Afisi ya Habari
Uingereza
H. 9 Rabi' I 1442 | Na: 06 / 1442 H |
M. Jumatatu, 26 Oktoba 2020 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Uislamu Umejengwa Juu ya Fikra Angavu na Hatupaswi Kukubali Chochote Kutoka kwa Watawala Wetu Kinyume na Hivi
Mwingine kusema kwamba ulimwengu hauna uongozi mzuri leo ni taarifa duni. Tumekulia tukizoea watu wengi wanaojifanya wakidai uaminifu wetu, kuwa wao peke yao ndio wanaoweza kurekebisha mambo jinsi tunavyotaka yawe. Kampeni zao zimeundwa kuvutia hamu zetu msingi. Hakuna nafasi ya uaminifu, uadilifu, au mwinuko wa fikra, ambayo ni mambo muhimu ya uongozi bora; badala yake kampeni hizi zimejaa uongo, ndoto, uchochezi na ulafi.
Hiki, baada ya yote, ndicho kiini cha demokrasia. Haiwezi kamwe kuleta uongozi wenye heshima ambao huinua wanadamu kuelekea yaliyo mema. Demokrasia inaahidi kuweka tu watu mashuhuri madarakani, ambao wana ujuzi mkubwa wa kudanganya watu kutamani kila ambacho kikundi chao kinachouza.
Kinaya ni kwamba wasekula waliupa jina la urongo mfumo wao kama bidhaa ya "uangavu" wao wakati kwa kweli umepitiliza mno fikra zote angavu kutabanni maridhiano ambayo yangeruhusu wale ambao tayari wako madarakani kubaki madarakani, wakati wakitoa mifupa machache kwa kila mtu mwingine. Kwa kweli mifupa hiyo ubora wake ulikuwa kidogo kuliko makombo ya mara kwa mara yaliyotolewa na watawala wa Ulaya, hata hivyo ukweli unabaki kuwa mfumo huu mpya haikupimwa usahihi wake kwa msingi wa kiakili; bali tu juu ya jinsi ulivyoweza kuvutia maoni na matamanio ya watu masikini na wenye njaa. Mifupa hii ilikuwa ikivutia wakati huo, licha ya ukosefu wake wa dutu na lishe.
Je! Ni nini kinachoangazwa juu ya kuwafanya wanasiasa kuogopa kupoteza umaarufu wao, na kuwafanya kuwa wa muda mfupi katika mtazamo wao? Je! Ni nini kinachoangazwa juu ya kudhibiti uwajibikaji kwa kura kila baada ya miaka mitano, na kujitenga katikati ya kipindi hicho? Je! Ni nini kinachoangazwa juu ya kutegemea kampuni za vyombo vya habari kuwahesabu viongozi hawa? Kwa kuongezea, ni nini kinachoangazwa kabisa juu ya kuliepuka swali muhimu la uwepo, na kutabanni usekula kama maridhiano?
Ulimwengu unahitaji uongozi halisi ulioangazwa, ambao umejengwa juu ya fikra zilizoangazwa, sio fikra duni ya wingi. Badala yake tuna wagombea wadogo wanaotoa taarifa za mgawanyiko ili kuchochea kundi moja la ushabiki dhidi ya jengine. Nchini Uingereza, Ufaransa na Amerika, viongozi wanatoa matamshi ambayo yanavutia ngome zao za wafuasi, wakati hawawakasirikii madalali wa madaraka wanaodhibiti maslahi makubwa ya biashara. Trump anasimama na wabaguzi wa rangi ili kuendelea kubaki maarufu kwao, akidai kuvuruga kikundi cha Washington, huku Biden akidai kusimama na wanyonge. Kwa kweli, hakuna upande unaofanya kazi kwa ajili ya watu. Trump hajaboresha maisha ya wafuasi wake, wala kudhoofisha mshiko wa mashirika, na Obama na Biden hawakumaliza kabisa ubaguzi wa rangi nchini Amerika. Hakuna upande wowote uliokuwa tayari au kuweza kufanya kile walichoahidi, kwani hiyo lingehitaji uhakiki wa kina wa maoni na maadili yaliyoenea nchini Amerika. Ingehitaji utayari wa kuyaondoa matabaka yasiyostahili ya waliotononoka ambao wamejinyakulia mali na mamlaka kutoka kwa watu wa kawaida. Demokrasia ipo kulinda wachache kama hao, sio kuhatarisha msimamo wao.
Ulimwengu juu ya demokrasia umekuwa kichocheo kichounda virusi hatari kuwa janga la maambukizi ya kiulimwengu. Viongozi walikuwa wamepooza mno na hitaji lao kubaki maarufu, kwa hivyo walichelewesha, wakipendelea wafadhili wao matajiri, na wakakikanzana wenyewe kwa kila hatua. Matokeo yake, watu sasa wamechanganyikiwa ni njia ipi ya kuigeukia, wakiwa wamepoteza uaminifu wote kwa kizazi cha sasa cha watu maarufu na madai yao ya kupendeza. Sasa ndio wakati ambao mfumo unaoendelea kulisha mashine ya fikra ya wingi kuletwa mbele kwa ajili ya kuhojiwa.
Imani ya Kiislamu fikra kweli angavu kuhusu mwanadamu, maisha na ulimwengu, na sio suluhisho duni la kihistoria la maridhiano kati ya waasi wa Ulaya na watawala wao dhalimu. Uislamu hujibu swali la uwepo kwa njia inayokinaisha akili, kwani imejengwa juu ya uthibitisho wa kiakili, na inakubaliana na maumbile yetu ya kibinadamu. Imani ya Kiislamu ni msingi wa mifumo na mwongozo wa maisha juu ya jinsi ya kupanga uhusiano wetu na Muumba wetu, na nafsi zetu, na sisi kwa sisi, kiasi ya kuwa hakuna tabaka la waliotononoka kukandamiza kila mtu mwengine. Uislamu unakuza uongozi wa fikra kuliko kitu chengine chochote, kiasi ya kuwa fikra ya wingi haina nafasi. Uongozi wa Kiislamu sio wa muda mfupi katika mtazamo wake, kwani mtawala haogopi kuchaguliwa kwake tena, kwa hivyo ambayo ulimwengu haujawahi kuona kwa karne nyingi.
Haihitaji kabisa kusema kuwa viongozi waliochaguliwa na wasiochaguliwa katika ulimwengu wa Kiislamu leo wako mbali na dhana ya Kiislamu ya uongozi, kwani wote ni viamba wa Magharibi, walioajiriwa kuwatumikia warasilimali huko Magharibi, sio Uislamu na wala watu. Hizb ut Tahrir ni chama cha siasa cha Kiislamu kinachofanya kazi katika ulimwengu wa Kiislamu kunyanyua fikra katika jamii ili ulimwengu uweze kuona tena uongozi wa kweli uliojengwa juu ya msingi wa fikra angavu.
Tunawaalika kujisajili na kujiunga na Hizb ut Tahrir / Uingereza katika kongamano lake la kimataifa mtandaoni: Kurudi kwa Mfumo wa Kiulimwengu wa Kiislamu.
Wazungumzaji watahutubu mada zifuatazo:
Kutoka kwa Janga la Maambukizi hadi BLM: Wanadamu Wanatafuta Badali kwa Hamu
Uchumi Mpya, Usiotumikia Asilia Mia Moja
Nidhamu ya Khilafah, Utunzaji wa Watu
Kuasisi Uongozi wa Uislamu Duniani na Wajibu wetu
Jumamosi, 31 Octoba Saa Nane Mchana GMT
Jisajili katika
Yahya Nisbet
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Uingereza
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Uingereza |
Address & Website Tel: +44 (0) 7074 192400 www.hizb.org.uk |
E-Mail: media@domainnomeaning.com / press@hizb.org.uk |