Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Uturuki

H.  5 Dhu al-Qi'dah 1444 Na: 1444 / 14
M.  Alhamisi, 25 Mei 2023

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Bandari Mpya ya Miungano "Uadui kwa Wakimbizi"
(Imetafsiriwa)

Kwa kuwa hapakuwa na mgombea ambaye asilimia ya kura zake zilizidi 50 + 1 katika uchaguzi uliofanyika Jumapili, Mei 14, raundi ya pili ya uchaguzi itafanyika mnamo Jumapili, Mei 28. Kwa sababu ya kauli zilizorushianwa kati ya miungano, vyama na viongozi wakati wa mchakato wa uchaguzi, jamii iligawanywa katika sehemu mbili, na watu wakawa maadui wa kila mmoja. Ambapo wanasiasa walituhumiana kwa maneno machafu na ya matusi kama vile magaidi, wezi, waongo, walaghai na wanyang'anyi, na wakapikiana majungu. Hii iliwalazimu Waislamu wa Uturuki kuchagua kati ya mfumo wa urais wa mtindo wa Marekani unaopigiwa upatu na Muungano wa Watu, na mfumo wa bunge wa mtindo wa Uingereza unaopigiwa upatu na Muungano wa Taifa. Pande zote mbili zimeonyesha kuwa uchaguzi huu muhimu ni suala la uhai au kifo. Wakati huo huo, ilibainika kuwa ukosefu wa maadili katika siasa ulifikia kilele katika mchakato huu wa uchaguzi; ambapo wanasiasa walizikanyaga sheria, kanuni na maadili yao wenyewe kwa kufanya hesabu za mapato ya kibinafsi kwa ajili ya manufaa na maslahi.

Wagombea hao wawili ambao hawakuweza kufikia asilimia ya kutosha ya kura katika raundi ya kwanza ya uchaguzi huo, sasa wanatafuta kujiunga na muungano wa Jacobin, wa ATA wenye ubaguzi wa rangi, unaolea uhasama dhidi ya wakimbizi na kuzua uhasama na vitendo na balagha. Ili kila mmoja kumshinda mwengine, wagombea wa miungano yote miwili walikaa kando na Sinan Ogan na Umit Ozdag na kujadili hali ya ndugu zetu wa Syria waliokimbilia katika nchi yetu kulinda maisha, heshima na watoto wao. Ingawa wanajua fikra ya Sinan Ogan na Umit Ozdag, ambao walikuwa wakiendesha kampeni ya uchaguzi kwa kulisha uhasama kwa wakimbizi, waliiendea bandari ya uadui kwa wakimbizi katika raundi ya pili ili kushinda uchaguzi. Mwishoni mwa majadiliano haya, mgombea wa Muungano wa Watu Erdogan alikubaliana na Sinan Ogan, na mgombea wa Muungano wa Kitaifa Kilicdaroglu akakubaliana na Umit Ozdag.

Katika maandishi ya makubaliano ya pamoja yaliyokubaliwa na Kilicdaroglu na Ozdağ, iliandikwa kwamba wakimbizi wote na wale wanaokimbia, haswa Wasyria, watarejeshwa ndani ya kipindi cha mwaka mmoja hivi karibuni. Katika mkutano na waandishi wa habari, Umit Özdag alisema kuwa mgogoro wa kiuchumi utatatuliwa tu kupitia kurejea kwa wakimbizi. Alidai kuwa wakimbizi ndio chanzo cha kupanda kwa bei ya kodi, ukosefu wa ajira, kuenea kwa dawa za kulevya na hata ukosefu wa usalama mitaani. Kulaumu kwa Ozdag kwa matatizo yote ya jamhuri ya kisekula ya miaka 100 kwa wakimbizi kuko mbali na ukweli na kunatokana na uadui wake dhidi ya Uislamu na Waislamu.

Ukweli kwamba Chama cha Ushindi na kiongozi wake, waliotengwa kwa vitendo na maneno yao, wanafikiwa na miungano, na kujadiliana juu ya suala la wakimbizi kwa 2.23% ya kura walizopata katika raundi ya kwanza, inaonyesha kuwa chochote kinaweza kufanywa kupata viti na manufaa. Maneno ya shauku yaliyosemwa kabla ya uchaguzi wa Mei 14 kuhusu udugu wa Kiislamu wa Muhajirina na Ansar yalisahauliwa. Kadhalika, Waziri wa Mambo ya Nje Mevlut Cavusoglu alisema kuwa zaidi ya wakimbizi 550,000 wa Syria wamerudishwa katika maeneo yanayodhibitiwa na Uturuki, na lengo lao sasa ni kuwapeleka katika maeneo yanayodhibitiwa na utawala huo.

Enyi Waislamu: Ukweli kwamba uchaguzi wa kidemokrasia hauwezi kutatua matatizo na dhiki ni ukweli unaong'aa. Kwa sababu msingi wa serikali ni mbovu, mfumo wake ni mbovu, na kazi yake ni mbovu. Kwani chanzo cha matatizo ya kiuchumi, kisiasa na kimaadili ambayo jamii inakabiliwa nayo, sio wakimbizi, bali ni mfumo wa kisekula unaotekelezwa. Mfumo usipobadilika, unyonyaji, taabu, dhulma, ufisadi, rushwa, upendeleo na uasherati utaendelea kwa kasi kubwa. Kwa hivyo hakuna kitakachobadilika na uchaguzi. Kwa hiyo wanachopaswa kufanya Waislamu ni kubadili mfumo na sio vyama, viongozi, wabune au serikali, kitu chengine chochote isipokuwa Uislamu ni batili na dhulma. Uislamu ndio Dini pekee ya haki kutoka kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote na mfumo mpana wa maisha unaotatua matatizo yote. Na njia pekee ya kuutabikisha Uislamu ni dola ya Khilafah Rashida ambayo itarejesha maisha kamili ya Kiislamu. Waislamu wanyofu wanapaswa kulingania na kufanya kazi kwa ajili ya kusimamishwa kwake.

[أَفَحُكْمَ الْجَاهِلِيَّةِ يَبْغُونَ وَمَنْ أَحْسَنُ مِنَ اللَّهِ حُكْماً لِّقَوْمٍ يُوقِنُونَ]

“Je, wao wanataka hukumu za Kijahiliya? Na nani aliye mwema zaidi katika kuhukumu kuliko Mwenyezi Mungu kwa watu wenye yakini?” [Al-Ma’ida: 50].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Uturuki

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Uturuki
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu