Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Uzbekistan

H.  25 Rabi' I 1446 Na: 1446 / 02
M.  Jumamosi, 28 Septemba 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Je, Mahakama ya Rufaa Inaweza Kurekebisha Makosa ya Serikali ya Uzbekistan na Kuwaachilia Huru Wanaodhulumiwa?
(Imetafsiriwa)

Miezi michache iliyopita, wafungwa 23 wa zamani wa kisiasa walihukumiwa huko Tashkent. Ilibainika kuwa 15 kati yao waliainishwa kama “wahalifu hatari sana wa kurudia” na walihukumiwa vifungo vya miaka 7 hadi 14, kutumikia katika kituo maalum cha kizuizi cha serikali. Wanane waliosalia walihukumiwa kifungo cha nyumbani kwa hadi miaka 5.

Ni muhimu kufahamu kuwa Mashababu (wanaume) hawa waliofika mbele ya mahakama walikuwa tayari wamekaa jela miaka 20, ambapo walikuwa wakikabiliwa na shinikizo mbalimbali za kisaikolojia na kimwili. Mawakili wao wamekata rufaa katika Mahakama ya Rufaa ili kuangalia upya kesi hiyo. Kwa sasa, Mashababu 15 wako katika awamu ya rufaa. Kwa mujibu wa taarifa zilizopo, jaji msimamizi wa Mahakama ya Rufaa ni Kuchkarov Sinjar Kuchkarovich. Kesi hii inapaswa kutathminiwa kimsingi kutoka kwa mitazamo miwili: Kisharia (Shari’) na kisiasa. Kwa upande wa Shari’ah, swali linajitokeza: tangu lini kuwalingania watu kwenye njia ya Mwenyezi Mungu imekuwa kosa? Hata hivyo, katika nchi kama Uzbekistan, ambako wasomi mashuhuri kama vile Bukhari na Tirmidhi waliibuka, matukio hayo ya ajabu na yenye kutatanisha yanatokea leo! Kila mtu anajua kwamba kulingania Uislamu na kuishi kwa mujibu wa mafundisho yake ni faradhi kwa kila Muislamu, na dhati ya maisha yao inatokana na imani hii ya kimsingi ya Kiislamu. Je, sio aibu kwa serikali ya sasa ya Uzbekistan kuwaweka vijana hawa mahakamani tena, licha ya kuwa walikuwa wahasiriwa wa “utawala fisadi” uliopita, haswa wakati ukweli uko wazi? Zaidi ya hayo, kutumia ibara “wahalifu hatari sana wa kurudia” kuwahusu si chochote ila ni kutia chumvi na uzushi. Tuambieni, je, watu hawa walijihusisha na ufisadi, hongo, au kufuja mabilioni ya pesa? Je, walipora mali ya taifa? Je, waliuwa? Je, waliwanyima watu haki zao? Je, walisaliti nchi na watu wake kwa kutumikia wakoloni wa kigeni kama vile Urusi na Amerika? Mwishowe, wale wanaofanya mambo makubwa kama haya yaliyoharamishwa na Mwenyezi Mungu mara nyingi hawafichi matendo yao, na wengi wanatembea wakiwa huru, lakini hakuna hata mmoja aliye na ujasiri wa kuwafikisha kwenye haki.

Kwa bahati mbaya, hivi majuzi mahakama hiyo ilimhukumu mtu mmoja ambaye alitoa wito wa kuregeshwa kwa Muungano wa Sovieti wa zamani kifungo cha miaka mitatu pekee. Makosa haya ya kweli yanapata adhabu nyepesi, wakati wale wanaolingania Uislamu wanakumbana na ukali na kutovumiliwa kupindukia! Sera hii ya kinafiki haiakisi chochote ila upendeleo wa utawala wa Uzbekistan dhidi ya Uislamu na kutovumilia kwake Da’wah ya Kiislamu.

Kwa mtazamo wa kisiasa, hakuna shaka kwamba dola za kikoloni kama vile Urusi zinahusika na unyanyasaji wa utawala wa Uzbekistan dhidi ya Waislamu wanaodhulumiwa. Sheria na hatua zinazochukuliwa na utawala huo ili kutokomeza Da’wah ya Kiislamu katika nchi yetu na kuwaweka Waislamu wetu mbali na Uislamu ni kwa ajili ya kuzifurahisha dola hizi. Hata hivyo, hili haliwaondolei viongozi wa serikali wajibu, wala halipunguzi kuhisabiwa kwao mbele ya Mwenyezi Mungu. Kwa kuwa wale walioko serikalini wanajiona kuwa ni Waislamu, basi juhudi zao za kutaka kuwafurahisha watawala wa kikoloni ambao ni maadui wa Uislamu na Waislamu na kujiweka sawa nao, zinachukuliwa kuwa ni kumsaliti Mwenyezi Mungu, Mtume wake na jamii ya Kiislamu. Hakika, Mwenyezi Mungu ameharamisha dhulma na khiyana.

Tunasisitiza kwamba hakuna tishio kwa watu wetu na nchi yetu kutoka kwa vijana hawa au wito wa Kiislamu wanaoubeba. Kinyume chake ni vijana shupavu, tayari kujitolea maisha yao kwa ajili ya Umma huu na watu wake! Hawaoni hata serikali ya Uzbekistan, inayofanya ukatili huu, kama adui yao. Maadui wa kweli wa sisi Waislamu ni dola za kikoloni kama Marekani na Urusi. Hivi kwa nini walio serikalini hawaelewi wanachofanya vijana hawa? Je, hawatafakari juu ya hali ya ulimwengu leo ​​na kutambua nani ni rafiki, na nani ni adui, na hatari ya kweli iko wapi?

Kwa hiyo, tunauambia utawala wa Uzbekistan kwamba haujachelewa; unaweza kurekebisha makosa yake kwa kuwaachilia huru vijana hawa. Zaidi ya hayo, unapaswa pia kuwaachilia huru makumi ya wafungwa wa zamani wa kisiasa ambao wamepelekwa katika magereza mbalimbali. Njia pekee iliyo sawa na sahihi ya wokovu ni kwa utawala huu kuacha kufuata njia za dola za kikoloni, kurudi kwa Mwenyezi Mungu, na kujiingiza katika siasa huku ukishikilia kwa uthabiti mwongozo Wake. Kwa kufanya hivyo huenda wakakuta nyuso zao zikiwa na nuru mbele ya Mwenyezi Mungu na kupata rehema zake, kwani Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema:

[إِنَّ اللهَ مَعَ الَّذِينَ اتَّقَوا وَّالَّذِينَ هُم مُّحْسِنُونَ]

‎‏ “Hakika Mwenyezi Mungu yu pamoja na wenye kumcha, na watendao mema..” [An-Nahl:128].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Uzbekistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Uzbekistan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu