Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Uturuki

H.  3 Rabi' II 1441 Na: 1441 / 05
M.  Jumamosi, 30 Novemba 2019

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kuifufua Jamii Inategemea Kusimamishwa kwa Uislamu
(Imetafsiriwa)

Wakati wa Baraza la 6 la Kidini lililoandaliwa na Bodi Kuu ya Uongozi wa Maswala ya Kidini huko Ankara kuanzia tarehe 25 hadi 28 Novemba 2019, majadiliano kadhaa yalifanyika kwa lengo la kubaini mikakati mipya inayohusiana na huduma za Maswala ya Kidini, katika muktadha wa athari ya mabadiliko katika uelewa wa kidini juu ya mpangilio wa kijamii na kitamaduni ambao unajilazimisha wenyewe ulimwenguni kote, ambao umeathiri mahusiano ya dini na maisha na mustakbali wa dini. Mashauriano yalimaliza kazi yake kwa kushiriki kwa Erdogan, rais wa jamhuri, na usomaji wa taarifa ya mwisho iliyojumuisha vifungu 37. Taarifa ya mwisho ilijumuisha misemo hii: “Sawia na kinachotokea kote ulimwenguni, mabadiliko ya kiuchumi, kijamii na kitamaduni yameongezeka kama matokeo ya athari za utandawazi na sababu nyingine nyingi, pia kiwango cha tishio kimefikia itikadi za kidini, maadili na utamaduni wa kitaifa. Kwa upande mwingine, kutokana na athari za utandawazi aina ya utamaduni maarufu umetengenezwa ambao haujali kuhusu maadili au itikadi za kidini haswa miongoni mwa watoto na vijana. Hali hizi mpya zimetia sintofahamu katika maisha ya kidini, kudhoofisha uwezo upinzani wa Waislamu na kutia shauku juu ya mtizamo wa mustakbali.” Kwa kuongezea, maendeleo ya kisayansi na kiteknolojia pia yamefanya njia ya kufikiria ya kisayansi na mbinu ya kifalsafa ya kubadilisha kwa uelewa ambao unabadilsha dini kwa kiwango kikubwa. Na imekuwa ni kigezo cha kutishia uwepo wa dini na dori yake, na kwa hivyo imepelekea udhalimu wa dini binafsi na kuzaliwa kwa miito mipya ya kidini ambayo iko mbali na mtazamo sahihi wa dini. Kuanza kwa mfumo huu msisitizo uliwekwa kwenye maamuzi muhimu yaliyoelezea nini kifanyike kukabiliana na mabadiliko ya kitamaduni na kijamii ambayo yanafisidi watu binafsi na jamii, licha ya hayo, chanzo cha kesi na sababu zake na suluhisho sahihi ambazo zinalingana na Imani ya Kiislamu zimepuuzwa.

Ukweli ni nchi yenyewe, na nidhamu ya kikafiri ambayo inatabikisha; inasimama nyuma ya kukengeuka kutoka katika dini na mabadiliko ya kijamii na kitamaduni katika Ummah wa Kiislamu kwa ujumla na jamii nchini Uturuki haswa. Kama serikali ndiyo inayokuza uelewa wa kidini kuendana na mfumo wake wa kidunia, tangu uamuzi wake mbaya uliovunja Khilafah katika mwaka wa 1924, na kusimamisha mambo ya kidini ili iweze kutoa huduma kwa niaba ya maisha ya kidini – kama inavyodai –chini ya kivuli cha nidhamu ya kidemokrasia ya kidunia “bila ya kugusa mfumo wa kikafiri uliopo au hata kufikiria kuubadilisha”.

Kwa bahati mbaya Uongozi wa Maswala ya Kidini haukuweza kumaliza kazi hii na msingi huu wa kifisadi ili kuweza kuiondoa jamii katika michakato inayoendelea ya ufisadi. Kwa kweli huwezi kamwe kuishi kulingana na dini au kuitetea chini ya nidhamu ya kisekula. Kwani Uislamu na itikadi yake na sheria zake ni mfumo hai unaokusanya mambo yote ya kimaisha. Uongozi wa Maswala ya Kidini unautizama Uislamu kama tamaduni, na unafundisha na kusambaza na kuhamasisha misikiti na maimamu ndani ya mpangilio huu, na kujaribu kulinda umoja wa familia: wanawake, vijana na wavulana pamoja na mtaala wa kisasa ambao ni bidhaa ya Wamagharibi, hata kama walibeba katika majengo yao wanasayansi ambao wana sifa ya kisayansi na kitaaluma; kwa bahati mbaya haitoweza kupata matokeo iyatakayo.

Hivyo basi, haitakuwa na chaguo jingine isipokuwa kupoteza juhudi za dhati za watoto wa Ummah huu, na kupoteza wakati mwingi, na kusimama – kutafuta hifadhi ya Mwenyezi Mungu – uso kwa uso na hatari mbaya. Kazi ambayo Uongozi wa Maswala ya Kidini imejitwika juu yake, na huduma ambazo huwasilisha, na matokeo ya yote hayo; yanaonekana wazi.

Hapana shaka kuwa juhudi za dhati ambazo zinafanywa zinastahili kushukuriwa na kuthaminiwa, lakini kinachohitajika na Uongozi wa Maswala ya Kidini na wasomi sawa na wale wenye uelewa sahihi wa Uislamu miongoni mwa watoto wa Ummah ni kunyanyuka na kuanza kukiri kuwa asili ya ufisadi katika Ummah na jamii ni watawala na wanachuoni, na kuhofiwa kuhesabiwa na Mwenyezi Mungu, na kutoa maelezo yao ya kuwa warithi wa Mtume ni haki yao, na kumiliki mwito wa mabadiliko makubwa bila kuogopa lawama ya mtu yeyote. Na wanapaswa kurejesha maisha ya Kiislamu kwa ukamilifu, na kuanzisha Dola la Khilafah ya uongofu kwa Njia ya Utume kufuata ahadi ya Mwenyezi Mungu na bishara njema za Nabii Wake (saw) na kung’oa nidhamu za kikafiri kutoka katika nchi za Kiislamu kwa hivyo zisirudi tena kamwe, na kuelewa kuwa bila hili hakuna njia nyengine ya kuweka kikomo kwa mchakato uliopo wa kuumaliza ufisadi

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ اسْتَجِيبُواْ لِلّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُم لِمَا يُحْيِيكُمْ وَاعْلَمُواْ أَنَّ اللّهَ يَحُولُ بَيْنَ الْمَرْءِ وَقَلْبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ﴿

“Enyi mllio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele, na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake na kwamba hakika kwake Yeye tu mutakusanywa.” [Al-Anfal: 24]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Wilayah Uturuki

 

 

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Uturuki
Address & Website
Tel: 
http://www.hizb-turkiye.org
E-Mail: bilgi@hizb-turkiye.org

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu