Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Nchi Zinazozungumza Kijerumani

H.  29 Rajab 1441 Na: 1441 / 04
M.  Jumanne, 24 Machi 2020

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kuhusu Janga la Virusi vya Korona
(Imetafsiriwa)

Kuenea kwa janga la virusi vya Korona na matokeo yake yamedhihirisha mapengo makubwa katika mfumo wa Kirasilimali na nidhamu huru ya Kijamii. Punde tu janga hilo lilipotokea katika mkoa wa China wa Hubei, mtingishiko mkubwa ulitokea katika Soko la Fedha la Kimataifa. Ndani ya wiki chache, farahisi ya soko la hisa la Ujerumani (DAX) ilipungua kwa asilimia 40, na kuporomoka kwa alama 8.442 na 17/3. Pamoja na kuongezeka kwa idadi ya waliojeruhiwa, harakati za kiuchumi na maisha ya umma nchini Ujerumani yalikaribia kusimamishwa kikamilifu, kiasi kwamba Chansela wa Ujerumani alisema mnamo tarehe 18/3/2020, “Tangu kuunganishwa kwa Ujerumani, hapana, tangu Vita Vya Pili vya Dunia, hakuja kuwepo na changamoto yoyote kwa taifa letu iliyo hitaji kiwango cha hatua za kawaida na za pamoja...”

Baada ya kusitasita mwanzoni, Serikali ya Majimbo iliamua kufunga taasisi zote za kielimu na maduka ambayo hayakuchangia kuhakikisha usambazaji wa bidhaa msingi. Pia, uhuru wa kuzunguka ulipunguzwa, matamasha ya umma na mikusanyiko, na makutano ya moja kwa moja kati ya watu yamezuiliwa, yote chini ya tishio la adhabu kali. Na huku Kampuni za Kimataifa, kama vile Mercedes, Volkswagen na BM zimeamua kufunga viwanda vyao, kampuni nyingi zisizo hesabika ndogo ndogo na za wastani zinahofia kufilisika kikamilifu. Kwa mujibu wa makadirio ya Wizara ya Kazi, idadi ya watu wasio na ajira wanaopokea pensheni ya usalama wa jamii itaongezeka kwa milioni 1.2 kama matokeo ya janga hili. Mnamo tarehe 21 Machi, Waziri wa Fedha, Olaf Schultz, alitangaza kutenga vifurushi vya misaada ya kifedha vya mabilioni ya dolari ili kukabiliana na kudorora kwa uchumi. Pia alitangaza nia ya serikali ya kuongeza deni hilo kwa euro bilioni 156 na kuunda mwavuli wa uokoaji wa kifedha ambao unaweza kufikia euro bilioni 600. Mwishowe, Benki ya Shirikisho la Ujerumani ilitangaza katika ripoti yake ya kila mwezi tarehe 23/3 yafuatayo: “Mtelezo katika mdororo wazi hauepukiki ... Mbali na kuporomoka huku, maendeleo ya kiuchumi yanaonyesha shauku isiyo ya kawaida”.

Mfumo wa afya wa Ujerumani pia uko kwenye hatari ya kufilisika katika wiki chache kutokana na janga hili. Gerald Gass, Rais wa Jumuiya ya Hospitali ya Ujerumani, anakadiria kuwa vitanda 28,000 vya utunzaji mkubwa vitatengwa kikamilifu, na anakosoa ukweli kwamba majimbo yanayowajibika kwa hospitali hayakuwekeza vya kutosha katika sekta ya kliniki ya hospitali. Kulingana na takwimu za Taasisi ya Hospitali ya Ujerumani, kuna upungufu wa takriban 17,000 wa wafanyikazi wa hospitali katika vituo vya afya, na kwamba hospitali tatu kati ya nne zinatafuta madaktari. Hali katika jimbo la Rhine-Westphalia Kaskazini inaonekana kuwa mbaya zaidi, kwani ndilo jimbo lililoathiriwa zaidi na janga hilo. Mamlaka ya Hospitali ya Rhine-Westphalia Kaskazini imekosoa kwamba vifaa vya kuzuia katika vituo vingi vya afya vinatosha kwa siku 14 pekee. Alikosoa ukweli kwamba majukumu yalibandikwa moja kwa moja kwa vyama vingine: Muungano huo unashikilia jukumu kwa majimbo, na majimbo yanabeba jukumu la hospitali, na kadhalika. Tatizo, kwa mujibu wa taarifa ya mamlaka, ni kwamba mfumo wa afya wa Ujerumani unategemea ufanisi wa uchumi, na kwamba asilimia 40 ya hospitali hunakili hasara. Mfumo mbovu wa afya pia unaonyesha udhaifu wa silsila ya usambazaji wa kimataifa. Waziri wa Afya wa Rhine-Westphalia Kaskazini, Karl Josef Laumann, alilazimika kukiri ukweli huu hadharani, na hii ilikuwa tarehe 8/3, ambayo ni, kabla ya hali kuwa mbaya zaidi.

Hata uti wa mgongo wa Jumuiya ya Ulaya, zoni ya Schengen, iko kwenye hatari kubwa kwa sababu ya janga la virusi vya Korona. Mbali na Ujerumani, karibu nchi 12 za Ulaya sasa zinafanya ukaguzi wa mipaka ndani ya Soko la Pamoja, ikisimamisha kabisa matembezi ya bidhaa na watu. Hii ilisababisha msongamano wa trafiki wa kilomita kadhaa kwenye mipaka ya ndani ya Soko la Pamoja, na kufikia kilomita sitini kwenye mpaka wa Ujerumani-Poland!

Janga la virusi vya Korona limeonyesha ulimwengu kwa mara nyingine tena jinsi gani mfumo wa kiuchumi wa kirasilimali ulivyo dhaifu. Nguvu za soko ambazo zinapaswa kusababisha usambazaji mzuri wa rasilimali hazijafanikiwa. Nguvu hizi zilishindwa kwa mara ya tatu katika miongo miwili iliyopita baada ya janga la kifedha la 2008 na janga la euro la 2010. Serikali zinalazimika kuingilia kati tena ili kuokoa soko huru kutokana na kuanguka, ingawa fikra halisi ya kirasilimali inakataza hilo. Hivyo, ikawa wazi kuwa mantiki ya ufanisi wa kiuchumi imedhoofisha sana mfumo wa kinga ya jamii. Ikiwa kampuni, taasisi za elimu, na hata hospitali zinafanya kazi kulingana na kiwango cha chini na kiwango cha juu cha upembuzi yakinifu wa kiuchumi, mshtuko mdogo unatosha kuvuruga mifumo yote ya miundombinu. Kwa sababu ya uzinduzi wa msingi wa maendeleo na mantiki ya matarajio ya masoko ya fedha, viashiria hasi vya kiuchumi vimeathiri moja kwa moja uchumi wa kihakika, na kufunua nguvu zao za uharibifu kwa njia ya kufilisika kwa kuendelea na ufutaji wa wafanyikazi wengi. Kwa sababu ya utandawazi, ambao umesababisha kuingiliana kukubwa kwa masoko kwa sababu ya kuongezeka kwa biashara ya kimataifa, shughuli za kifedha na uwekezaji, uchumi mzima wa kiulimwengu umeanikwa wazi zaidi kwa hatari za kimfumo. Kwa hivyo, janga liliweza kugeuka kuwa janga la kiuchumi la kimataifa ambalo mwisho wake bado haujulikani.

Mfumo huru wa kijamii pia umetikiswa na janga hilo. Hatua za kuzuia zilizo chukuliwa zimepunguza sana uhuru ulio dhaminiwa na Katiba. Stephen Giuseppe, profesa wa falsafa katika Chuo Kikuu cha Freie huko Berlin, anasema: “Ninaona kufungwa kwa vitongoji vyote na miji kuwa ni shida mno ... Ni kweli kwamba mtu binafsi humalizika wakati uhuru wa wengine unapo kiukwa, lakini kupunguza uhuru huu kwa sababu za kisiasa na za kishirika - hili ni gumu...”. Lakini jambo kubwa mbele ya jamii ya huru ni kwamba katika shida hii wanalazimika kusawazisha maisha ya watu dhidi ya wao kwa wao! Kwa sababu ya ukosefu wa vifaa na wafanyikazi katika sekta ya afya, madaktari lazima watapendelea wagonjwa wenye matarajio makubwa ya kupona, na waache wengine kwa majaaliwa yao. Picha ya mwanadamu na jamii inayo chorwa na usekula katika akili za watu na ambayo kwayo mtu binafsi sio sehemu ya kikundi na hadhibitiwi chini yake, picha hii imeonyesha kutofaulu kwake katika hali ya sasa ambayo inahitaji juhudi za pamoja, ambayo kwa upande mwengine inahitaji kujitolea muhanga kwa watu binafsi. Imeonekana dhahiri kuwa muundo huu wa kimfumo wa jamii ambao kwao dola inapata uhalali wake kulinda tu uhuru wa watu binafsi ni udanganyifu hatari ambao hauwakilishi uhalisia wa mwanadamu, sio katika nyakati za kawaida wala katika nyakati za majanga.

Hizb ut Tahrir katika Nchi Zinazo zungumza Kijerumani inatoa wito watu wa Ujerumani kulichukulia tukio hili kuu kuwa ndio sababu ya uhakiki kamili wa kiitikadi. Mfumo dhaifu kama huu, ulio jengwa juu ya msingi wa utendakazi usio wa kihakika wa kiuchumi na ukuaji kamili, utaongoza jamii kwenye ukingo wa kuzimu mara kwa mara tena, na utashindwa kutatua shida za watu kwa usahihi na uthabiti. Mfumo tu unao linganisha ukweli na kukubaliana na umbile la kibinadamu kikamilifu ndio pekee unaotoa njia ya kujinasua kutokana na mzunguko huu baina ya furaha ya kibinafsi na mwamko mchungu katika msingi wa ukweli. Ni Uislamu ndio ulio wafinyanga na kuwaunganisha watu ndani ya kinu kimoja, na kuwapa utulivu wa kiuchumi na kimfumo ndani ya Dola ya Kiislamu kwa miaka 1,300..

(وَمَا أَرْسَلْنَاكَ إِلَّا رَحْمَةً لِلْعَالَمِينَ)

“Nasi hatukukutuma, [Ewe Muhammad], ila uwe ni Rehema kwa walimwengu wote.” [Al-Anbiya: 107].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Nchi Zinazozungumza Kijerumani

#Covid19  #Korona  كورونا#

 

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Nchi Zinazozungumza Kijerumani
Address & Website
Tel: 0043 699 81 61 86 53
Fax: 0043 1 90 74 0 91
E-Mail: shaker.assem@yahoo.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu