Afisi ya Habari
Uingereza
H. 10 Jumada II 1441 | Na: 1441 H / 14 |
M. Jumanne, 04 Februari 2020 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Chuki za Ofsted dhidi ya Uislamu ni Dhahiri kuwa ni Msukumo wa Uongo
Shule huru ya Kiislamuu inatafuta tathmini ya mahakama kuhusu kushindwa kwake katika kufaulu ukaguzi wa viwango vya ubora wa elimu kwa msingi kwamba katika maktaba yake kuna vipeperushi vyenye zaidi ya miaka 25 vikifafanua juu ya Kongamano la Khilafah lililo andaliwa na Hizb ut Tahrir nchini Uingereza mnamo 1994.
Kongmano hili lili fanyika katika viwanja vya Wembley na kuhudhuriwa na Waislamu zaidi ya elfu kumi kutoka maeneo mbalimbali ya nchi. Kongamano hili liliibua swali kuhusu athari za ukoloni katika ardhi za Waislamu na kuwalingania washiriki kuubeba ujumbe na kulingania kuhusu kuukataa ukoloni na badala yake wahitajie kurejea kwa Khilafah ya Kiislamu, ambayo itaukinga Ummah wa Kiislamu kutoka katika uovu wa ubeberu wa magharibi.
Khilafah huchaguliwa na Waislamu ili itawale kwa mujibu Shariah za Kiislamu ambazo chimbuko lake hasa ni Qur’an na Sunnah za Mtume (saw); ambazo huleta amani na mafanikio kwa watu. Kinyume chake ni kwamba ukoloni Umagharibi haukuleta katika ulimwengu chochote zaidi ya umwagaji damu, umasikini na uharibifu.
Mtazamo wa kwamba toleo linalohusu kongamano ni sababu tosha ya kutofaulu shule katika ukaguzi kwa msingi kwamba kunawasilisha hatari kwa usalama wa watoto, taasisi hii isiyokuwa ya kiserikali lakini inapokea msaada wa serikali; ina dhihirisha kutotenda haki na pia kuwa na upendeleo: Afisi ya Viwango vya Elimu, Huduma za Watoto na Ujuzi (Ofsted). Uingereza huwapa upendeleo wasomi wake na serikali yake huenda mbio kuhuisha ukoloni wake, pia kufanya juhudi kuonesha utukufu wa ubeberu wao. Ofsted hakika ni mwangwi wa utamaduni dhaifu na ipo tayari kutoa maagizo yasiyoingia akilini ili kuwatishia watu waukatae Uislamu kwa kuhofia usalama wao.
Hakika, hatari halisi katika kuwalinda watoto ipo katika kutangaza na kuendeleza matendo na maneno ya wasomi wa kisekula, kuwafundisha watoto kuhudumu kama askari watiifu wa jeshi dhidi ya “tishio” kama sifa iliyo bebwa ndani ya mfumo wa maisha ya Kiislamu katika Magharibi.
Bishara ya Mtume (saw) kwamba Khilafah itarudi tena, hakika itatatimia, na wakoloni walafi wameingiwa na wasiwasi kwamba biashara zao za kikoloni zitakoma ikisimama. Huu ndio msingi wa hakika wa ajenda za chuki za serikali dhidi ya Uislamu na Waislamu. Cha kusikitisha ni kwamba Ofsted na zaidi vyombo vya habari vimejiruhusu kutumika kama mawakala wa kueneza uongo wa ubinafsi unaotoka kwa wasomi wateule wakitaraji malipo kidogo sana.
Waislamu katika Uingereza na pia watu wote yapasa kuona upotoshaji wa Ofsted, vyombo vya habari na serikali. Kwa sasa lazima tufahamu kwamba sio tu ni msukumo wa chuki zao dhidi ya Uislamu, bali ni maradhi ya uraibu wa matakwa yao binafsi, ambayo yakiwekwa pamoja na kutokuwepo kwa misingi imara, huwapa nafasi ya kuongea uongo ili kuhalalisha matukio maovu dhidi ya ubinadamu.
Yahya Nisbet
Mwakilishi Kwa Vyombo vya Habari Hizb ut Tahrir Uingereza
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Uingereza |
Address & Website Tel: +44 (0) 7074 192400 www.hizb.org.uk |
E-Mail: media@domainnomeaning.com / press@hizb.org.uk |