Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Uturuki

H.  18 Sha'aban 1445 Na: 1445 / 11
M.  Jumatano, 28 Februari 2024

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kutoka Karne ya Upotevu hadi Mustakbali wenye Bishara Njema (Karne ya Uislamu)!
(Imetafsiriwa)

Imepita miaka 100 tangu kuvunjwa kwa Khilafah mnamo Machi 3, 1924 M, kuashiria karne kamili tangu maafa makubwa zaidi yaliyowakumba Waislamu katika historia yote ya Kiislamu. Wakati mbegu za mifarakano iliyopandwa na ukoloni wa Kimagharibi miongoni mwa Waislamu katika ardhi za Kiislamu ilipoota mizizi, fikra za utaifa zilienea miongoni mwa Waislamu, na kupelekea kuvunjwa kwa dola hiyo kubwa iliyodumu kwa miaka 1300. Waingereza, kwa kusaidiwa na washirika wao wa ndani, waliivunja Khilafah, ambayo Makafiri hawakuweza kuishinda kwenye medani ya vita. Kwa kuvunjika ngao ya Ummah na mamlaka ya Uislamu, Khilafah, kuvunjwa, Waislamu walipoteza utu na nguvu zao dhidi ya Makafiri. Kwa kuporomoka kwa Khilafah, amani na usalama vilipotea sio tu katika ardhi za Kiislamu bali duniani kote. Dunia ilitawaliwa na ubepari. Dola za kikoloni za Magharibi zilivamia ardhi zetu, zikapora rasilimali za dunia, na kumwaga damu za Waislamu kwa wingi.

Karne hii bila Uislamu ni karne ya upotevu, si kwa Waislamu tu bali kwa wanadamu wote. Ulimwengu unajikwaa katika korido za ubepari muovu, na wanadamu wanakandamizwa chini ya mifumo ya kikoloni. Ni wazi kwamba kile ambacho Magharibi hukiita haki za binadamu, maadili ya kibinadamu, haki, sheria na uadilifu kwa wote ni uongo. Hivi leo, kwa uungaji mkono wa Mayahudi wanaokalia kwa mabavu, nchi zote za Magharibi zinashiriki kwa utaratibu katika mauaji na utekelezaji mauaji ya halaiki dhidi ya Waislamu wachache mjini Gaza kwa takriban miezi mitano mbele ya macho ya dunia nzima.

Kwa sababu Wamagharibi wanaona kuporomoka kwa ubepari na mifumo ya kikoloni, wanajaribu kuzuia mwamko wa Uislamu na Waislamu na kusimamishwa kwa Khilafah. Hata hivyo, hawatafanikiwa, kwa sababu baada ya karne ya upotevu, mustakbali ni wa Uislamu na Waislamu, Mwenyezi Mungu akipenda.

Sisi, katika Hizb ut Tahrir Wilayah ya Uturuki, kwa mnasaba wa kumbukumbu ya miaka 100 ya kuvunjwa kwa Khilafah, tunaanzisha kampeni yenye kichwa "Kutoka Karne ya Upotevu  Hadi Mustakbali wenye Bishara Njema (Karne ya Kiislamu)." Katika muktadha huu, tutafanya makongamano, halaqa za majadiliano, na semina katika miji mingi ya Uturuki. Tunamuomba Mwenyezi Mungu aijaalie kazi yetu iwe ni njia ya kheri. Pia tunawaalika Waislamu wote kuunga mkono kazi zetu na kushiriki katika shughuli zetu na mapambano ya kusimamisha Khilafah.

Enyi Waislamu! Baada ya miaka 100 bila ya Khilafah, ni wakati wa nyinyi kusimama na kuongoza ulimwengu. Ni wakati wa kuifanya dunia kuwa mahali pazuri pa kuishi tena kwa nuru ya Uislamu, uadilifu wake, rehema na baraka zake. Zaidi ya hayo, matukio ya Gaza katika kipindi cha miezi mitano pekee iliyopita yanaonyesha ukubwa wa haja yetu a Khilafah. Miaka mia moja iliyopita, tulikuwa na Serikali na Khalifah (Khalifa). Leo, kuna dola 57 na viongozi 57, lakini hawachukui nafasi ya Khalifa mmoja. Matukio ya Gaza yamevua barakoa za watawala na kufichua jinsi walivyo kuwa vibaraka watiifu wanaothamini viti vyao. Kwa hiyo, jiepusheni na mifumo na sheria hizi zilizopitwa na wakati, na fanyeni kazi kuelekea kusimamisha mfumo wa Mwenyezi Mungu duniani na kusimamisha Khilafah. Dhurufu za kilimwengu ni nzuri kwa ajili ya kusimamishwa kwake, na Waislamu na hata watu wa Magharibi wanatazamia kwa hamu Uislamu na Khilafah. Ulimwengu mzima unahitaji Khilafah na baada ya karne ya upotevu, karne hii itakuwa karne ya Uislamu, Mwenyezi Mungu akipenda. Basi simameni kutimiza ahadi ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na fanyeni kazi ya kupata bishara njema ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw). Wala msisahau kwamba ushindi unatoka kwa Mwenyezi Mungu pekee, na siku hiyo Waumini watafurahi.

«ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةٌ عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ»

“Kisha itakuwepo Khilafah kwa njia ya Utume.” [Imepokewa na Ahmad].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Uturuki

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Uturuki
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu