta ulifikia ukosefu wa kuzilazimisha kampuni zinazozalisha mafuta kushughulikia na kutatua umwagikaji wowote wa mafuta kwani husababisha maafa kwa mazingira, na kuziwajibisha kuondoa viwango vya mafuta yaliyomwagika, na hata kutatua hali ambazo zitaathiri wanadamu, wanyama na mimea kutokana na uvujaji mkubwa wa mafuta. Athari ya mafuta ghafi kwa maisha hutokana na uchafuzi wake wa matabaka yaliyo na maji, na kwa hivyo huchafua visima vinavyozalisha maji kutoka kwa matabaka yaliyochafuliwa, na kusababisha uvimbe kwa wanadamu, kuumiza wanyama na kuharibu mimea, kama Mwenyezi Mungu (swt) anavyosema:
[وَإِذَا تَوَلَّى سَعَى فِي الْأَرْضِ لِيُفْسِدَ فِيهَا وَيُهْلِكَ الْحَرْثَ وَالنَّسْلَ وَاللَّهُ لَا يُحِبُّ الْفَسَادَ]
“Na anapo tawala hufanya juhudi katika nchi kwa kufisidi humo na kuteketeza mimea na viumbe. Na Mwenyezi Mungu hapendi ufisadi.” [Al-Baqara: 205].
Enyi Watu wa Imani na Hekima: Wale wanaowatawala kwa nguvu jijini Sana'a na Aden wameshindwa kukutunzeni vizuri, sembuse kukukingeni na majanga. Majanga ngapi?! Wanakutawaleni kwa mfumo wa kirasilimali unaotenganisha dini na maisha, na kufuata manufaa, na sio kwa hukmu za Itikadi ya Kiisilamu, kwa nini basi mnawatii, na hali ya kuwa wamekurithisheni maangamivu, na kukutieni majanga? Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema:
«كَانَتْ بَنُو إِسْرَائِيلَ تَسُوسُهُمْ الْأَنْبِيَاءُ، كُلَّمَا هَلَكَ نَبِيٌّ خَلَفَهُ نَبِيٌّ، وَإِنَّهُ لَا نَبِيَّ بَعْدِي وَسَيَكُونُ خُلَفَاءُ فَيَكْثُرُونَ. قَالُوا فَمَا تَأْمُرُنَا؟ قَالَ: فُوا بِبَيْعَةِ الْأَوَّلِ فَالْأَوَّلِ، أَعْطُوهُمْ حَقَّهُمْ فَإِنَّ اللَّهَ سَائِلُهُمْ عَمَّا اسْتَرْعَاهُمْ»
“Banu Isra’il wanasiasa wao walikuwa ni mitume wao, kila mtume mmoja akifa mwengine alichukua nafasi yake. Na hakika yake hakutakuwa na mtume mwengine baada yangu, lakini watakuwepo makhalifa na watakuwa ni wengi.” Wakasema je, watuamrisha nini? Akasema: “Mpeni bay'ah (ahadi ya utiifu) mmoja baada ya mwengine, wapeni haki yao kwani hakika Mwenyezi Mungu atawauliza kuhusu yale aliyowapa uchungaji kwayo.” (Bukhari na Muslim)
Fanyeni kazi na Hizb ut-Tahrir ili kusimamisha dola ya Khilafah, kwani italinda milki ya umma na kuzuia kumilikiwa kwake na kampuni za mafuta za kigeni, kukuwezesha kunufaika nayo, na kuzuia uharibifu wake kwa niaba yenu kupitia utumiaji wa nidhamu ya kiuchumi katika Uislamu ndani ya nidhamu zenginezo za kisiasa na kijamii .. nk, katika dola ya Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) asema:
«ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةٌ عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ»
“Kisha itakuwepo Khilafah kwa njia ya Utume”.
[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ]
“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele.” [Al-Anfal: 24]
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Yemen
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Yemen |
Address & Website Tel: 735417068 http://www.domainnomeaning.com |
E-Mail: yetahrir@gmail.com |