Afisi ya Habari
Uingereza
H. 3 Rajab 1445 | Na: 1445 H / 10 |
M. Jumatatu, 15 Januari 2024 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Hizb ut Tahrir / Uingereza Yalaani Tangazo la Serikali ya Uingereza Kukipiga Marufuku Chama Hiki
(Imetafsiriwa)
Tangazo la leo la Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uingereza kutaka kuipiga marufuku Hizb ut Tahrir ni hatua ya kutapatap ya kudhibiti mjadala kuhusu mauaji ya halaiki nchini Palestina na kusitisha badali adilifu ya kisiasa ya Uislamu.
Hizb ut Tahrir inakanusha vikali wazo lolote kwamba ni chama cha chuki dhidi ya Mayahudi au kinahimiza ugaidi. Mara kwa mara tumetoa wito wa kusimamishwa upya kwa mfumo wa Kiislamu katika Mashariki ya Kati ulioruhusu Mayahudi, Waislamu na Wakristo kuishi bega kwa bega kwa karne nyingi. Ni maadili matukufu ya Uislamu ambayo huondoa dhulma kutoka kwa jamii na haibagui rangi, kabila, dini au jinsia. Kwa hakika ni ugaidi pekee ni ule unaofanywa hivi sasa na umbile la Kizayuni huko Gaza, likiungwa mkono na wanasiasa wa Uingereza ambao wanahusika katika uhalifu wa kivita, mauaji ya kikabila na mauaji ya halaiki.
Kwa kutaka kuipiga marufuku Hizb ut Tahrir, Uingereza itaungana na dola kama vile Urusi ya Putin, Misri ya Sisi na dola nyenginezo za kiimla katika kunyamazisha sauti ya kuregesha hadhara badali ya Kiislamu kwa ulimwengu wa Kiislamu. Pia inadhihirisha kwamba mazungumzo yote kuhusu mjumuiko anuwai, kupinga udhibiti na uhuru wa kuzungumza, yanakubalika tu mradi tu mtu akubaliane na ajenda ya Wazayuni wenye itikadi kali ya 10 Downing Street.
Hizb ut Tahrir ina rekodi ya zaidi ya miaka 70 ya kufuata njia ya shughuli za kisiasa zisizo na vurugu dhidi ya madikteta wanaotawala ulimwengu wa Kiislamu kwa idhini ya Magharibi. Katika kazi yake ya kusimamisha Khilafah ya Kiislamu, Hizb ut Tahrir haijawahi kutumia aina yoyote ya vurugu au mapambano ya kisilaha. Katika historia yake imefanya kazi kwa njia za kifikra na kisiasa huku wanachama wake wakiteswa na kuuawa kwa maelfu.
Hizb ut Tahrir Uingereza inasema kwa uwazi kwamba itapinga marufuku hiyo iliyopendekezwa kwa kutumia njia zote za kisheria zinazopatikana. Bila kujali matokeo kwa Hizb ut Tahrir, mapambano ya kisiasa katika kuangazia mauaji ya halaiki huko Gaza, kufichua ajenda ya kikoloni ya nchi za Magharibi na wajibu wa kufanya kazi ya kuregesha Uislamu kama mfumo adilifu wa maisha daima itaendelea.
Vidokezi kwa Wahariri:
Hizb ut Tahrir / Uingereza itafanya Mdahalo kwenye mtandao wa X kesho (Jumanne 16 Januari 2024) ili kujadili zaidi hali nchini Palestina, Yemen na kanda nzima.
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Uingereza
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Uingereza |
Address & Website Tel: +44 (0) 7074 192400 www.hizb.org.uk |
E-Mail: media@domainnomeaning.com / press@hizb.org.uk |