Afisi ya Habari
Uingereza
H. 22 Rabi' II 1445 | Na: 1444 H / 06 |
M. Jumatatu, 06 Novemba 2023 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Wajumbe Jijini London Watembelea Misheni ya Kidiplomasia ya Waislamu ili Kuzihisabu Serikali kwa Kutochukua Hatua kwao Juu ya Ukaliwaji Kimabavu wa Palestina
(Imetafsiriwa)
Hizb ut Tahrir / Uingereza ilituma wajumbe kwa misheni ya kidiplomasia ya nchi za Waislamu ambazo hadi sasa zimepuuza kuchukua hatua kali kuwaokoa watu wa Gaza na kumaliza ukaliaji kimabavu wa Palestina. Wajumbe hao walitembelea Balozi zilizoko jijini London za Misri, Uturuki, Saudi Arabia na Pakistan kuwakumbusha jukumu lao kwa Ummah na wajibu wao kwa Mwenyezi Mungu (swt).
Uliwasilisha ujumbe ambao ulionyesha jinsi serikali hizo zilivyojitenga na watu, ambao wamezitaka kuchukua hatua madhubuti, ikiwemo uhamasishaji wa rasilimali za kijeshi, kulinda watu wa Palestina, mali zao, na ardhi yenyewe iliyobarikiwa.
Ujumbe pia ulijaribu kuwashirikisha wale waliokuwepo katika majadiliano kuhusu ukosefu wa nguvu halisi wa uvamizi wa Wazayuni; na kwamba ulinzi wake mkuu ni kukataa kwa nchi jirani kuchukua hatua dhidi ya maslahi ya wakoloni.
Hatimaye, ujumbe uliwasilisha mpango wa nukta 10 zifuatazo za muitiko mmoja wa ulimwengu wa Kiislamu:
1. Kubatilisha mara moja mikataba yote ya amani na umbile la Kizayuni na kuwafukuza wawakilishi wao.
2. Kusitisha aina zote za ushirikiano wa kijasusi, utoaji njia za majini na angani.
3. Kukomesha aina zote za ushirikiano pamoja na uhusiano wa kibiashara na kitamaduni.
4. Kuzuia usambazaji wote wa mafuta kwa umbile la Kizayuni.
5. Kutekeleze kizuizi cha majini katika Bahari ya Mashariki mwa Mediterenia na Ghuba ya Aqaba ili kuzuia silaha zinazofikia jeshi la Kizayuni la mauaji ya halaiki.
6. Kufungua mipaka kwa majeshi jirani ya Waislamu kulizunguka umbile la Kizayuni.
7. Kushirikiana na Pakistan kuhamasisha na kupeleka silaha zake za nyuklia kwa eneo hilo ili kuzuia uvamizi wa mauaji ya halaiki kutokana na hata kufikiria juu ya kutumia silaha za nyuklia.
8. Kutenganisha mauzo yote kwa masoko ya kimataifa kutokana na dolari.
9. Ulimwengu wa Kiislamu lazima ujumuike kwa haraka na uchunguze machaguo yote ya kuikumbusha Marekani kuhusu jinamizi la siasa ya kieneo, kiasi kwamba italazimika kuchagua kati ya kulisaidia umbile la Kizayuni, kuilinda Ulaya, au kuzilinda nchi za Asia Pasifiki.
10. Kukoma kuitambua sheria ya kimataifa, ambayo Magharibi huichana ipendapo.
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Uingereza
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Uingereza |
Address & Website Tel: +44 (0) 7074 192400 www.hizb.org.uk |
E-Mail: media@domainnomeaning.com / press@hizb.org.uk |